Rapper Travis Scott ameonyesha yeye sio mtu wa mchezo mchezo hasa linapokuja jambo kuhusu mpenzi wake Kylie Jenner kutoka familia ya Kardashian.

Rapper Scott ameona isiwe shida amemtunuku mzazi mwenzake huyo ndinga mpya aina ya Ferrari, kama zawadi baada ya kumletea mtoto wa kike aitwaye Storm hivi karibuni.

Gari hiyo aina ya Ferrari yenye rangi nyeusi imekadiriwa kuwa na thamani ya kiasi cha dola milioni 1.2 sawa na kiasi cha shilingi bilioni mbili za Kitanzania.(2,697,263,826.90)

Kwa sasa wawili hao wamekuwa wakifatana kila waendapo na picha ya kwanza imenaswa wakiwa katika mtoko wao wa kula chakula cha mchana maeneo ya Nobu mjini Malibu, nchini Marekani.

Picha za gari hiyo ziliweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram wa mrembo huyo.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh