Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thierry Henry anasema angependa kuchukua nafasi yake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal (Sky Sports)

Chelsea ndio wako kifua mbele katika kumsaini mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski. Mchezaji huyo raia wa Poland anataka kujiunga na Premier League. (Sun)

AC Milan wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Swansea raia wa Korea Kusini Ki Sung-yueng, 29. (Calciomercato - in Italian)

Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Yacine Adli 27. Manchester City, Barcelona na Juventus pia wanamwinda raia huyo wa Ufaransa. (L'Equipe, via Sun)

Washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Philippe Coutinho wameidhinisha mipango ya klabu hiyo kuwaleta wachezaji watatu wapya msimu unaokuja. (Diario Gol - in Spanish)

Tottenham wanapanga kumsaini mshambulizi wa Sheffield United wa umri wa miaka 20 David Brooks. Klabu hiyo ya Premier League ina mpango wa kukubaliana pauni milioni 10 wa raia huyo wa Wales. (Sun)

0768671579

Add comment


Security code
Refresh