Kikosi cha Yanga kimeondoka hapo jana asubuhi kuelekea Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa barani afrika dhidi ya wenyeji St Louis.

Wakati wakiwa uwanja wa Ndege wa JKNIA Mwenyekiti wa kamati ya mashindano, Hussein Nyika amesema kikosi kimeelekea Shelisheli kikiwa na morari ya juu hasa baada ya matayarisho mazuri na ushindi mnono kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji.

Vijana wako fiti na wana morari ya hali ya juu tumefanya mazoezi ya kutosha kwa muda wa siku tatu, hapo kabla tulikuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji mchezo ambao mwalimu aliutumia kurekebisha makosa aliyoyaona kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya St Louis na sasa kikosi chake kiko kamili kwenda kumaliza kazi huko Shelisheli.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh