Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema wachezaji wake, Alexis Sanchez na Mesut Ozil wataendelea kusalia katika timu hiyo na kamwe hawatoondoka dirisha la usajili la mwezi Januari.

Meneja huyo wa The Gunners, Wenger amesema hakuna uwezekano wowote kwa wachezaji hao wa kimataifa wa Chile na Ujeruman kuondoka Emirates katika dirisha hili lijalo la usajili kutokana na makubaliano waliyoafikiana toka mwanzo mwa msimu.

Arsene Wenger ameyasema hayo wakati wakielekea katika mchezo wao wa hapo kesho dhidi ya Huddersfield “Huwa sifikirii kama wataondoka lakini kwakuwa bado wapo hapa tutalazimika kuwapatia kila mahitaji muhimu watakayo hitaji kupewa ndani ya klabu.

“Ndani ya kichwa changu ninachofahamu tutaendelea kuwa nao hadi mwishoni mwa msimu. Hayo nimaamuzi ambayo tumeyafanya tangu mwanzoni mwa msimu vinginevyo kutokee kitu kisichotarajiwa.”

0768671579

Add comment


Security code
Refresh