Wachezaji wa ligi ya soka Marekani kwa pamoja wameendelea kumpinga Rais Trump kwa kugoma kuimba wimbo wa Taifa la nchi hiyo katika mchezo wa Jumapili.

Walionekana wakiwa wameweka tu mikono vifuani ama mabegani mwa wachezaji wenzao huku wimbo huo ukiendelea.

Wengine walipiga magoti.

Cam Newton mchezaji nyota wa Carolina Panthers yeye alinyoosha mkono wake juu wakati wimbo huo ukiimbwa.

Hata hivyo mgomo wa wiki hii haukuwa na nguvu kama wa wiki iliyopita.

Katika mchezo baina ya Dallas Cowboys na Los Angeles Rams uliendelea bila ya mgomo wowote.

Trump ameandika katika mtandao wa Tweeter akiwataka viongozi wa chama cha soka Marekani kuwachukulia hatua wote waliohusika.

Mgomo huo ulianza mwaka jana baada ya mchezaji Colin Kaepernick wa San Francisco 49ers kuelezea namna raia weusi wa Marekani wanavyoteseka baada ya mlolongo wa kupigwa risasi na polisi.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh