Baada ya kutoa ngoma na Harmonize ‘Unaionaje’ kumekuwa na maswali mengi kutaka kujua iwapo msanii huyo amejiunga na label ya WCB licha ya hapo awali kutolea ufafanuzi suala hilo.

Kuendelea kusisitiza suala hilo Young Killer amesema, “kiukweli mimi sifanyi kazi katika label yoyote, nafanya kazi zangu mwenyewe lakini kuna watu ambao tunajaribu kushirikiana kufikisha muziki wetu pale ambapo tunahitaji kufika,” ameiambia Safari Redio na kuongeza.

“Nimeshawahi kufuatwa na menejimenti tofauti tofauti na mameneja wa kujitengemea mmoja mmoja, hatukuweza kufika muhafaka au makubaliano ya kuhakikisha mimi naweza kuwa chini yao, so hatukuweza kufanikisha hilo zoezi, nafanya kazi mwenyewe ila kuna watu tunajaribu kusaidiana na wanajaribu kuniongoza,” amesema Young Killer.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh