blog category

 

 

WACHEZAJI WA LIVERPOOL WAMUUNGA MKONO JAMES MILNER

Wachezaji wa klabu ya Liverpool wakiwa na wapenzi wao hapo jana siku ya Jumapili wamemuunga mkono mchezaji wa timu hiyo, James Milner katika sherehe ya taasisi yake ya kusaidia vijana yenye lengo la kukuza, kuendeleza na kutoa fursa kupitia michezo ya mpira ikiwemo Mpira wa miguu, Rugby na Kriketi katika kuimarisha afya zao.

James Milner mwenye umri wa miaka 31, anamiliki taasisi ya vijana ya michezo yenye lengo la kuimarisha afya zao.

Kati ya wapenzi walihudhuria hapo jana ni pamoja na straika wa Liverpool, Danny Ings akiwa na mpenzi wake Georgia Gibbs

Milner anaecheza nafasi ya winga, kiungo na beki wa kushoto ndani ya klabu ya Liverpool anamiliki taasisi hiyo inayojulikana kama Lost World Charity Ball ambayo hapo jana aliwaalika wachezaji wenzake pamoja na meneja Jurgen Klopp.

MUZIKI YA DARASSA YATEKA UFALME WA BONGO FLAVA NDANI YA MWAKA MMOJA

Novemba 23 ya mwaka 2016 ilikuwa ni siku ambayo Darassa aliweza kupata tobo kupitia ngoma yake ya ‘Muziki’.

Hakika wimbo huo uliteka Bongo Flava katika kipindi kifupi na kuanza kugeuka kuwa kama wimbo wa taifa.

Hii hutokea kwa nadra sana na tena kwa wasanii wachache tu wenye ngekewa zao.

Hali hii ilimfanya msanii huyo kama ni soka, basi alikuwa amepiga hat-trick na kuanza kubadili maisha yake kiulaini kwa kupata show lukuki kila kukicha.

Bila promo kubwa kufanywa wimbo huo uliweza kutoboa na kupenya kwenye masikio ya watu wa rika zote.

Lakini kubwa zaidi wimbo huu mpaka sasa umetimiza mwaka mmoja na umefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 10 katika mtandao wa Youtube.

Huu umekuwa wimbo wa kwanza wa msanii wa Hip Hop hapa Bongo kutazamwa mara nyingi zaidi lakini pia umeweza kutikisa mpaka video nyingi za wasanii wa kuimba ambazo nyingi bado hazijafikia level za ‘Muziki’.

Huwezi kuamini video hii imezizidi mpaka ngoma nyingine zikiwemo za wasanii wa WCB ambao ndio wanaonekana kutazamwa zaidi kutokana na kuwa na wingi wa mashabiki wanaowapa support.

Kutoka WCB ni video kadhaa za Diamond na ngoma ya ‘Bado’ ya Harmonize ndio zimefanikiwa kutazamwa mara nyingi zaidi ya wimbo huo wa Darassa.

Lakini kwa upande wa Alikiba ni ngoma yake ya ‘Mwana’ pekee ambayo ilitoka takribani miaka miwili iliyopita na kutazamwa mara milioni 17 ndio imefanikiwa kuizidi ‘Muziki’ ya Darassa.

BATE BORISOV WASHINDA LIGI DAKIKA YA 96 BELARUS

Bate Borisov walifanikiwa kushinda taji la ligi kwa mara ya 12 mtawalia nchini Belarus kwa njia ya kipekee - kwa kufunga bao dakika ya 96.

Dinamo Minsk, ambao walikuwa wanashindania taji hilo walikuwa wameshinda mechi yao 4-1 na walikuwa na kila matumaini ya kutwaa ubingwa kwani Bate Borisov walikuwa nyuma mechi yao.

Lakini bahati yao haikusimama. Mirko Ivanic alifunga bao la kusawazisha dakika ya 96 na kufanya mambo kuwa 3-3 wakiwa ugenini dhidi ya Gorodeya.

Sare yao iliwasaidia kushinda ligi kwani walikuwa wamewazidi nguvu Dinamo klabu hizo zilipokutana.

Klabu zote mbili zilimaliza ligi zikiwa na alama 68.

Tofauti ya mabao ya Bate ni +42 nao Dinamo walikuwa na +31.

Dinamo Minsk mara ya mwisho walishinda ligi 2004.

Shakhtyor Soligorsk ilikuwa klabu ya mwisho, kando na Bate, kushinda taji hilo, mwaka 2005.

Dinamo walikuwa wameshinda msimu uliotangulioa.

Bate walikuwa nyuma 3-1 mechi yao wakati mmoja kabla ya kufungiwa penalti na Vitali Rodionov mechi ikiwa imesalia na dakika 12 muda wa kawaida.

Kwa sasa wanashika mkia Kundi H katika Europa League na wanahitaji kulaza Arsenal tarehe 7 Desemba ndipo wawe na matumaini ya kusonga kutoka hatua ya makundi.

YANNICK BOLLASIE WA EVERTON ARUDI KATIKA MAZOEZI

Mshambuliaji wa Everton Yannick Bolasie amerudi katika mazoezi baada ya miezi 11 akiuguza jeraha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata jeraha baya wakati klabu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United mnamo mwezi Disemba 4, 2016 na hadi kufikia sasa amefanyiwa upasuaji mara mbili.

Raia huyo wa DR Congo alifanya mazoezi na timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 wiki iliopita kabla ya kujiunga na kikosi kikuu siku ya Jumatano.

Klabu hiyo imesema kuwa alipokea pongezi kutoka kwa wachezaji wenza baada ya kurudi.

Bolasie ameichezea klabu hiyo mara 15 tangu ahamie kutoka Crystal palace 2016.

HUDDAH MONROE AMKINGIA KIFUA MTOTO WA MUGABE

Kuna nini kati ya mtoto wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zimbabwe, Chatunga Bellarmine Mugabe na Huddah Monroe.

Mrembo huyo wa Kenya ameandika ujumbe kupitia mtandao wa Snapchat, kumkingia kifua mtoto huyo ambaye anaonekana kuchukiwa na watu wengi kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa hivi karibuni kabla ya Rais Mugabe kutangaza kujiuzulu.

Huu ni ujumbe wa Huddah ambao ameandika kwenye mtandao huo.

JORDIN SPARKS NA MUMEWE DANA ISAIAH WATARAJIA KUPATA MTOTO WA KWANZA

Jordi Akiongea na People, msanii huyo ambaye pia aliwahi kuwa mshindi wa shindano la American Idol katika msimu wa sita mwaka 2007, amethibitisha kuwa ni mjamzito kwa sasa.

“We’re both really excited. He’s been like, ‘I want to shout it from the mountain tops!’ We’re really proud to be married to each other and to be celebrating this. It was about five days after he moved to L.A. He comes in and I go ‘I’m pregnant.’ It was such a shock for both of us. I turned around and started bawling in the closet,” amesema Jordin.

Msanii huyo ameongeza kwa kusema, “Once we got over the initial shock of it, now again just like it is with the marriage, to be able to share that this amazing thing is happening, it’s such a great thing. We did this together!.”

Wawili hao walifunga ndoa yao ya siri Julai 16 ya mwaka huu huko Hawaii n Sparks na mumewe ambaye ni mwanamitindo Dana Isaiah wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

USAJILI: AZAM FC YANASA SAINI YA STRAIKA GHANA

Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imemsajili mshambuliaji, Bernard Arthur akitokea Liberty Professional ya Ghana.

Arthur amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex, na zoezi zima limefanikishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed, aliyekuwepo nchini Ghana kukamilisha usajili wake.

Usajili wa Arthur mwenye umri wa miaka 20, ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo kwenye usajili huu wa dirisha dogo, anayekuja kuziba pengo la straika mwingine, Yahaya Mohammed, aliyeondoka kwa makubaliano maalumu ya pande mbili wiki chache zilizopita.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya WAFA (Ghana) na Asec Mimosa ya Ivory Coast, anaungana na washambuliaji wengine wa timu hiyo katika kukiongezea makali kikosi hicho, ambao ni Mbaraka Yusuph, Wazir Junior, Yahya Zayd, Shaaban Idd pamoja na wale waliopandishwa kutoka Azam B, Paul Peter na Andrea Simchimba.

Liberty Professional ni moja ya kitovu kikubwa cha kutoa mastaa wa baadaye nchini Ghana, wachezaji waliotesa barani Ulaya waliowahi kupitia hapo ni nyota wa zamani wa Chelsea, Michael Essien, Sulley Muntari (Pescara, Italia) na Asamoah Gyan (Kayserispor, Uturuki).

Azam FC inamatumaini makubwa kuwa usajili wa nyota huyo, utaweza kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji na kutatua tatizo la ukosefu wa mabao linaloonekana, hii ikitarajia kuendeleza mbio za kuwania taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania walizozianza vema hadi sasa.

Arthur aliyekuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya vijana ya Ghana chini ya umri wa miaka 20 (Ghana U-20), ni mmoja wa washambuliaji bora kwa sasa katika Ligi Kuu nchini Ghana (GPL), msimu huu akifunga jumla ya mabao 11, tisa akifunga ndani ya ligi hiyo na mawili (Kombe la FA).

Moja ya sifa zake kubwa ni uwezo wa kumiliki mpira na kuwatoka mabeki wa timu pinzani kwa spidi, kukaa na mipira na kusambaza kwa wachezaji wenzake, kutumia vizuri miguu yote miwili, uwezo wa kupiga mashuti kwenye eneo lolote la ushambuliaji pamoja na kusaidia ukabaji pale timu pinzani inapokuwa ikishambulia.

Arthur alianzia soka lake katika timu ya Mighty Cosmos kwenye eneo alilozaliwa na kukulia la Dansoman nchini Ghana, akiwa kijana mdogo mwaka 2005-2010.

Cosmos aliyoanzia soka lake Arthur, pia wamewahi kucheza nyota wengi wa soka la Ghana wakiwamo nahodha wa zamani na timu ya Taifa ‘Black Star’, Stephen Appiah na Michael Essien.

Mbali na kucheza Liberty, mshambuliaji huyo pia amewahi kucheza kwa mabingwa wa msimu uliopita nchini Ghana, WAFA huku pia akiwahi kutolewa kwa mkopo kujiunga na vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosa.

Nyota huyo anavutiwa na staa wa Ghana, Asamoah Gyan, ambaye ndiye mfano wake wa kuigwa (role model), ambapo anapenda siku moja wacheze naye pamoja katika timu Taifa.

KENDRICK LAMAR AUPELEKA MUZIKI WA HIP HOP KATIKA JARIDA LA ‘FORBES’ ’30 UNDER 30′

Unapozungumizia moja ya rapper wanaofanya vizuri kwa sasa basi huwezi kuacha kumtaja, Kendrick Lamar kuwa ni moja ya rapper bora kwa sasa na hata baadae.

Mshidi huyo wa tuzo za ‘Grammy’ na mkali wa albamu ya ‘DAMN’ iliyotoka mwaka huu na kufanya kudhihirisha ukali wake ameng’ara katika jarida hilo kubwa la Forbes ’30 under 30′ akiwa mstari wa mbele kabisa huku akiwa na mwanadada Cardi B wakizungumzia muziki wa Hip Hop.

Kwa upande wa Lamar ambaye amekava jarida hili linalotarajiwa kutoka mwaka 2018 amezungumzia ni jinsi gani muziki huo umeweza kumuingizia mtonyo, huku mwanadada Cardi B yeye akiweka bayana juu ya ngoma yake ya ‘Bodak Yellow’ ilivyoweza kuweka historia katika chati za Billboard Hot100.

Jarida hilo pia limeweka mastaa wengine wanaofanya poa katika muziki ambao ni:

Lil Uzi Vert (23)

SZA (28)

Young M.A. (25)

Travis Scott (26)

Young Thug (26)

Migos (Takeoff – 23, Offset – 26, and Quavo – 26)

H.E.R. (20)

Khalid (19)

Mike Posner (29)

Bebe Rexha (28)

producer WondaGurl (21)

Beyoncé choreographer JaQuel Knight (28) na wengineo

Page 2 of 67