SPORTS & ENTERTAINMENT

 

 

ALEXIS SANCHEZ AKINUKISHA ,ARSENAL IKIILAZA FC COLOGNE

Alexis Sanchez aliisaidia Arsenal kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Ujerumani Cologne katika mechi ya Yuropa iliocheleweshwa kwa saa moja kutokana na matatizo ya mashabiki.

Sanchez ambaye karibia aihame klabu hiyo ili kujiiunga na Manchester City katika siku ya mwisho ya uhamisho , aliuchukua mpira nje ya eneo hatari na kuupinda huku kipa Timo akishindwa kuokoa mkwaju huo.

Mechi hiyo hatahivyo haikuanza katika muda iliopangiwa baada ya maelfu ya mashabiki wa Cologne kuwasili katika uwanja wa Emirates bila tiketi na baadaye kuzozana na wanaowakaribisha wageni ndani ya uwanja huo.

Na mechi ilipoanza , Cologne ilichukua uongozi baada ya Jhon Cordoba kumfunga kipa David Ospina akiwa maguu 40.

Mshambuliaji Olivier Giroud alipiga nje kichwa cha wazi akiwa maguu sita pekee karibu na goli .

Lakini mchezaji wa ziada Sead Kolasinac alisawazisha kabla ya Sanchez kufunga bao la pili.

Beki wa kulia wa Arsenal Hector baadaye alifunga bao la tatu huku kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere akiichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza tangu Agosti 2016.

BLAC CHYNA KUACHIA ALBAMU YAKE YA KWANZA

Kwa kumuangalia Blac Chyna unafikiria mbali na kazi ya video vixen ni kitu gani kingine anaweza kufanya?

Basi mrembo huyo anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza ambayo amerap.

Inadaiwa kuwa katika albamu hiyo Chyna amepata msaada kutoka kwa wakali wa rap kama Yo Gotti, Tory Lanez, Jeremih na Swae Lee.

Mally Mall ambaye pia amewahi kufanya kazi na rapper Tyga, ametajwa kuandaa albamu hiyo.

Duru za habari kutoka nchini humo, zinadai kuwa Nicki Minaj ndio amemvuta Blac kuingia kwenye muziki.

MOROCCO NA KENYA ZAWIKA VOLBALL YA WALEMAVU RWANDA

Mashindano ya voliboli ya walemavu kuwania ubingwa wa Afrika yameingia katika siku yake ya pili leo mjini Kigali timu ya Morocco ikiwa ya kwanza kujihakikishia tiketi ya robo fainali.Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema timu ya Morocco imeendelea kuonyesha umahiri katika mashindano hayo.

Mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita Morocco imeilima Afrika Kusini seti 3-0.Ushindi huu unafuatia ushindi mwingine wa jana Morocco ilipoizaba Kenya seti 3-0 za 25-21,25-19 na 25-18.

Mchezaji wa Kenya James Mang'erere akakiri kuzidiwa maarifa.Jana usiku pia Rwanda ilikandika Afrika kusini seti 3-0 25-10,25-16 na 25-17.Upande wa wanawake Misri ilichapwa na Kenya seti 3-2 huku Rwanda ikiichalaza DRC seti 3-0.

Mnamo mechi za leo, inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Rwanda na Kenya wanaume, mechi inachezwa usiku huu.

TOTTENHAM, MADRID ZAONESHA UBABE UEFA, LIVEPOOL YAZUIWA

Mshambuliaji Harry kane alifunga mabao mawili huku Tottenham ikiishinda Borussia Dortmund na hivyobasi kupiga jeki matumaini yao ya kombe la vilabu bingwa Ulaya katika uwanja wa Wembley.

Umahiri wa kane mbele ya goli ndio tofauti kubwa waliokuwa nayo Suprs ambao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo walilazimika kulinda lango la kutokana na mchezo mzuri ulioonyeshwa na vijana wa Dortmund.

Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba na mpira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.

Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motisha ya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.

Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya beki Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.

GENNADY 'GGG' GOLOVKIN KUZICHAPA DHIDI YA SAUL 'CANELO' ALVAREZ

Pigano la uzani wa middleweight kati ya Gennady 'GGG' Golovkin dhidi ya Saul 'Canelo' Alvarez limetajwa kuwa la aina yake ikilinganishwa na lile lililodaiwa kuwa na mbwembwe kati ya Floyd Mayweather na bingwa wa UFC Conor McGregor.

Tayari tiketi zote za pigano hilo la Jumamosi zimeuzwa kwa £18,000 kila moja huku mataji mawili ya uzani wa middleweight yakipiganiwa na kuwa mojawapo ya mapigano yaliotarajiwa na wengi mjini Las Vegas.

Canelo Alvarez ambaye ameshindwa mara moja pekee katika mapingano zaidi ya 50 aliyoshiriki huku GGG akiwa hajashindwa katika mapigano yake yote na ndiye anayeshikilia mataji ya IBF na IBC katika uzani huo.

Kulingana na duru za pigano hilo Alvarez amelitaja kuwa pigano 'hatari' zaidi katika historia ya mapigano aliyoshiriki.

Hii ni taarifa yenye maana kubwa kwa bondia wa umri wa miaka 27 ambaye ameipigana ndondi za kulipwa kwa takriban miaka 12 huku akipoteza pigano moja pekee kwa aliyekuwa bingwa wa zamani katika uzani huo Floyd Manny Mayweather 2013.

Hatahivyo Canelo ambalo jina lake linamaanisha 'mdalasini' kutokana na nywele zake nyekundu alikuwa akivutia wengi kwani pigano lake la Mayweather limetajwa kuwa pigano la tatu kuu lililovutia kiwango cha juu cha watazamaji katika historia ya mchezo huo.

PAUL POGBA: KUKAA NJE WIKI SITA KUTOKANA NA JERAHA

ujao.

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba huenda akakaa nje ya uwanja kwa kati ya mwezi mmoja na wiki sita baada yake kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Basel Jumanne.

Mfaransa huyo wa miaka 24 alifanyiwa uchunguzi kuhusu jeraha hilo Jumatano.

Inafahamika kwamba Pogba atakosa kucheza angalau kwa mwezi mmoja.

Hilo lina maana kwamba huenda atakuwa na kibarua kujaribu kuwa sawa kucheza mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Liverpool ugenini 14 Oktoba.

Meneja wa United Jose Mourinho anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake katika kikao na wanahabari Ijumaa.

Pogba atakosa mechi za ligi dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu Jumatano dhidi ya Burton.

Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.

Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.

Ufaransa wanahitaji kushinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka

ARIANA GRANDE ALAMBA DILI NA KAMPUNI YA REEBOK

Mrembo huyo ambaye ana followers milioni 113 kwenye mtandao wake wa Instagram, amepata dili hilo kwa ajili ya kutangaza bidhaa za kampuni hiyo.

Grande ameonyesha kufurahishwa na mkataba huo kwa kuandika kupitia mtandao wake wa Instagram, “Confidence, self belief and self expression ?♡? I am proud to partner with @Reebok who has the same ideals and beliefs as me & that I hope to instill in my babes ?#BeMoreHuman #ArianaxReebok.”

Msanii huyo sio wa kwanza kusaini mkataba na kampuni hiyo, wengine waliowahi kufanya kazi na Reebok ni pamoja na Kendrick Lamar, Future, Rick Ross na Rae Sremmurd.

BARCELONA YAIZABA JUVENTUS BAKORA 3-0

Mabao mawili ya Lionel Messi yalitosha kuisaidia Barcelona kuiadhibu Juventus mabao 3-0 katika uwanja wa Nou Camp.

Messi alifunga bao la kwanza baada ya kupa ni kupe na mshambuliaji Luis Suarez.

Ivan Rakitic aliifungia Barcelona bao la pili baada ya shambulio la Messi kuokolewa katika laini ya goli.

Mshambuliaji huyo wa Argentina baadaye alihakikisha kuwa timu yake inachukua ushindi dhidi ya Juventus walioshiriki katika fainali ya kombe hilo mwaka uliopita baada ya kufunga bao zuri kwa kutumia mguu wake wa kushoto kwa umbali wa maguu 20.

Akicheza mbele ya mabeki wa Juve, Messi aliwachenga mabeki waliokuwa wakimkaba kabla ya kumwacha kipa wa miaka mingi Gianluigi Buffon bila jibu.

Page 10 of 70