blog category

 

 

MENEJA WA CRYSTAL PALACE APIGWA KALAMU

Meneja wa Crystal Palace amepigwa kalamu na klabu hiyo baada ya kuongoza michezo mitano.

The Eagles wako katika nafasi ya 19 katika ligi ya Premia kwa kupoteza kwa Burnley 1-0 siku ya Jumapili. Crystal ilishindwa kufunga bao lolote latika mechi zao nne za ligi chini ya meneja De boer.

Meneja huyo wa zamani wa Ajax , De Boer , 47 alichukua kazi hiyo ya umeneja mwanzoni mwa msimu huu, baada ya Sam Allardyce aliyeiaga timu hiyo baada ya kuwaepesha katika hatua ya kushushwa daraja msimu uliopita.

HATUHUSIKI NA MABADILIKO YA RATIBA: SIMBA

SIKU mbili baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), kutoa ratiba mpya ya Ligi Kuu iliyofanyiwa marekebisho, uongozi wa klabu ya Simba umesema haijashinikiza mabadiliko hayo kama inavyodaiwa na baadhi ya wadau wa soka.

Baada ya TFF kusogeza mbele michezo iliyokuwa ichezwe leo ikiwamo mechi yao dhidi ya Azam na kusogezwa hadi Jumamosi, baadhi ya mashabiki walilalamika kuwa mabadiliko hayo yamelenga kuisaidia Simba ambao wanasubiri kurejea kwa nyota wao wa wawili, Juuko Murshid na Emmanuel Okwi waliopo kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda ambacho leo kinacheza na Misri.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema Simba haihusiki na mabadiliko hayo ya ratiba ya ligi.

“Huku ni kushinikiza mambo, naomba niweke wazi klabu ya Simba haihusiki na mabadiliko haya, watu wanaosema mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuisaidia Simba ni wazushi na si wanamichezo,” alisema Manara.

Alisema wanaamini mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na ratiba ya awali kuingiliana na michezo ya kimataifa ya Kalenda ya Shirikisho la Soka duniani (Fifa).

“Taratibu zinataka kunapokuwapo na mashindano ya Fifa, hakupaswi kuwa na michezo mingine ya ligi, tunaona hili hata kwa wenzetu Ulaya sasa sisi Simba tunaingizwaji hapo,” aliongeza kusema Manara.

Mabadiliko ya Ratiba yanaonyesha Simba itaifuata Azam kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex Jumamosi ijayo huku pia mchezo wao dhidi ya watani zao, Yanga ukisogezwa mbele kwa wiki mbili kutoka Oktoba 14 mpaka Oktoba 28, mwaka huu.

MANVIR SINGH ATAMBA KATIKA MASHINDANO YA MAGARI RWANDA

Mashindano ya mbio za magari ya Rwanda mountain Rally yanaendelea huku dereva kutoka Kenya Manvir Singh akiendelea kutamba.

Manvir Singh akiendesha gari lake aina ya skoda ameshinda awamu zote zilizochezwa mwishoni mwa Juma na kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa wa mashindano haya hata kutwaa taji la afrika.

Magari 10 ndiyo yamesalia katika mashindano hayo yaliyoanza Ijumaa yanayoshirikisha washindani 16.

Gari hilo aina ya Skoda ndiyo gari ya kisasa miongoni mwa magari yanayotumiwa katika mashindano ya mbio za magari bei yake ikiwa ni 280.000 USD kulingana na Dereva huyo.

Dereva huyo kutoka Kenya Manvir Singh akiwa anahitaji alama 25 za shindano hili la Rwanda ili kutangazwa bingwa wa Afrika kabla hata ya shindano la mwisho litakalofanyika Zambia. Mbio za Jumamosi ni za urefu wa km 140 zikizunguka katika barabara mbovu za upande wa kusini mashariki mwa Rwanda.

Jumla ya magari 16 yameshiriki mashindano haya ya siku tatu.

HARMORAPA KUJIFUNZA KIINGEREZA

Mwanamziki wa bongo fleva asiyekaukiwa matukio, Harmorapa anatarajia kuanza kujinoa katika suala zima la Lugha ya Kingereza kwa mtaalam wa kufundisha lugha hiyo, James Mramba ‘Mr. English’.

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kuona kuna fursa anaikosa katika suala zima la kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali hususan atakapokwenda kupiga shoo nje ya nchi.

“Nimeamua kujifunza Kingereza na sehemu sahihi kwangu ni kwa Mr. English kwa sababu anatoa huduma za mobile.

Atanifuata nyumbani, najifunza private,” alisema Harmorapa. Mr. English anatoa huduma hiyo katika ofisi yake iliyopo Sinza-Mapambano .

UJUMBE WA HAMISA MOBETTO KWENYE BIRTHDAY EX WAKE MAJAY WAZUA GUMZO

Jumamosi hii bosi wa kituo cha EFM, Majay amesherekea siku yake ya kuzaliwa – Hamisa Mobetto ambaye pia ni ex wake hakubaki nyuma kumuandikia ujumbe mzuri.

Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameandika “Happy Birthday Baba Fantasy … Ahsante Kwa kua Baba bora Na zaidi Kwa Mwanetu.

M/Mungu Akutunze, Akulinde Na Akuzidishie Maendeleo Tele . Tunakupenda sana & Thank you for always being here 🙏🏾💕#coparentingatitsfinest @majizzo.”

Majay na Hamisa waliwahi kuwa na mahusiano ambapo walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike kabla ya kuachana.

TUNDA ATOLEA POVU PICHA ZA UTUPU

Mrembo machachari Bongo, Tunda Sebastian amewapa makavu mamodo wanaoibuka kwa staili ya kupiga picha za utupu akisema fasheni hiyo hivi sasa imefeli, hivyo ni bora wakitafuta namna nyingine ya kutoka.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Tunda alisema wasichana wanaokuja na kudhani kuwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni kutawafanya wawe maarufu, wamechemsha kwa sababu wanachokifanya ni ujinga uliopitiliza.

“Ninachokiona hapo ni upumbavu tu na tamaa ya umaarufu bila kutafakari madhara yake, kifupi watafute plan B maana A imefeli na kuwadhalilisha,”alisema.

Z ANTO AACHIA WIMBO MAALUMU WA KUMUOMBEE AFYA NJEMA LISSU (AUDIO)

Msanii mkongwe wa Muziki, Z Anto ameingia studio na kurekodi wimbo maalumu kwaajili ya kumuombea afya njema Mbunge wa Singida kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu aliyelazwa nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma muda mchache akitokea Bungeni.

Z amesema amefanya wimbo huo maalumu ili kuwahimiza watanzania kuendelea kumuombea mwanasiasa huyo mpaka pale afya yake itakapo kuwa fiti.

“Dua ndio kila kitu kwa sasa, watanzania wote kwa dini zetu, tuungane kumuombea afya njema ndugu yetu kwa sababu tukio lililomkuta sio la kawaida kabisa katika maisha yetu ya kawaida,” alisema Z Anto.

Muimbaji huyo amedai alikuwa na mpango wa kuachia wimbo wake mpya wiki hii lakini amesitisha mpango huo na kuamua kuandaa wimbo maalumu ambao utawafanya watanzania kuombea afya njema Lissu.

WANAWAKE NCHINI IRAN WAPIGWA KITANZI KUHUDHURIA MECHI KATI YA IRAN NA SYRIA

Wanawake nchini Iran walizuiwa kuingia uwanja wa kitaifa ambapo timu ya taifa ya nchi hiyo ilikuwa ikicheza mechi ya kufuzu kombe la dunian dhidi ya Syria licha ya wao kuwa na tiketi.

Wanawake hao walikusanyika nje ya uwanja wa Azadi mjini Tehran kulalamika wakati waliamrishwa kuondoka, huku wanawake raia Syria wakiruhusiwa kuingia uwanjani bila tatizo lolote baada ya kuonyesha paspoti zao.

Wanawake wamepigwa marufuku ya kuhudhuria mechi za kandanda ya wanaume nchini Iran.

Wanawake kadha walikuwa wamenunua tiketi kwa njia ya mtandao wiki moja mapema kabla ya mechi.

Lakini shiriko la kandanda nchini Iran lilisema kuwa tiketi hizo ziliuzwa kimakosa na kuahidi kuwarejeshea pesa wanawake ambao walikuwa tayari wamezinunua.

Wale waliokuwa na tiketi hata hivyo waliamua kuelekea uwanjani jana Jumanne wakitaka kujaribu ikiwa wangeruhusiwa kuingia.

Page 9 of 67