blog category

 

 

ARIANA GRANDE ALAMBA DILI NA KAMPUNI YA REEBOK

Mrembo huyo ambaye ana followers milioni 113 kwenye mtandao wake wa Instagram, amepata dili hilo kwa ajili ya kutangaza bidhaa za kampuni hiyo.

Grande ameonyesha kufurahishwa na mkataba huo kwa kuandika kupitia mtandao wake wa Instagram, “Confidence, self belief and self expression 💡♡🌙 I am proud to partner with @Reebok who has the same ideals and beliefs as me & that I hope to instill in my babes 🌩#BeMoreHuman #ArianaxReebok.”

Msanii huyo sio wa kwanza kusaini mkataba na kampuni hiyo, wengine waliowahi kufanya kazi na Reebok ni pamoja na Kendrick Lamar, Future, Rick Ross na Rae Sremmurd.

BARCELONA YAIZABA JUVENTUS BAKORA 3-0

Mabao mawili ya Lionel Messi yalitosha kuisaidia Barcelona kuiadhibu Juventus mabao 3-0 katika uwanja wa Nou Camp.

Messi alifunga bao la kwanza baada ya kupa ni kupe na mshambuliaji Luis Suarez.

Ivan Rakitic aliifungia Barcelona bao la pili baada ya shambulio la Messi kuokolewa katika laini ya goli.

Mshambuliaji huyo wa Argentina baadaye alihakikisha kuwa timu yake inachukua ushindi dhidi ya Juventus walioshiriki katika fainali ya kombe hilo mwaka uliopita baada ya kufunga bao zuri kwa kutumia mguu wake wa kushoto kwa umbali wa maguu 20.

Akicheza mbele ya mabeki wa Juve, Messi aliwachenga mabeki waliokuwa wakimkaba kabla ya kumwacha kipa wa miaka mingi Gianluigi Buffon bila jibu.

BLAC CHYNA KUACHIA ALBAMU YAKE YA KWANZA

Kwa kumuangalia Blac Chyna unafikiria mbali na kazi ya video vixen ni kitu gani kingine anaweza kufanya?

Basi mrembo huyo anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza ambayo amerap.

Inadaiwa kuwa katika albamu hiyo Chyna amepata msaada kutoka kwa wakali wa rap kama Yo Gotti, Tory Lanez, Jeremih na Swae Lee.

Mally Mall ambaye pia amewahi kufanya kazi na rapper Tyga, ametajwa kuandaa albamu hiyo.

Duru za habari kutoka nchini humo, zinadai kuwa Nicki Minaj ndio amemvuta Blac kuingia kwenye muziki.

SHABIKI AINGIA UWANJANI NA KUJARIBU KUMPIGA TEKE MBAPPE WA PSG

Klabu ya Celtic imeshtakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya shabiki mmoja kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.

Kisa hicho kilitokea katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo siku ya Jumanne muda mfupi baada ya wageni hao kuwafunga Celtic bao la tano.

PSG pia inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanja huo.

Kesi hiyo itaangaziwa na kitengo cha maadili na nidhamu katika shirikisho la Uefa tarehe19 Octoba.

Mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya mashabiki kumzomea jamaa huyo aliyeingia uwanjani.

Nadhani hatua iliochukuliwa na mashabiki kumzoma jamaa huyo ilikuwa jibu zuri.

Inakatisha tamaa katika uwanja wowote wa klabu yoyote unapoona shabiki anaingia katika uwanja kama alivyofanya.

TOTTENHAM, MADRID ZAONESHA UBABE UEFA, LIVEPOOL YAZUIWA

Mshambuliaji Harry kane alifunga mabao mawili huku Tottenham ikiishinda Borussia Dortmund na hivyobasi kupiga jeki matumaini yao ya kombe la vilabu bingwa Ulaya katika uwanja wa Wembley.

Umahiri wa kane mbele ya goli ndio tofauti kubwa waliokuwa nayo Suprs ambao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo walilazimika kulinda lango la kutokana na mchezo mzuri ulioonyeshwa na vijana wa Dortmund.

Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba na mpira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.

Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motisha ya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.

Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya beki Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.

BARNABA AMMISI MAMA MTOTO WAKE

Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amefunguka na kudai anam-miss sana mama Steve 'Zuu Namela' japokuwa kwa sasa hayupo tayari kumrudia mzazi mwenzake huyo.

Msanii Barnaba akiwa na mama Steve 'Zuu Namela' enzi hizo mapenzi yakiwa moto moto kabla ya kuachana kwao.

Barnaba ameeleza hayo baada ya kupita muda mrefu tokea aachane na mzazi mwenzake huyo na kupelekea kuwa single mpaka kipindi hiki.

"Sitaweza kurudiana na mama watoto wangu japo nam-miss sana", amesema Barnaba.

Aidha, Barnaba amesema kwa upande wake mapenzi hayajawahi kumuendesha hata kidogo kama baadhi ya watu wengine wanavyokuwa baada ya kuachana na wapenzi wao kwa kushindwa hata kuendelea kufanya kazi zao.

Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "Kila unachokiona kinatokea katika maisha yako kiwe kizuri au kibaya ni mapito tu, kwa sababu kilichotuleta duniani ni kingine na tunachokifanya ni kingine kwa hiyo muda mwingine kutendwa na vitu vingine ni kutenda dhambi zaidi 'so sometimes' unatakiwa upokee kwa furaha chochote utakachokumbana nacho katika maisha yako, kwa sababu hujui mpango wa Mungu ukoje.

Ninachoamini mimi ni kwamba nilikuwa napita kwenye daraja ili niweze kuendela na safari aliyopanga Mungu 'so' sijui 'next' nilichopangiwa na Mwenyezi Mungu", amesisitiza Barnaba.

Kwa upande mwingine, Barnaba japo wameachana na Zuu lakini bado wanamawasiliano mazuri baina yao na kudai hivi karibuni aliongea naye kuulizia maendeleo ya Steve ya kimasomo na kumtumia pesa kwa ajili ya matumizi ya shule.

PAUL POGBA: KUKAA NJE WIKI SITA KUTOKANA NA JERAHA

ujao.

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba huenda akakaa nje ya uwanja kwa kati ya mwezi mmoja na wiki sita baada yake kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Basel Jumanne.

Mfaransa huyo wa miaka 24 alifanyiwa uchunguzi kuhusu jeraha hilo Jumatano.

Inafahamika kwamba Pogba atakosa kucheza angalau kwa mwezi mmoja.

Hilo lina maana kwamba huenda atakuwa na kibarua kujaribu kuwa sawa kucheza mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Liverpool ugenini 14 Oktoba.

Meneja wa United Jose Mourinho anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake katika kikao na wanahabari Ijumaa.

Pogba atakosa mechi za ligi dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu Jumatano dhidi ya Burton.

Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.

Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.

Ufaransa wanahitaji kushinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka

HALI YA MC PILIPILI YA ZUNGUMZIWA KILA KONA NCHINI

Hali ya mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu Mc Pilipili aliyepata ajali ya gari bado haijaimarika, imeelezwa.

Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikolazwa Mc Pilipili, Lucy Joseph amesema yupo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu akisubiria kufanyiwa vipimo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi.

Amesema ajali hiyo ilitokea jana Jumanne saa kumi jioni katika Barabara ya Mwanza – Shinyanga.

Haule amesema ndani ya gari aina ya Toyota Prado mali Mc Pilipili walikuwa watu watatu.

Kamanda Haule amesema dereva wa gari hilo alikuwa Saidi Hassan (28), mkazi wa Dar es Salaam na walikuwa wakitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

Gari hilo amesema liliacha njia na kupinduka na kwamba, Mc Pilipili amepata majeraha sehemu mbalimbali mwilini ikiwemo kifuani.

Kamanda Haule amesema dereva alipata michubuko mkono wa kulia.

Katibu Muhtasi wa Kampuni ya Pilipili Events, Stella Maswenga alisema jana kuwa walipokea taarifa za ajali hiyo jana Jumanne jioni.

Maswenga amesema Mc Pilipili alialikwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusherehesha harusi wikiendi iliyopita.

Page 8 of 67