blog category

 

 

HATIMAYE WANYAMA AMEJIUNGA NA TOTTENHAM HOTSPURS

Baada ya kiungo wa kimataifa wa Kenya na nahodha wa Harambee Stars aliyekuwa anaichezea klabu ya Southampton ya England Victor Wanyama mwenye umri wa miaka 24 kuhusishwa kwa muda mrefu kutaka kujiunga na Tottenham Hotspurs, amemaliza rasmi uvumi huo.

Wanyama ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga na Tottenham Hotspurs kwa zaidi ya wiki mbili, amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Tottenham Hotspurs, kwa ada ya uhamisho ambayo ni siri pande zote mbili hawajaweka wazi.

Wanyama alikuwa akitajwa atajiunga na Tottenham Hotspurs kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 11, ambazo ni zaidi ya bilioni 35 za kitanzania. Taarifa hizo zinakuwa njema kwa Afrika Mashariki, kwani staa huyo pekee Afrika Mashariki katika Ligi Kuu Englandatapata nafasi ya kucheza UEFA Champions League msimu ujao.

ANDY MURRAY AREJEA KWA KOCHA WAKE WA ZAMANI

Mchezaji Tenisi Andy Murray hatimaye anaungana tena na kocha wake wa zamani Ivan Lendl kabla ya michuano ya Aegon .

Murray mwenye miaka 29, amekuwa bila kocha huyo muda mfupi kabla ya kuanza kwa michuano ya wazi ya ufaransa mwezi uliopita.

Mskoti huyo akiwa na kocha Ivan Lendl alishinda michuano ya wazi ya Wimbledon na Michuano ya wazi ya Marekani ya Olimpiki katika kipindi cha miaka miwili 2012-2014.

Lendl ni mshindi namba moja duniani na mshindi wa wa mara nane wa Grand Slam na amekuwa mtumishi katika chama au shirikisho la Tenisi la Marekani.

Vardy asaini kandarasi mpya na Leicester

Mshambuliaji wa Uingereza na Leicester Jamie Vardy amekubali kuweka kandarasi mpya na viongozi wa ligi ya Uingereza Leicester.

Leicester imesema kuwa mchezaji huyo wa miaka 29 ambaye mabao yake yameisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu uliopita ameongeza kandarasi yake hadi miake minne na klabu hiyo.

''Pande zote mbili zinatumai tangazo hilo litamaliza uvumi wa hivi karibuni kuhusu hatma ya Jamie'',taarifa ya klabu imesema.

Vardy alitarajiwa kununuliwa na klabu ya Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 20 na Arsenal kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016 huku The Gunner ikitoa kitita cha pauni 120,000 kila wiki kwa mchezaji huyo.

Leicester nayo ilijibu kwa kutaka kumpatia pauni 100,000 kwa wiki.

SERIKALI YA UFARANSA YAPIGA MARUFUKU VILEVI UWANJANI EURO

Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve,amewataka waandaaji wa michuano ya bara la ulaya ya Euro 2016 juu ya kukataza vilevi katika maeneo ya michezo. Amesema maeneo ya michezo ni nyeti wakati mechi zikichezwa na hata siku moja kabla ya michuano.

Tamko hilo limekuja siku tatu baada ya fujo kuibuka kutoka kwa mashabiki wa Marseille ambao walikua wamelewa.

Shirikisho la soka barani ulaya,UEFA wameionya England na Urusi kuwa ziko kwenye wasiwasi wa kutolewa katika mashindano ya michuano ya soka barani ulaya mwaka huu,euro 2016 kama mashabiki wao wataendelea kufanya fujo.

Michuano hiyo ya UEFA imeomba radhi kwa hali ya utovu wa nidhamu au vurugu zilizojitokeza kati ya urusi na mashabiki wa waingereza huko Marseille

MZAMBIA ATUA YANGA KWA MILION 240

YANGA imemnasa mshambuliaji mpya raia wa Zambia, Obrey Chirwa anayechezea klabu ya Platinum FC ya Zimbabwe kwa kitita cha dola za Marekani 120,000 (zaidi ya Sh milioni 240 za Tanzania).

Kwa mujibu wa gazeti la The Herald la Zimbabwe jana lilieleza kuwa Chirwa ambaye amewahi kuichezea timu ya Konkola Blades ya Zambia, ameifungia Platinum mabao matano katika mechi nane alizocheza kwenye Ligi Kuu ya Zimbabwe.

Chirwa, ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23 imeelezwa na gazeti hilo kuwa aliondoka Zimbabwe juzi kuja Dar es Salaam na alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam jana.

Chirwa anatarajia kushirikiana na mshambuliaji mahiri wa Yanga Donald Ngoma, ambaye pia ametokea timu hiyo ya Zimbabwe. Awali Yanga ilikuwa ikimuwania winga Walter Musona kutoka Platinum kabla ya kughairi dakika za mwisho na Chirwa kuonekana mtu sahihi kwa nafasi hiyo.

Viongozi wa Yanga hawakupatikana jana kuzungumzia suala hilo na hata Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm ambaye yupo Algeria na Yanga, alipotafutwa kwa njia ya mtandao kuhusu usajili huo alisema hana cha kuzungumza.

Wakati huohuo, Yanga iliwasili salama jana asubuhi nchini Algeria tayari kwa mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) dhidi ya wenyeji MO Bejaia. Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema wachezaji wote wapo katika ari ya ushindi kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.

“Nashukuru tumewasili salama hapa Bajaia, wachezaji wote tupo salama hakuna majeruhi na kila mmoja wetu ana ari kuhakikisha tunaanza vizuri kwa kupata ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya ushindi,”alisema Cannavaro.

Yanga iliingia kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa mabao 2-1, ikiwa ni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 nyuma kabla ya kufungwa 1-0.

Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi wa Morocco, Bouchaib El Ahrach atakayekuwa katikati akisaidiwa na Redouane Achik na Youssef Mabrouk. Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa wa Afrika, TP Mazembe Juni 28.

GAME KATI YA POLAND NA UJERUMANI ITATOA MWELEKEO WA KUNDI C: JOCHIM LOW

Mara baada ya mchezo wa Ujerumani dhidi ya Ukraine,Ambao ulimalizika kwa mabao 2 kwa 0 na ukrine kocha wa Ujerumani Jochim Low amewaambia waandishi wa habari kwamba, haikuwa rahisi kupata ushindi dhidi ya Ukraine yenye safu ngumu ya ulinzi lakini walifanikiwa kufanya hivyo

Low pia ameutaja mchezo wa Alhamisi kati ya Ujerumani dhidi Poland ndiyo utaamua msimamo wa kundi nani anaongoza na nani tafuata. Poland pia wamefanikiwa kushinda mchezo wao dhidi ua Ireland ya Kaskazini uliochezwa mapema.

kocha wa Ujerumani Jochim Low amesema“Tulitawala lakini haikuwa kazi rahisi dhidi ya Ukraine yenye ukuta mzuri, lakini tulipata njia na mwisho wa siku nimeridhika.”

Hata hivyo taarifa yake imeendele kusema “Mchezo dhidi ya Poland utaamua huku timu zote zikiwa zimeshinda mechi za awali na matokeo ya mechi hiyo yatatengeneza mwonekano wa msimamo wa Kundi.

Aidha taarifa yake imesema kuwa Tunawachezaji wengi ambao hawana majeraha lakini nafikiri wachezaji waliocheza wamefanya kazi nzuri.”

UFARANSA KUWATIMUA MASHABIKI WA URUSI

Kiongozi wa chama cha mashabiki wa kandanda nchini Urusi, anatimuliwa kutoka nchini Ufaransa kufuatia ghasia zilizotokea wakati wa mechi za kuwania kombe la taifa bingwa barani Ulaya, kati ya Urusi na Uingereza mjini Marseille.

Alexander Shprygin ni mmoja wa mashabiki 20 wa Urusi wanaotimuliwa kutoka Ufaransa.

Walikamawa siku ya Jumanne wakiwa safarini kutoka Marseille kwenda Lille kudhudhuria mechi kati ya Urusi na Slovakia

Kukamatwa kwao kuliikasirisha urusi iliyomuita balozi wa Ufaransa humo kupinga.

Chama hicho cha mashabiki kinachoongozwa na Shprygin kinaungwa mkono na serikali ya Urusi.

Mashabikia wa uingereza na Urusi walipamabana kabala ya na baada ya timu hizo kucheza siku ya Jumamosi.

Polisi wa Ufaransa walisema kuwa wahuni 150 wa Urusi waliopewa mafunzo ndio walihusika

Mwili wa Mohamed Ali umewasili mjini Louisville, Kentucky kwaajili ya mazishi ijumaa

Mwili wa aliyekuwa bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali, umewasili mjini Louisville, Kentucky, ambako atazikwa siku ya Ijumaa.

Mwili wa bondia huyo wa zamani ulisafirishwa kwa msafara wa magari kutoka uwanja wa ndege wa Louisville .

Mazishi yake yanatarajiwa kuwa hafla kubwa ya umma.

Ali alikuwa mmoja wa wanamichezo maarufu zaidi duniani katika karne hii ya 20.

Page 68 of 70