blog category

 

 

ORODHA YA WACHEZAJI 100 WENYE THAMANI KUBWA ULIMWENGUNI IMETOKA, MESSI KINARA

Taasisi inayosihusisha na masuala ya soka ya CIES Football Observatory imetoa utafiti ambao unaonesha wachezaji 100 wenye thamani ya juu kwa sasa ulimwenguni kutoka ligi tano bora Ulaya.

Katika orodha hiyo, nyota wa Barcelona Lionel Messi ameibuka kidedea kuwa na thamni kubwa ya Euro milioni 211.1 sawa na Pauni 163, hiyo imetokana na ubora aliozidi kuuonesha msimu wa ligi ulioisha hivi karibuni.

Neymar Jr. ameshika nafsi ya pili akimshinda nyota wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ambaye anashika nafasi ya tatu.

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ndio kinara wa wachezaji wote wa EPL akiwa na thamani ya Euro milioni 112.5.

Kane anafuatiwa kwa karibu na Anthony Martial wa Manchester United, Paul Pogba na Gareth Bale na wengine.

Angalia orodha yenyewe hapa;

 

 

VIONGOZI MTWAREFA WACHUANA.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) kimefanikiwa kupata viongozi wapya kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika wilayani Masasi mkoani hapa.

Uchaguzi huo uliohudhuriwa na wajumbe 30 wa mkutano mkuu, ulitanguliwa na mkutano mkuu ambao uliendeshwa kwa muda mfupi na mwenyekiti wake Athumani Kambi ambaye baadaye alijiuzulu kwa ajili ya kugombea upya nafasi yake.

Jumla ya wagombea 14 walikuwa wakiwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo ambapo wagombea watano walikuwa wakiwania nafasi tatu za ujumbe wa mkutano mkuu wa MTWAREFA huku nafasi za mweka hazina, mwakilishi wa vilabu na mjumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zikiwa na mgombea mmoja kila nafasi ambapo walipigiwa kura za ndiyo na hapama.

Nafasi nyingine ambazo zilikuwa na mgombea mmoja ni katibu mkuu, makamu mwenyekiti na mwenyekiti huku nafasi ya katibu mkuu msaidizi ikiwaniwa na watu watatu ambao ni Baraka Jamali, David Paul na Abasi Mkuwaje.

Katika matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya MTWAREFA, Hussein Kingi, yalimfanya Athuman Kambi kufanikiwa kuitetea nafasi yake kwa kupata ushindi wa kishindo wa asilimia 100 baada ya kupigiwa kura za NDIYO na wajumbe wote 30 wa mkutano huo.

Aidha, Edward Kapwapwa pia amefanikiwa kuitetea nafasi yake ya makamu mwenyekiti kwa kupata kura za NDIYO 29 kati ya 30 za wajumbe wote huku kura moja ndio ambayo ilikuwa ya HAPANA.

Viongozi wengine waliochaguliwa kihalali kupitia uchaguzi huo watakaoongoza kwa muda wa miaka mine ni Kizito Mbano ambaye amepata nafasi ya katibu mkuu wa chama kwa kura za NDIO 29, Baraka Jamali anayekuwa katibu mkuu msaidizi kwa kupata kura 16 na kuwashinda wapinzani wake David Paul kura 9 na Abasi Mkuwaje kura 5.

Nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF imeendelea kusalia kwa Mohamed Remtula (Mamu) ambaye amepigiwa kura za NDIO 29, huku nafasi ya mwakilishi wa vilabu ikibakia kuwa kwa Yahaya Jamali aliyeitetea kwa kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kupata kura za NDIO 30 na Thomasi Mhanga akipata nafasi ya mweka hazina baada ya kupewa kura 21 na NDIO huku kura 9 zikimkataa.

Nafasi tatu za wajumbe wa MTWAREFA zilizokuwa zikiwaniwa na wagombea watano na idadi ya kura zao kwenye mabano, zilienda kwa Hamisi Kangomba (25), Fredrick Nachinuka (24) na Keneth Kilinga (21).

BMT yaisimamisha PST mwaka mmoja

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limelisimamisha kwa mwaka mmoja Shirikisho la Masumbwi la Ngumi za Kulipwa nchini (PST) kujishughulisha na mchezo huo baada ya kugundulika kukiuka kanuni na sheria za mchezo husika.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limefikia maamuzi hayo baada ya kugundulika kukiuka kanuni na sheria za mchezo husika.

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema uongozi wote wa PST hautaruhusiwa kujishughulisha na masumbwi baada ya kuwachezesha mabondi wenye umri chini ya miaka 18 jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Aidha, Kiganja amesema Baraza la Michezo la Taifa limetengua ukatibu wa Emmanueli Mlundwa katika kamati ya ngumi za kulipwa maamuzi yaliyoanza kuanzia hii leo.

Newcastle yanusurika,Sunderland yapata sare

Klabu ya Newcastle imaimarisha matumaini yake ya kusalia katika ligi kuu ya Uingereza kufuatia bao la Andros Townsend na penalti iliopanguliwa na kipa wa kilabu hiyo dhidi ya Crystal palace.

Huku Norwich ikicheza dhidi ya Arsenal na Sunderland kutoka sare na Stoke,Newcastle sasa imepanda hadi nafasi ya 17 na kuondoka katika eneo la kushushwa daraja.

Towsend aliipatia Newcastle bao la kwanza baada ya mapumziko kupitia shambulio kali.

Kipa Darlow baadaye aliokoa Newcastle alipookoa penalti ya Yohan Cabaye.

Marcus Rashford sasa rasmi kikosi cha Uingereza

Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 18, alifunga goli lake la kwanza akiichezea timu ya taifa Uingereza kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki walioshinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Australia siku ya Ijumaa.

Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Daniel Sturridge ameorodheshwa kwenye kikosi hicho, hata hivyo mchezaji wa Newcastle United Andros Townsend na Danny Drinkwater wa Leicester City wameachwa.

Kikosi chote cha Uingereza kilichotangazwa na kocha Roy Hogson ni kama ifuatavyo:-

Makipa: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley).

Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool).

Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal).

Washambuliaji: Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester United).

TFF YAPATA AFISA HABARI MPYA.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzaia leo Aprili 27, 2016.

Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS).

Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri. Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha.

ULIMWENGU KAMBINI NA TAIFA STARS KUIVAA MISRI

Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amejiunga na timu ya taifa, Taifa Stars leo kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri utakaochezwa Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.

Ulimwengu amechelewa kujiunga na Taifa Stars kutokana na klabu yake ya TP Mazembe ya DRC Congo kumuomba abaki kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu nchi humo.

Mchezaji huyo ameingia nchini leo, jijini Dar es salaam na moja kwa moja kuingia kambini.

Taifa Stars sasa inamsubiri mshambuliaji na Nahodha, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji pekee, ambaye naye klabu yake ilimuomba abaki kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa mchujo wa kuwania kucheza Europa League msimu ujao.

Samatta na Ulimwengu, wote wameziongoza klabu zao kushinda mwishoni mwa wiki, Genk ikiilaza 5-1 Sporting Charleroi na kufuzu Europa League na Mazembe ikiichapa 2-0 AS Vita katika Ligi ya DRC Congo.

SHILOLE APASUA JIPU KUHUSU MRITHI WA NUH MZIWANDA, UNATAKA KUMJUA NI NANI? BOFYA HAPA

Shilole a.k.a Shishi Baby amesema baada ya kuachana na Nuh Mziwanda bado jimbo la moyo wake halijapata mgombea mpya wa kuziba nafasi yake.

Page 67 of 67