SPORTS & ENTERTAINMENT

 

 

ALIKIBA KUACHIA JIWE LINGINE SIKU ZA KARIBUNI

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma Seduce Me katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika ujumbe ambao kwa kiasi fulani unahashiria ujio wa ngoma mpya.

Ujumbe huo ambao ulilenga kumpongeza msanii mwenzake, Abby Skillz kwa kufunga ndoa uliishia kwa kudokeza hilo.

Hongera Mkongwe nakutakia Kheri Na mafanikio Katika Ndoa Yako

Na ngoma Mpya Inafuata

#SapportedByKiba #KingKiba

Hata hivyo haijaeleweka iwapo ngoma hiyo itakuwa ya Abby Skillz pekee kwani amekuwa akifanya kazi na Alikiba kupitia King’s Music.

Ikumbukwe wawili hawa walishatoa wimbo pamoja mwaka jana ‘Averina’ ambao Mr. Blue alishirikishwa pia.

Wiki mbili zilizopita katika mahojiano na Bongo5 Alikiba alisema ngoma yake ‘Seduce Me’ ikifikisha views milioni 10 katika mtandao wa YouTube atatoa ngoma mpya. Hadi kufikia sasa ngoma hiyo ina views milioni 6.1.

WAZIRI MWAKYEMBE AKANUSHA KUPIGA STOP MISS TANZANIA

Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni, na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amekanusha kufuta mashindano ya Miss Tanzania na Tuzo za wasanii.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo jana usiku wakati akihojiwa katika kipindi cha michezo cha Safari Sports kinacho Rushwa na Safari Radio kila siku kuanzia saa moja mpaka saa mbili usiku hii, ambapo amesema mashindano na tuzo hapa nchini huanzishwa bila kuwa na andiko la uendelezaji, hivyo ametoa agizo kwa Baraza la Sanaa (Basata) kwamba mtu yeyote akija na shindano au wazo la tuzo watamruhusu pale tu atakapotoa msingi wa mwendelezo na siyo kwa kuwa amepata mfadhili wa muda.

“Hata mashindano ya ulimbwende tumeshachoka watoto wa kike wanahangaika, lakini zawadi zikitangazwa unaambiwa mshindi wa kwanza gari namba mbili pikipiki ila sijawahi kuona hata mmoja ambaye amewahi kuzipata au ikatokea utoaji wa zawadi usio na kelele,” amesema.

Dk Mwakyembe amesema amekuwa akifuatwa na warembo kadhaa ofisini kwake wakilalamikia kutopewa zawadi zao mara baada ya mashindano ya Miss Tanzania.

Hivyo amesema alikaa na Basata miezi miwili iliyopita na kuwapa maagizo, “Kuanzia sasa chombo chochote au kampuni inayoendesha mashindano ya ulimbwende ambayo iliwahi kuahidi vijana wetu wa Kitanzania zawadi na haijatoa tusigombane, watoe zawadi zote wawatafute warembo wawape.”

SIMBA SC YAKWEA KILELENI KWA KUICHAPA STAND UNITED

Klabu ya Simba SC leo imefanikiwa kupata matokeo ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Stand United kunako dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Shiza Kichuya na Laudit Mavugo huku goli la kufutia machozi la Stand United likifungwa na Mutasa Munashe.

Kwa sasa Simba ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara kwa alama 11 ikifuatiwa na Mtibwa Sugar na Azam FC zote zikiwa na alama 11 ikiwa tofauti ni magoli ya kufungwa na kufunga.

WEUSI WAONESHA UTOFAUTI NA WCB

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka sababu za wao kutosaini wasanii.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kihasara’amsema kuamua kumsaini msanii ni kukubali kubeba ndoto zake zote alizonazo kitu ambacho kwa sasa hawapo tayari.

“Ukisema unafungua label au una kumsaiini mtu, ina maana anakukabidhi ndoto zake mikononi mwako, je unaweza kuzifikisha??, watu wanataka watengeneza maisha yao, sisi tunavyoona bado,” amesema Nikki wa Pili.

“Unamuona Chin Bees tumekuwa naye kitambo kwanini hatukumsaini lakini tumemsaidia mpaka amekuja kupata Wanene.

Nikisema sasa hivi namsaini Chin Bees atanidai video kama tatu, atanidai promotion, hiyo itakuwa baadaye one step at a time,” ameongeza.

Nikki wa Pili ameshafanya kolabo tatu na Chin Bees ya kwanza ikiwa ni Role Model, Sweet Mangi na sasa Kihasara.

JOHANNA KONTA ACHAPWA TENA CHINA OPEN

Johanna Konta amepoteza katika michuano ya China open mbele ya mchezaji nambari 65 duniani Monica Niculescu.

Amechapwa kwa seti 6-1 6-2 mjini Beijing.

Konta hajawa na kiwango kizuri tokea kumalizika kwa michuano ya Wimbledon ambapo aliondolewa katika hatua ya nusu fainali.

Garbine Muguruza, Simona Halep, Karolina Pliskova, Elina Svitolina, Venus Williams na Caroline Wozniacki tiyari wamejihakikishia nafasi katika hatua zinazofuata kwenye michuano hiyo.

Konta anasema iwapo atapata nafasi ya kuendelea mbele katika michuano yoyote inampasa kujipanga upya ili aweze kukabiliana na wachezaji nguli.

CHELSEA USO KWA USO NA ATLETICO MADRID-KLABU BINGWA ULAYA

Michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi inapigwa hii leo jumanne usiku kwa michezo mbalimbali .

Kundi E - Sevila inacheza na Maribor, Spartak Moscow dhidi ya Liverpool, Kundi F - Manchester city inacheza na Shakhtar Donetsk, Napoli inacheza na Feyenoord.

Kundi G- Besiktas inacheza na Rasen Ballsport , Monaco dhidi ya FC Porto. Kundi H - Apoel Nicosia dhidi ya Tottenham na Borussia Dortmund inachuana na Real Madrid.

Kesho Jumatano Kundi A - FC Basel itacheza na Benfica, CSKA Moscow na Manchester United. Kundi- B Anderlecht dhidi ya Celtic, PSG itakwaruzana na Bayern Munich.

Kundi C- Qarabag dhidi ya As Roma, Atletico Madrid wanakutana na Chelsea, Kundi - D Juventus itacheza na Olympiacos huku Sporting ikichuana na Barcelona.

TRUMP APINGWA NA WACHEZAJI WA SOKA MAREKANI

Wachezaji wa ligi ya soka Marekani kwa pamoja wameendelea kumpinga Rais Trump kwa kugoma kuimba wimbo wa Taifa la nchi hiyo katika mchezo wa Jumapili.

Walionekana wakiwa wameweka tu mikono vifuani ama mabegani mwa wachezaji wenzao huku wimbo huo ukiendelea.

Wengine walipiga magoti.

Cam Newton mchezaji nyota wa Carolina Panthers yeye alinyoosha mkono wake juu wakati wimbo huo ukiimbwa.

Hata hivyo mgomo wa wiki hii haukuwa na nguvu kama wa wiki iliyopita.

Katika mchezo baina ya Dallas Cowboys na Los Angeles Rams uliendelea bila ya mgomo wowote.

Trump ameandika katika mtandao wa Tweeter akiwataka viongozi wa chama cha soka Marekani kuwachukulia hatua wote waliohusika.

Mgomo huo ulianza mwaka jana baada ya mchezaji Colin Kaepernick wa San Francisco 49ers kuelezea namna raia weusi wa Marekani wanavyoteseka baada ya mlolongo wa kupigwa risasi na polisi.

ASHLEIGH AMLAZA KONTA- WUHAN

Mwingereza Johanna Konta ameshindwa kufurukuta dhidi ya Ashleigh Barty baada ya kufungwa katika mchezo wa raundi ya pili katika michuano ya Wazi ya Wuhan, China.

katika mchezo huo Konta alijitahidi kukabiliana vikali na mpinzani lakini mwishoo alijikuta anapoteza mchezo kwa kufungwa 6-0 4-6 7-6 (7-3) .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amepoteza mechi saba za zamani zilizopita tangu kufikia nusu fainali za Wimbledon. Naye Peng Shuai wa china amemgalagaza Petra Kvitova wa Jamhuri ya Czech seti 7-6 (9-7) 6-7 (5-7) 7-6 (7-3) katika mchezo ambao ulijaa upinzani .

Page 7 of 70