SPORTS & ENTERTAINMENT

 

 

TIGER WOODS YUKO FITI KUREJEA UWANJANI

Tiger Woods anatarajiwa kurejea tena katika mchezo wa gofu miezi nane baada ya kuandamwa na majeraha.

Atajitupa uwanjani kuanzia Novemba 30 mpaka Desemba 3.

Woods mshindi wa vikombe 14 vya kimataifa, anapona majeraha ya upasuaji wa mgongo aliyofanyiwa miaka mitatu iliyopita ambayo kwa wakati fulani alikuwa akirudia upasuaji mara kwa mara na kumfanya kuwa dhaifu.

Alijiondoa katika michuano ya Dubai mwezi Februari kwa sababu hiyohiyo.

''Ninajipanga kurejesha heshima yangu, furaha yangu na uwezo wangu kupitia mchezo ninaoupenda, alisema Woods''

Woods hajashinda taji lolote kubwa tokea mwaka 2008.

DEREVA LEWIS HAMILTON ANYAKUA TAJI LA NNE LA DUNIA

Dereva Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda taji la nne la dunia katika michuano ya Mexico grand prix licha ya kumaliza akiwa nafasi ya tisa baada kugongana na Sebastian Vettel.

Mafanikio ya Hamilton yanamfanya kuwa dereva wa Uingereza kufanikiwa zaidi katika historia akiwa amevunja rekodi ya Jackie Stewart.

Anaungana na Vettel na mfaransa Alain Prost wenye vikombe vinne.

Aligongana na Vettel wakati walipokuwa wakijaribu kupishana katika kona.

LAMAR ASEMA PRODUCER WA BONGO WANATOZA GHARAMA ZA CHINI ZAIDI AFRIKA

Kutokana na hilo Lamar ameshauri kuwa ni vema kwa wasanii kutoa sapoti kwa producer wa Bongo na si vinginevyo.

“Soko letu katika producers sisi ndio ambao tunatoza gharama za chini kimuziki Afrika, ukienda South Africa watu wanachajiwa mpaka dola 5,000 kurekodi lakini sisi gharama za juu sidhani hata kama inafika milioni mbili/tatu” Lamar ameiambia Safari Media.

“Kwa hiyo wasanii wanatakiwa wasapoti producer wao, unakuta msanii anaweza kwenda South Africa akalipia labda dola 3,000 kufanya wimbo lakini huku hataki kulipia hela hiyo au anataka bure” ameongeza.

Producer wa muziki kutoka studio za Fish Crab, Lamar amesema producer wa Bongo wanatoza gharama za chini zaidi katika kurekodi ukilinganisha na nchini nyingine Afrika.

BRAVO AWAOKOA MAN CITY MIKONONI MWA WOLVES

Claudio Bravo aliwafaa sana Manchester City baada ya kuwasaidia kulaza Wolves kupitia mikwaju ya penalti katika Kombe la Carabao na kuwasaidia kufika robofainali.

Bravo, alifanya kazi ya ziada kuzuia wasifungwe bao muda wa kawaida wa mechi, na aliendeleza hilo kwa kuzuia mikwaju ya Alfred N'Diaye na Conor Coady wakati wa matuta ya baada ya mechi baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare tasa.

City walifunga mikwaju yao yote, mkwaju wa Sergio Aguero ukiwa wa ushindi.

Wolves walikuwa ndiyo timu ya kwanza kuwalemea viongozi hao wa Ligi ya Premia na kuwazuia kufunga msimu huu.

Wolves, wamo alama mbili mbele kileleni katika Ligi ya Championship na walicheza vizuri sana mechi hiyo iliyochezewa Etihad, wakishangiliwa na mashabiki wao wapatao 6,000.

Kabla ya kufika Etihad, vijana hao wa Nuno Espirito Santo walikuwa wamefungwa mabao 13 pekee katika michezo 16 msimu wote.

City watakuwa ugeninit West Bromwich Albion Jumamosi wakilenga kuendeleza ubabe wao Ligi ya Premia.

Wolves nao watakuwa ugenini kucheza dhidi ya QPR uwanjani Loftus Road katika ligi ya Championship siku hiyo.

ANTHONY JOSHUA AJIPA TUMAINI MWAKA 2018

Bondia Anthony Joshua amesema upo uwezekano wa mwaka 2018 kuanza vizuri baada kumaliza 2017 kwa kumchapa Carlos Takam.

Joshua bingwa wa uzito wa juu wa taji la WBA na IBF aliendeleza ushindi wake alioupata mwezi April dhidi ya Wladimir Klitschko kwa kumchapa Takam ndani ya raundi 10 mjini Cardiff.

Mdhamini wake Eddie Hearn amesema kuna uwezekano akachauana na Deontay Wilder huku kocha wake Rob McCracken akimtaja Joseph Parker kuwa anafaa zaidi.

Antony Joshua amekuwa miongoni mwa wanamichezo wanaovutia zaidi kwa siku za karibuni, huku akiweka rekodi ya kushinda kwa asilimia mia moja kwenye michuano yake yote.

HARMORAPA ADAI SHOW ZA MIKOANI PASUA KICHWA

Harmorapa ameeleza kuwa ukimya wake unasababishwa na biashara anazofanya nje ya muziki pamoja na show zake za mikoani ambazo amekuwa akifanya mara nyingi.

“Nipo bize sana na mishe nyingine nje ya muziki, namaanisha mimi ni mfanyabiashara, so huwa mara nyingi nasafiri, mara nyingi huwa napiga tour zangu mikoani na project zangu za muziki zipo kama kawaida” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na hilo ni vigumu sana kumkuta Dar es Salaam kwani anakuwa bize sana.

FEDERER AMCHAKAZA DEL POTRO MICHUANO YA USWISI

Mchezaji namba mbili kwa ubora katika tenisi duniani kwa upande wa wanaume Roger Federer amefanikiwa kumshinda Juan Martin Del Potro katika michuano ya ndani ya Uswisi.

Ameshinda kwa seti 6-7 (5-7) 6-4 6-3 huku akionyesha kiwango cha hali ya juu ikiwa ni wiki moja kabla ya michuano ya Paris Masters.

Ushindi huu unamfanya kupunguza pengo kati yake na mchezaji namba moja duniani Rafael Nadal.

Federer ameshinda taji lake la nane katika michuano hiyo ya Basel likiwa niu la saba kwa mwaka 2017.

NYOTA NDOGO AFUNGUKA YALIYOMKUTA

Muimbaji wa Kenya, Mwanaisha Abdallah maarufu kama Nyota Ndogo amekuwa akiwaacha mashabiki wake na maswali mengi kwa kulalamika muda mwingi kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa kuna baadhi ya vitu vimekuwa vikimtesa kwa takribani miaka 17 sasa.

Je unataka kujua ni vitu gani hivyo ambavyo vimekuwa vikimsumbua mrembo huyo kwa muda wote huo? Kupitia mtandao wa Instagram, Nyota Ndogo ameahidi kufunguka kila kitu kwa kuweka wazi Jumatano hii.

MUNGU nipe ujasiri inshalla kesho hasubui nitawaeleza kila kitu kinachonisumbua mybe hakuna atakae nisaidia couse kila mtu anamatatizo yake but nataka tu mujue nayopitia couse sometimes nakula chakula sio kwakuskia utamu ila unakula ili usikae njaa 10:30 nitaanza kuweka voicenot mtanisamehe nisipofanya hivi sijui maisha yangu yatakua yakulia tu na naona basi nafaa kuwacha kulia.

Page 6 of 70