blog category

 

 

TRUMP APINGWA NA WACHEZAJI WA SOKA MAREKANI

Wachezaji wa ligi ya soka Marekani kwa pamoja wameendelea kumpinga Rais Trump kwa kugoma kuimba wimbo wa Taifa la nchi hiyo katika mchezo wa Jumapili.

Walionekana wakiwa wameweka tu mikono vifuani ama mabegani mwa wachezaji wenzao huku wimbo huo ukiendelea.

Wengine walipiga magoti.

Cam Newton mchezaji nyota wa Carolina Panthers yeye alinyoosha mkono wake juu wakati wimbo huo ukiimbwa.

Hata hivyo mgomo wa wiki hii haukuwa na nguvu kama wa wiki iliyopita.

Katika mchezo baina ya Dallas Cowboys na Los Angeles Rams uliendelea bila ya mgomo wowote.

Trump ameandika katika mtandao wa Tweeter akiwataka viongozi wa chama cha soka Marekani kuwachukulia hatua wote waliohusika.

Mgomo huo ulianza mwaka jana baada ya mchezaji Colin Kaepernick wa San Francisco 49ers kuelezea namna raia weusi wa Marekani wanavyoteseka baada ya mlolongo wa kupigwa risasi na polisi.

ASHLEIGH AMLAZA KONTA- WUHAN

Mwingereza Johanna Konta ameshindwa kufurukuta dhidi ya Ashleigh Barty baada ya kufungwa katika mchezo wa raundi ya pili katika michuano ya Wazi ya Wuhan, China.

katika mchezo huo Konta alijitahidi kukabiliana vikali na mpinzani lakini mwishoo alijikuta anapoteza mchezo kwa kufungwa 6-0 4-6 7-6 (7-3) .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amepoteza mechi saba za zamani zilizopita tangu kufikia nusu fainali za Wimbledon. Naye Peng Shuai wa china amemgalagaza Petra Kvitova wa Jamhuri ya Czech seti 7-6 (9-7) 6-7 (5-7) 7-6 (7-3) katika mchezo ambao ulijaa upinzani .

WAZIRI MWAKYEMBE AKANUSHA KUPIGA STOP MISS TANZANIA

Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni, na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amekanusha kufuta mashindano ya Miss Tanzania na Tuzo za wasanii.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo jana usiku wakati akihojiwa katika kipindi cha michezo cha Safari Sports kinacho Rushwa na Safari Radio kila siku kuanzia saa moja mpaka saa mbili usiku hii, ambapo amesema mashindano na tuzo hapa nchini huanzishwa bila kuwa na andiko la uendelezaji, hivyo ametoa agizo kwa Baraza la Sanaa (Basata) kwamba mtu yeyote akija na shindano au wazo la tuzo watamruhusu pale tu atakapotoa msingi wa mwendelezo na siyo kwa kuwa amepata mfadhili wa muda.

“Hata mashindano ya ulimbwende tumeshachoka watoto wa kike wanahangaika, lakini zawadi zikitangazwa unaambiwa mshindi wa kwanza gari namba mbili pikipiki ila sijawahi kuona hata mmoja ambaye amewahi kuzipata au ikatokea utoaji wa zawadi usio na kelele,” amesema.

Dk Mwakyembe amesema amekuwa akifuatwa na warembo kadhaa ofisini kwake wakilalamikia kutopewa zawadi zao mara baada ya mashindano ya Miss Tanzania.

Hivyo amesema alikaa na Basata miezi miwili iliyopita na kuwapa maagizo, “Kuanzia sasa chombo chochote au kampuni inayoendesha mashindano ya ulimbwende ambayo iliwahi kuahidi vijana wetu wa Kitanzania zawadi na haijatoa tusigombane, watoe zawadi zote wawatafute warembo wawape.”

MANCHESTER UNITED YAREKODI MAPATO YA JUU YA £581M

Klabu ya Manchester United imeripoti mapato ya £581m kwa kipindi cha fedha cha 2017 huku mapato ya runinga yakiongezeka.

Katika mwaka mmoja baada ya kushinda kombe la bara Yuropa, na EFL klabu hiyo imetia saini kandarasi 12 za ufadhili huku mapato ya matangazo pamoja na yale yanaopatikana wakati wa mechi yakiongezeka.

Klabu hiyo ilifaidika kutoka kwa ongezeko la mapato ya runinga wakati wa kipindi cha 2016-17 ikiwa ndio mwaka wa kwanza kati ya mitatu ya makubaliano ya matangazo ya runinga.

Klabu hiyo ya Old Trafford ni ya pili katika ligi ya premia.Ina alama sawa na mabao na viongozi wa ligi Manchester City.

Mnamo mwezi Juni tarehe 30 mapato ya matangazo yaliongezeka hadi £194m kutoka £140m mwaka mmoja kabla ikiwa ni ongezeko la silimia 38.

Msimu huu klabu hiyo imerudi katika ligi ya vilabu bingwa baada ya kushinda kombe la Yuropa dhidi ya Ajax mnamo mwezi Mei.

WEUSI WAONESHA UTOFAUTI NA WCB

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka sababu za wao kutosaini wasanii.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kihasara’amsema kuamua kumsaini msanii ni kukubali kubeba ndoto zake zote alizonazo kitu ambacho kwa sasa hawapo tayari.

“Ukisema unafungua label au una kumsaiini mtu, ina maana anakukabidhi ndoto zake mikononi mwako, je unaweza kuzifikisha??, watu wanataka watengeneza maisha yao, sisi tunavyoona bado,” amesema Nikki wa Pili.

“Unamuona Chin Bees tumekuwa naye kitambo kwanini hatukumsaini lakini tumemsaidia mpaka amekuja kupata Wanene.

Nikisema sasa hivi namsaini Chin Bees atanidai video kama tatu, atanidai promotion, hiyo itakuwa baadaye one step at a time,” ameongeza.

Nikki wa Pili ameshafanya kolabo tatu na Chin Bees ya kwanza ikiwa ni Role Model, Sweet Mangi na sasa Kihasara.

EBITOKE ASEMA BEN POL ANAMZINGUA

Mchekeshaji Ebitoke amesema kwa sasa hayupo katika mahusiano mazuri na Ben Pol. Wawili hao ambao walitangaza kuwa mapenzini miezi kadhaa iliyopita baada Ebitoke kujitokeza hadhara na kueleza anampenda mkali huyo wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol na hatimaye kuwa pamoja, kwa Siku za hivi karibuni hawajaonekana pamoja kama ilivyokuwa mwanzo.

Ebitoke ameeleza kuwa kwa sasa Ben Pol amekuwa akimpuuzia kwa mambo kadhaa hasa katika suala zima la mawasiliano.

“Simuelewi Ben Pol, simu hapokei, text hanilibu, ananipuuzia sijui kwanini” amesema Ebitoke.

Hata hivyo ameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa suala hilo linamuumiza sana kwani walikuwa na malengo makubwa sana.

“Hawezi kunichomoka kwa sababu tulipanga kabisa malengo na nitaendelea kuyapigania,” amesema.

Ameongeza kuwa wakati wanaanza uhusiano wao Ben Pol alikuwa single hivyo hana wasi wasi iwapo anafanya hivyo kutokana na mahusiano aliyokuwa nayo hapo awali.

CHELSEA USO KWA USO NA ATLETICO MADRID-KLABU BINGWA ULAYA

Michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi inapigwa hii leo jumanne usiku kwa michezo mbalimbali .

Kundi E - Sevila inacheza na Maribor, Spartak Moscow dhidi ya Liverpool, Kundi F - Manchester city inacheza na Shakhtar Donetsk, Napoli inacheza na Feyenoord.

Kundi G- Besiktas inacheza na Rasen Ballsport , Monaco dhidi ya FC Porto. Kundi H - Apoel Nicosia dhidi ya Tottenham na Borussia Dortmund inachuana na Real Madrid.

Kesho Jumatano Kundi A - FC Basel itacheza na Benfica, CSKA Moscow na Manchester United. Kundi- B Anderlecht dhidi ya Celtic, PSG itakwaruzana na Bayern Munich.

Kundi C- Qarabag dhidi ya As Roma, Atletico Madrid wanakutana na Chelsea, Kundi - D Juventus itacheza na Olympiacos huku Sporting ikichuana na Barcelona.

TIWA SAVAGE AACHIA MIXTAPE YAKE

First lady wa Mavin Records Tiwa Savage ameamua kufuata nyendo za msanii za Wizkid kwa kuachia Mixtape yake ‘Sugarcane’.

Mixtape hiyo iliyotoa inajumla ya ngoma sita itauza kiasi cha dola 5.94 sawa na kiasi cha shilingi 13,327.53 za kitanzania na ngoma kama ‘Ma Lo’ aliyomshirikisha Wizkid na Spellz pamoja na ‘All Over’ zitapatika humo.

Page 5 of 67