blog category

 

 

FEDERER AMCHAKAZA DEL POTRO MICHUANO YA USWISI

Mchezaji namba mbili kwa ubora katika tenisi duniani kwa upande wa wanaume Roger Federer amefanikiwa kumshinda Juan Martin Del Potro katika michuano ya ndani ya Uswisi.

Ameshinda kwa seti 6-7 (5-7) 6-4 6-3 huku akionyesha kiwango cha hali ya juu ikiwa ni wiki moja kabla ya michuano ya Paris Masters.

Ushindi huu unamfanya kupunguza pengo kati yake na mchezaji namba moja duniani Rafael Nadal.

Federer ameshinda taji lake la nane katika michuano hiyo ya Basel likiwa niu la saba kwa mwaka 2017.

NYOTA NDOGO AFUNGUKA YALIYOMKUTA

Muimbaji wa Kenya, Mwanaisha Abdallah maarufu kama Nyota Ndogo amekuwa akiwaacha mashabiki wake na maswali mengi kwa kulalamika muda mwingi kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa kuna baadhi ya vitu vimekuwa vikimtesa kwa takribani miaka 17 sasa.

Je unataka kujua ni vitu gani hivyo ambavyo vimekuwa vikimsumbua mrembo huyo kwa muda wote huo? Kupitia mtandao wa Instagram, Nyota Ndogo ameahidi kufunguka kila kitu kwa kuweka wazi Jumatano hii.

MUNGU nipe ujasiri inshalla kesho hasubui nitawaeleza kila kitu kinachonisumbua mybe hakuna atakae nisaidia couse kila mtu anamatatizo yake but nataka tu mujue nayopitia couse sometimes nakula chakula sio kwakuskia utamu ila unakula ili usikae njaa 10:30 nitaanza kuweka voicenot mtanisamehe nisipofanya hivi sijui maisha yangu yatakua yakulia tu na naona basi nafaa kuwacha kulia.

DEREVA LEWIS HAMILTON ANYAKUA TAJI LA NNE LA DUNIA

Dereva Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda taji la nne la dunia katika michuano ya Mexico grand prix licha ya kumaliza akiwa nafasi ya tisa baada kugongana na Sebastian Vettel.

Mafanikio ya Hamilton yanamfanya kuwa dereva wa Uingereza kufanikiwa zaidi katika historia akiwa amevunja rekodi ya Jackie Stewart.

Anaungana na Vettel na mfaransa Alain Prost wenye vikombe vinne.

Aligongana na Vettel wakati walipokuwa wakijaribu kupishana katika kona.

ALIKIBA KUACHIA JIWE LINGINE SIKU ZA KARIBUNI

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma Seduce Me katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika ujumbe ambao kwa kiasi fulani unahashiria ujio wa ngoma mpya.

Ujumbe huo ambao ulilenga kumpongeza msanii mwenzake, Abby Skillz kwa kufunga ndoa uliishia kwa kudokeza hilo.

Hongera Mkongwe nakutakia Kheri Na mafanikio Katika Ndoa Yako

Na ngoma Mpya Inafuata

#SapportedByKiba #KingKiba

Hata hivyo haijaeleweka iwapo ngoma hiyo itakuwa ya Abby Skillz pekee kwani amekuwa akifanya kazi na Alikiba kupitia King’s Music.

Ikumbukwe wawili hawa walishatoa wimbo pamoja mwaka jana ‘Averina’ ambao Mr. Blue alishirikishwa pia.

Wiki mbili zilizopita katika mahojiano na Bongo5 Alikiba alisema ngoma yake ‘Seduce Me’ ikifikisha views milioni 10 katika mtandao wa YouTube atatoa ngoma mpya. Hadi kufikia sasa ngoma hiyo ina views milioni 6.1.

BRAVO AWAOKOA MAN CITY MIKONONI MWA WOLVES

Claudio Bravo aliwafaa sana Manchester City baada ya kuwasaidia kulaza Wolves kupitia mikwaju ya penalti katika Kombe la Carabao na kuwasaidia kufika robofainali.

Bravo, alifanya kazi ya ziada kuzuia wasifungwe bao muda wa kawaida wa mechi, na aliendeleza hilo kwa kuzuia mikwaju ya Alfred N'Diaye na Conor Coady wakati wa matuta ya baada ya mechi baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare tasa.

City walifunga mikwaju yao yote, mkwaju wa Sergio Aguero ukiwa wa ushindi.

Wolves walikuwa ndiyo timu ya kwanza kuwalemea viongozi hao wa Ligi ya Premia na kuwazuia kufunga msimu huu.

Wolves, wamo alama mbili mbele kileleni katika Ligi ya Championship na walicheza vizuri sana mechi hiyo iliyochezewa Etihad, wakishangiliwa na mashabiki wao wapatao 6,000.

Kabla ya kufika Etihad, vijana hao wa Nuno Espirito Santo walikuwa wamefungwa mabao 13 pekee katika michezo 16 msimu wote.

City watakuwa ugeninit West Bromwich Albion Jumamosi wakilenga kuendeleza ubabe wao Ligi ya Premia.

Wolves nao watakuwa ugenini kucheza dhidi ya QPR uwanjani Loftus Road katika ligi ya Championship siku hiyo.

SIMBA SC YAKWEA KILELENI KWA KUICHAPA STAND UNITED

Klabu ya Simba SC leo imefanikiwa kupata matokeo ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Stand United kunako dimba la Kambarage mjini Shinyanga.

Magoli ya Simba SC yamefungwa na Shiza Kichuya na Laudit Mavugo huku goli la kufutia machozi la Stand United likifungwa na Mutasa Munashe.

Kwa sasa Simba ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara kwa alama 11 ikifuatiwa na Mtibwa Sugar na Azam FC zote zikiwa na alama 11 ikiwa tofauti ni magoli ya kufungwa na kufunga.

HARMORAPA ADAI SHOW ZA MIKOANI PASUA KICHWA

Harmorapa ameeleza kuwa ukimya wake unasababishwa na biashara anazofanya nje ya muziki pamoja na show zake za mikoani ambazo amekuwa akifanya mara nyingi.

“Nipo bize sana na mishe nyingine nje ya muziki, namaanisha mimi ni mfanyabiashara, so huwa mara nyingi nasafiri, mara nyingi huwa napiga tour zangu mikoani na project zangu za muziki zipo kama kawaida” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na hilo ni vigumu sana kumkuta Dar es Salaam kwani anakuwa bize sana.

JOHANNA KONTA ACHAPWA TENA CHINA OPEN

Johanna Konta amepoteza katika michuano ya China open mbele ya mchezaji nambari 65 duniani Monica Niculescu.

Amechapwa kwa seti 6-1 6-2 mjini Beijing.

Konta hajawa na kiwango kizuri tokea kumalizika kwa michuano ya Wimbledon ambapo aliondolewa katika hatua ya nusu fainali.

Garbine Muguruza, Simona Halep, Karolina Pliskova, Elina Svitolina, Venus Williams na Caroline Wozniacki tiyari wamejihakikishia nafasi katika hatua zinazofuata kwenye michuano hiyo.

Konta anasema iwapo atapata nafasi ya kuendelea mbele katika michuano yoyote inampasa kujipanga upya ili aweze kukabiliana na wachezaji nguli.

Page 4 of 67