blog category

 

 

SERGIO AGUERO APOTEZA FAHAMU CHUMBA CHA KUBADILISHIA NGUO

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester City Sergio Aguero usiku wa kuamkia leo amedondoka ghafla na kuzimia katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya Nigeria mjini Krasnodar, Russia.

Aguero aliifungia timu yake mara mbili kabla ya mshambuliaji wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi kuandika la kwanza.

Aguero alipata fahamu baadae akiwa hospitali lakini madaktari wanasema asalie kwanza wodini ili hali itengemae zaidi.

Kelechi Ihenacho aliindikia Nigeria goli la pili kabla ya Ever Banega kuongeza jingine kwa Argentina.

Haijaelezwa nini kilichomsibu Aguero mpaka kuanguka na kupoteza fahamu na huenda taarifa zaidi zikatoka baadae.

MORATA ATAMANI KUISHI LONDON KWA MIAKA 10

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata amekanusha uvumi kwamba hapendi kuishi jiji la London na yupo tiyari kusaini mkataba wa miaka kumi kama itawezekana.

Awali Morata aliliambia gazeti moja la Italia kwamba hana maisha marefu katika jiji la London.

Alipoulizwa kuhusiana na kauli hiyo wakati akijiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Jumanne dhidi ya Roma, alisema alimaanisha hatokaa London baada ya kustaafu soka. <p.''Nina furaha sana hapa, na ninafurahia kila kitu cha London mimi na mke wangu,''alisema.

Morata mwenye miaka 25 amefunga magoli saba katika michezo 13 tokea aliposajiliwa kwa Pauni Milioni 60 kutoka klabu ya Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano.

TANZIA: NDIKUMANA AFARIKI DUNIA GHAFLA BAADA YA MAZOEZI

Mchezaji wa timu ya taifa ya Rwanda na beki wa zamani wa klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Ndikumana Hamad Katauti amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka ghafla.

Taarifa kutoka Kigali, Rwanda zinaeleza kuwa Hamad Kataut kabla ya kufikwa na umauti alikuwa mazoezini jana asubuhi.

Katauti alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, enzi za uhai wake na aliwahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga akitokea timu ya Cyprus.

Ndikumana alikuja nchini siku ya Simba Day Agosti 8 mwaka huu akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kufungwa bao 1-0.

Mchezaji Ndikumana Hamad amewahi kuwa mume wa muigizaji filam maarufu nchini, Irene Uwoya.

TIGER WOODS YUKO FITI KUREJEA UWANJANI

Tiger Woods anatarajiwa kurejea tena katika mchezo wa gofu miezi nane baada ya kuandamwa na majeraha.

Atajitupa uwanjani kuanzia Novemba 30 mpaka Desemba 3.

Woods mshindi wa vikombe 14 vya kimataifa, anapona majeraha ya upasuaji wa mgongo aliyofanyiwa miaka mitatu iliyopita ambayo kwa wakati fulani alikuwa akirudia upasuaji mara kwa mara na kumfanya kuwa dhaifu.

Alijiondoa katika michuano ya Dubai mwezi Februari kwa sababu hiyohiyo.

''Ninajipanga kurejesha heshima yangu, furaha yangu na uwezo wangu kupitia mchezo ninaoupenda, alisema Woods''

Woods hajashinda taji lolote kubwa tokea mwaka 2008.

PENZI KATI YA SELENA GOMEZ NA THE WEEKEND IMEBAKI STORI

Ni kama miezi kumi toka tumuone Selena Gomez na mpenzi wake The Weeknd aliyerithi mikoba ya Justin Bieber katika mahaba ila kwa sasa penzi la wawili hao imebaki stori.

Vyanzo vya karibu zimeeueleza mtandao wa People kuwa wawili hao waliwahi kuachana kwa muda ila wakarudiana na sasa huwenda ndio ikawa mwisho. Kwani Selena amekuwa akijaribu kuwa karibu hata kwenye matamasha ya mpenzi wake ila Abel(The Weeknd) haonyeshi ushirikiano.

‘Always made an effort” to attend his shows when she could, “that played a part in them getting distant,” adds the insider. “It’s over for now, but they’re still in touch,” kimeleza chanzo hicho kikimkingia kifua Selena.

Siku chache zilizopita Selena na Justin Bieber walinaswa na kamera za TMZ wakiwa katika mgahawa wa maeneo ya Westlake Village, California -Marekani jambo linaloashiria huwenda wamerudiana.

Selena na Justin Bieber wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi toka mwaka 2011-2015 walipoachana ila wawili hao bado wanaonyesha hali ya kutamaniana mara kwa mara.

LAMAR ASEMA PRODUCER WA BONGO WANATOZA GHARAMA ZA CHINI ZAIDI AFRIKA

Kutokana na hilo Lamar ameshauri kuwa ni vema kwa wasanii kutoa sapoti kwa producer wa Bongo na si vinginevyo.

“Soko letu katika producers sisi ndio ambao tunatoza gharama za chini kimuziki Afrika, ukienda South Africa watu wanachajiwa mpaka dola 5,000 kurekodi lakini sisi gharama za juu sidhani hata kama inafika milioni mbili/tatu” Lamar ameiambia Safari Media.

“Kwa hiyo wasanii wanatakiwa wasapoti producer wao, unakuta msanii anaweza kwenda South Africa akalipia labda dola 3,000 kufanya wimbo lakini huku hataki kulipia hela hiyo au anataka bure” ameongeza.

Producer wa muziki kutoka studio za Fish Crab, Lamar amesema producer wa Bongo wanatoza gharama za chini zaidi katika kurekodi ukilinganisha na nchini nyingine Afrika.

ALIKIBA AKATAA KUITWA ‘MUNGU WA BONGO FLAVA

Jinsi mashabiki wa soka wanavyochizika muda mwingine, ndivyo hivyo hata katika muziki. Kitu hiki kimemtokea shabiki mmoja wa Alikiba kitu kilichopelekea kumuita msanii huyo ‘Mungu wa Bongo Flava’.

Hata hivyo kilikuwa ni kitu ambacho hakikumpendeza Alikiba, ndipo alipoamua kumjibu shabiki huyo ambaye anatumia jina la Kibasalu katika mtandao wa Instagram;

 

 

Officialalikiba @kibasalu naomba msiniite hivyo siwezi kuwa wala siwezi kukubali imani yetu haturuhusu kujiita au kuitwa na mtu yoyote ule jina la MUUMBA.

Comment hiyo ya Alikiba inakuja mara baada ya shabiki huyo kwenda kwenye moja ya picha za msanii huyo katika mtandao wa Instagram na kuandika, ‘Bongo flaver god’.

ANTHONY JOSHUA AJIPA TUMAINI MWAKA 2018

Bondia Anthony Joshua amesema upo uwezekano wa mwaka 2018 kuanza vizuri baada kumaliza 2017 kwa kumchapa Carlos Takam.

Joshua bingwa wa uzito wa juu wa taji la WBA na IBF aliendeleza ushindi wake alioupata mwezi April dhidi ya Wladimir Klitschko kwa kumchapa Takam ndani ya raundi 10 mjini Cardiff.

Mdhamini wake Eddie Hearn amesema kuna uwezekano akachauana na Deontay Wilder huku kocha wake Rob McCracken akimtaja Joseph Parker kuwa anafaa zaidi.

Antony Joshua amekuwa miongoni mwa wanamichezo wanaovutia zaidi kwa siku za karibuni, huku akiweka rekodi ya kushinda kwa asilimia mia moja kwenye michuano yake yote.

Page 3 of 67