blog category

 

 

SERGIO RAMOS NA MPENZI WAKE PILAR RUBIO WAPATA MTOTO WA TATU

Beki kisiki wa klabu ya ska ya Real Madrid, Sergio Ramos na mpenzi wake Pilar Rubio wamefanikiwa kupata mtoto wao wa tatu.

Ramos amethibitisha hilo kupitia mtandao wa Instagram ambapo ameweka picha akiwa na Pilar na mtoto wao huyo na kuandika, “We are very happy to introduce you to Alejandro, born today at 6:24PM, 3.1kg. Thank you for sharing our joy. I love you Pilar Rubio.”

Mtoto huyo amezaliwa jana (Jumapili) akiwa na uzito wa 3.1kg na tayari amepewa jina la Alejandro.

Mtoto huyo anaungana na kaka zake wengine wawili akiwemo Sergio Jr (3) na Marco (2).

FAIZA ALLY AMTELEKEZA SUGU GEREZANI

MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye ni mzazi mwenza na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu, Faiza Ally amefunguka kuhusu kumpelekea mtoto gerezani kumuona baba yake huyo alikofungwa kwa miezi mitano.

Akizungumza na Safari Media baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kumpeleka mwanaye akamuone baba yake gerezani Mbeya na kumjulia hali, Faiza amesema kuwa, hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Sugu siyo ndugu yake.

“Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto akamuone gerezani kwa sababu kwanza siyo ndugu yangu, siyo rafiki yangu na siyo mpenzi wangu. Mapenzi yalishaisha zamani, amebakia kuwa baba wa mtoto, basi, hayo mengine siwezi kuyafanya kwa kweli,” alisema Faiza.

Sugu yupo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya akitumikia kifungo cha miezi mitano aliyohukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 26.03.2018

Meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa Arsenal Arsene Wenger mwisho wa msimu. (Kicker - kwa Kijerumani)

Hilo lisipofanyika, Tuchel basi badala ya kwenda Arsenal atajiunga na Paris St-Germain ya Ufaransa, ingawa Chelsea bado wanazisaka huduma zake. (Sportbuzzer - kwa Kijerumani)

Wawakilishi wa Barcelona watakutana na wenzao wa Atletico Madrid siku chache zijazo kwa lengo la kukamilisha makubaliano kuhusu uhamisho wa nyota Mfaransa Antoine Griezmann, 27. (Sport - kwa Kihispania)

Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ataihama klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote mwisho wa msimu huku Manchester City na Juventus wakidaiwa kumtaka iwapo klabu yake haitaongeza mshahara wake ambao kwa sasa ni £200,000 kila wiki. (Sun)

Manchester United wanamtaka beki wa Scotland wa miaka 20 anayechezea klabu ya Celtic Kieran Tierney. (Daily Record)

Inter Milan nao wamewapiku Manchester City na Barcelona na kupata saini ya beki Mholanzi Stefan de Vrij, 26, ambaye atajiunga nao kutoka Lazio bila ada yoyote mwisho wa msimu. (Gazzetta dello Sport - Kwa Kitaliano)

Kiungo wa kati kinda wa Manchester City Phil Foden, 17, na kinda anayechezea Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18, waliondolewa kwenye kikosi cha England cha wachezaji wa chini ya miaka 19 wanaocheza michuano ya ubingwa Ulaya baada yao kufika kwa mazoezi wakiwa wamechelewa. (Telegraph)

FILAMU YA "LAANA YA MKE" KUZINDULIWA RASMI KESHO IJUMAA MACHI 23

Mwaka mmoja baada ya kuachia Filamu ya ‘Nyama ya Ulimi’,Bongo Movies Shinyanga wanakuletea Filamu nyingine kali inaitwa “Laana ya Mke” ambayo itazinduliwa rasmi kesho Machi 23,2018.

Tayari wageni mbalimbali wakiwemo wasanii maarufu wa filamu nchini,viongozi wa bodi ya filamu wameshaanza kuwasili mjini Shinyanga kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa filamu hii ambayo imekuwa gumzo kila kona.

Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Juma Ibrahim Songoro ameiambia Ssafari Media, kuwa uzinduzi wa filamu ya Laana ya Mke utafanyika tarehe kesho katika ukumbi wa NSSF ya zamani “CCM mkoa wa Shinyanga” kuanzia saa tatu usiku.

Katika Filamu hii iliyoongozwa na Director mahiri Dave Skerah wamo Magwiji wa Filamu akiwemo Blandina Chagula ‘Johari’, Ibrahim Songoro ‘Songoro Gadafi’,Magreth Emmanuel, Mariam Bilal, Najma Shahel,Edward Joseph na Mzee Salum Kawelewele.

Filamu hiyo inahusu majanga na laana wanazopata wanaume wababe,wasio na fadhila wanaotafuta mali na wake zao kisha kuwafanyia ukatili.

MAUA SAMA AITAMANI GOSPO

HITMAKER wa Ngoma ya Mahaba Niue, Maua Sama amesema kuwa kati ya vitu anavyotamani kwenye muziki kwa sasa ni kujiingiza katika Muziki wa Injili ‘Gospo’.

Akizungumza na Safari Media Maua, anayebamba na Ngoma ya Nakuelewa amesema kuwa, japokuwa ni Muislam lakini amejikuta akitamani siku moja kuimba Injili.

“Napenda sana nyimbo za inspiration, kuna wakati nafikiria najikuta nikitamani kuimba hasa hizi za Gospo. Ipo siku nitaimba kwa sababu ni kitu ninacho-kipenda na kukitamani kutoka moyoni,” alisema Maua.

AFANDE SELE KUJIUNGA NA CCM

Rapa mkongwe nchini Tanzania, Afande Sele ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi leo Machi 15, 2018 mkoani Morogoro mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Afande Sele amesema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na rushwa na kuwajali wanyonge.

Hata hivyo, Mfalme huyo wa Rhymes amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi wampokee kwa mikono miwili.

Afande Sele kabla ya kujiunga na CCM alishawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na Chama cha ACT Wazalendo ambapo mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Rais Magufuli leo Machi 15, 2018 amezindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro ambapo Afande Sele alitumia nafasi hiyo kujiunga na CCM.

RAIS PUTIN AFUATA NYAYO ZA HITLER

Mwanasiasa maarufu wa Urusi, Boris Johnson amesema kuwa anaunga mkono kauli ya rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin kuwa ataitumia michuano ya kombe la Dunia kulifanya taifa hilo kuwa lenye amani kama alivyowahi kuitumia rais wa Ujerumani, Aldolf Hitler wakati wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 1936 katika masuala ya amani

Johnson amesema kuwa kutakuwa na mazungumzo ya haraka dhidi ya Urusi kuhusu usalama wa mashabiki katika mashindano hayo yajayo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi amesema kuwa raia wa nchi hiyo wameathirika na chuki iliyodumu kwa muda mrefu.

Mara kadhaa kumekuwa na matukio yakitokea ndani ya nchi hiyo ambayo huathiri wageni kwa namna moja ama nyingine. >Kuna maombi ya zaidi ya watu 24,000 kutoka Uingereza wakitaka kuwasili nchini Urusi kushuhudia kombe la dunia ukilinganisha na watu 94,000 waliyopata nafasi ya kushuhudia Rio mwaka 2014 nchini Brazili.

MAKAMU WA RAIS WA TFF, MICHAEL WAMBURA APIGWA AFUNGIWA MAISHA

Kamati ya maadili ya TFF, imemfungia kifungo cha maisha kutojihusisha na shughuli za soka Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Michael Wambura.

Wambura amekutana na adhabu hiyo nzito kutokana na kupokea fedha zisizo halali kiasi cha shilingi milioni 84 na makosa mengine matatu.

Makaosa hayo mengine matatu aliyokutwa nayo Wambura, ni kugushi nyaraka za malipo ya fedha, na kula njama kulipwa fedha na waliokua viongozi wa TFF Malinzi na Mwesigwa.

Kamati hiyo ya maadili imefikia maamuzi hayo kwenye kikao chao walichokutana jana (Jumatano).

Page 1 of 70