Maafisa wa polisi nchini Misri jana Jumapili wamewaua wanamgambo sita wanaoshukiwa kuhusika katika jaribio la mauaji lililoshindwa lililokuwa likimlenga afisa mkuu wa usalama siku moja kabla katika mji wa pwani wa Alexandria nchini humo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Misri katika taarifa yake imesema imebaini mtandao wa kigaidi katika nyumba moja ya makazi kwenye mkoa wa Beheira ulioko jirani na Alexandria ambako wanamgambo sita waliuawa wakati wa tukio la kufyatuliana risasi.

Hakukua na taarifa za mara moja za watu waliohusika na shambulizi hilo la bomu katika gari ambalo shirika la habari la serikali linalihusisha kufanywa na kundi la udugu wa kiisilamu lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh