Makamu wa rais wa bunge la Catalonia nchini Uhispania amelaani kutiwa mbaroni kwa aliyekuwa kiongozi wa jimbo hilo aliyeko uhamishoni Carles Puigdemont.

Polisi wa Ujerumani walimkamata Puigdemont baada ya kuvuka mpaka wa Denmark Jumapili hatua iliyoibua maandamano katika jimbo la Catalonia.

Makamu wa rais wa jimbo la Catalonia pia ameshutumu mahakama ya Uhispania kwa kumshikilia mgombea wa nafasi ya urais wa jimbo la Catalonia Jordi Turull wakati bunge lilipojaribu kumchagua kushika wadhifa huo.

Viongozi wengine tisa wa jimbo la Catalonia wanaounga mkono kujitenga wako gerezani na wengine watano wako uhamishoni.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh