Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamethibitisha kwamba wanafanya uchunguzi baada ya kupokea ripoti kwamba mkewe rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe amekuwa akisafirisha pembe za ndovu.

Vyombo vya habari vya serikali vinasema kuwa mamlaka ya wanyama pori nchini humo ilifichua kwamba Grace Mugabe kinyume na sheria alisafirisha kiwango kikubwa cha pembe za ndovu hadi China, Marekani na UAE .

Mpiga picha mmoja wa wanyama pori Adrian Steiirn alisema kuwa alipata thibitisho la kashfa ya usafirishaji pembe hizo zinazohusishwa na bi Grace Mugabe baada ya kufanya kazi kama jasusi nchini Zimbabwe.

Inadaiwa kwamba Bi Mugabe alifanikiwa kusafirisha pembe hizo kupitia uwanja wa ndege wa taifa hilo bila kufanyiwa ukaguzi wowote.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh