Nyota wa zamani wa kandanda duniani George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.

Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.

Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.

Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."

Kiongozi huyo ametumia hotuba yake kusifu uhusiano wa karibu kati ya taifa hilo na Marekani na China.

Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.

Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo katika uwanja wa Samuel Doe viungani mwa mji wa Monrovia.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh