Makundi ya wanawake kutoka mashirika tofuati nchini Kenya yameandamana ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua kuhusiana na madai kuwa akina mama waliojifungua wamekuwa wakidhulumiwa kingono katika Hospitali kuu ya Taifa, Kenyatta National Hospital.

Maandamano hayo yanafanyika wakati ambapo ripoti ya uchunguzi uliyoagizwa na waziri wa afya nchini humo inatarajiwa kutolewa rasmi.

Waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu aliagiza uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.

Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao siku ya Ijumaa zinadai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.

Wanaotuhumiwa ni wahudumu katika vyumba vya maiti, wanaonyooshewa kidole pia kwa kutumia maiti kuwashutua akina mama waliojifungua katika hospitali hiyo.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh