Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel ameitolea wito Sudan Kusini kuongeza jitihada za kutafuta amani nchini humo.

Wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Juba, Gabriel amesema hatua zaidi zinahitaji kuchukuliwa ili kuleta amani na taifa hilo lisonge mbele kuleta maendeleo ya kiuchumi pamoja na kuijenga tena nchi.

Gabriel ametoa matamshi hayo kufuatia ziara yake katika kambi kubwa kabisa ya wakimbizi nchini Uganda, inayohifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini wapatao milioni moja.

Sudan Kusini imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013, baada ya mzozo kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar. Maelfu ya watu wameuwawa na zaidi ya milioni nne wamepoteza makaazi yao.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh