Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambae yuko London kwa ajili ya matibabu, amefanya mkutano wake wa kwanza na anaye kaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili sasa.

Msemaji wa kaimu Rais, Yemi Osinbajo, ameelezea kuwa mkutano huo ulikuwa mzuri.

Buhari amekuwa jijini London tangu mwezi Mei, akipata matibabu kwa ugonjwa ambao haujatajwa.

Bwana Osinbajo anategemewa kurudi nchini Nigeria baada ya mkutano huo.

Ukimya wake umeibua mjadala nchini Nigeria iwapo Buhari ataweza kurudi na kuendelea na majukumu yake ama la.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh