blog category

TOM THABANE AGEUKA MBOGO MAUAJI YA MKUU WA JESHI LESOTHO

Waziri mkuu wa Lesotho ameelezea mauaji ya mkuu wa kikosi cha jeshi Khoantle Mots'omots'o yaliyofanywa na maafisa wa jeshi kama kitendo cha kurudisha nyuma juhudi za kutafuta amani nchini humo.

Tom Thabane amesema upelelezi unaendelea juu ya tukio hilo lililotokea katika mji mkuu Maseru siku ya Jumanne.

Mashuhuda wanasema, watu wawili waliovalia sare za jeshi waliingia katika ofisi ya Mots'omots'o na kisha kumfyatulia risasi kabla ya wao kuuawa na walinzi wa kiongozi huyo.

Lesotho ipo katika hali ya taharuki, ikiwa na hostoria ya mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara.

KOREA KUSINI YAFANYA MAJARIBIO YA MAKOMBORA KUJIBU MAJARIBIO YA KOREA KASKAZINI

Korea Kusini imefanya mazoezi ya makombora yake kuashiria shambulizi dhidi ya Korea Kaskazini, kujibu jaribio la sita la nyuklia lililofanywa na Korea Kaskazini.

Mazoezi hayo yalihusu kurushwa kwa makombora ya masafa marefu kutoka kwa ndege za kivita na ardhini.

Hii ni baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis kuonya kuwa tisho lolote kwa Marekani au washirika wake kutoka Korea Kaskazini litajibiwa vikali kijeshi.

Korea Kaskazini ilisema kwa ilifanyia jaribio bomu la haidrojeni linaloweza kuwekwa kwa kombora la masafa marefu.

Korea mara kwa mara imekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na shinikzo za kimataiafa ya kuitaka iachane na mpango wake wa zana za nyuklia.

Ndani ya miezi mwili iliyopita, Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombra ya masafa marefu na hata kurusha kombora kupitia juu ya anga ya Japan hadi bahari ya Pacific.

Korea Kaskazini yasifia jaribio jingine la nyuklia

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura leo kujadili jibu la hatua hiyo ya Korea Kaskazini.

ZIKA KUTIBU SARATANI YA UBONGO

Virusi hatari vinavyoweza kusababisha madhara kwa ubongo wa watoto vinaweza kusaidia kwenye matibabu mapya kwa saratani ya ubongo kwa mtu mzima, kwa mujibu wa wanasayansi nchini Marekani.

Hadi sasa virusi vya Zika vinaonekana tu kuwa tisho la afya duniani.

Lakini utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa virusi hivi vinaweza kuvamia na kuua seli zinazosababisha saratani ya ubongo wa mtu mzima.

Majiribio yaliyofanyiwa panya yalionyesha kuwa virusi vya Zika vilikula seli za saratani ya ubongo.

Binadamu bado hawajafanyiwa utafiti huo, lakini wataalamu wanaamini kuwa virusi hiyo vinaweza kuingizwa kwa ubongo wa binadamu wakati wa upasuaji ili kuangamiza seli za saratani ya ubongo.

Pia matibabu hayo ya kutumia Zika yameonekana kufaulu kwenye sampuli za binadamu katika mahabara.

Aina hii ya saratani husambaa kwa haraka, ikimaanisha kuwa ni vigumu kubaini imeanzia wapi na kuishia wapi.

MERKEL ASEMA UTURUKI HAIWEZI KUINGIA UMOJA WA ULAYA

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa anaamini kuwa Uturuki haiwezi kuingia kwenye umoja wa ulaya na kusema kuwa atahakikisha anasisitiza kutokuwepo kwa mazungumzo ya kukubaliwa Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Markel ambae anawania kushinda muhula wa nne katika uchaguzi utakaofanyika mwezi huu amezungumza hayo katika mdahalo na mpinzani wake Martin Schulz ulioonyeshwa kwenye televisheni.

Mahusiano kati ya Berlin na Ankara yameingia mashakani baada ya raia wa ujerumani kuwekwa kizuizini nchini Uturuki.

Mdahalo huo ulikijita katika suala la maelfu ya wahamiaji waliongia ujreumani.

CARIBBEAN WAFANYA MAANDALIZI YA MWISHO KABLA KUWASILI KIMBUNGA IRMA

Visiwa vilivyo eneo la Caribbean vimefanya matayarisho ya mwisho kwa kimbunga Irma, ambacho ni kimbunga chenye nguvu zaidi kwa mwongo mmoja, huku maafisa wakionya kuwa kimbunga hicho kinaweza kuwa chenye madhara makubwa.

Kimbunga Irma cha kiwango cha tano kimepata nguvu ya upepo wa kasi ya hadi kilomita 295 kwa saa.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga visiwa vya Leeward kabla ya kuelekea huko Puerto Rico, Haiti na Floirda.

Watu wameamrishwa kuondoka kwa lazima eneo la magharibi mwa Florida.

Wageni watatakiwa kuondoka Jumatano asubuhi huku wenyeji nao wakitakiwa kunodoka ifikapo jioni na safari zote za ndege kusitishwa.

Viwanja vya ndege vimefungwa kwenye visiwa kadha, maeneo maarufu ya kustarehe na mamlaka zimewataka watu kuenda maeneo salama.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza hali ya tahadhari huko Florida, Puerto Rico ba visiwa vya Virgin na kutangaza mikakati ya kukabiliana na majanga sehemu hizo.

SOMALIA YAONYA MPANGO WA ALSHABAB KUSAMBAZA URANIUM IRAN

Serikali nchini Somalia imeonya kuwa wapiganaji wa Alshabab wana mpango wa kusambaza uranium huko Iran wakipata msaada kutoka Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Somalia Yusuf Garaad amesema kuwa wapiganaji hao wamekua wakichimba madini ya uranium katika mkoa wanaoushikilia.

Idara ya ulinzi ya Marekani haijatoa maelezo yoyote.

MAREKANI YAPANGA KUIPIGA KOREA KASKAZINI IKIMGUSA MSHIRIKA WAKE

Waziri wa masuala ya ulinzi wa marekani James Mattis amesema kuwa tishio lolote kutoka korea kaskazini kwa Marekani ama washirika wake litajibiwa vikali na jeshi.

Mattis amezungumza hayo baada ya mkutano wake na Rais Trump juu ya masuala ya usalama wa nchi kufuatia jaribio la nyuklia huko Pyongyang.

Trump ameonya kuwa Marekani inaweza kusimamisha kufanya biashara na nchi yoyote inayoshiriki biashara na Korea Kaskazini.

Mwanafunzi anayetaka ukasomee Korea Kaskazini.

China ndio mshirika mkuu wa baishara na Pyongyang, ameongeza kuwa korea kaskazini imekua tishio na imeleta fedheha kwa Beijing.

Nayo korea kusini imesema kuwa imefanya majaribio matano kama majibu ya jaribio la nyuklia la korea kaskazini.

KIFO CHA NAJI KUCHUNGUZWA UPYA

Polisi wa Uingereza wamesema wanachunguza tena mauaji ya mchora Katuni wa Kipalestina Naji Al-Ali.

Aliepigwa risasi wakati alipokuwa akitembea kuelekea ofisini kwake jijini London Julai 1997.

Naji al- Ali anajulikana zaidi kutokana na katuni zake ambazo zilikuwa zikichapishwa katika gazeti la Kuwaiti, na mara kadhaa alikuwa akiwashutumu viongozi wa Kiarabu na utawala.

Polisi wa mji wa London wamesema wanamatumaini kwamba watu ambao hawakutaka kuzungumza wakati mauaji yalipotokea pengine sasa wataweza kuzungumza.

Page 10 of 101