blog category

RAIS KENYATTA ASEMA UAMUZI WA MAHAKAMA KENYA NI 'MAPINDUZI

Rais wa kenya Uhuru Kenyatta ameutaja uamuzi wa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kuwa mapinduzi ya mahakama.

Viongozi hao wawili walikuwa wakijibu uamuzi kamili wa mahakama ambapo majaji wa mahakama ya juu walitoa sababu zao kwa nini walifutilia mbali matokeo hayo ya urais.

Idadi kubwa ya majaji hao walisema kuwa matokeo hayo hayakuwa na 'uwazi wala kuhakikiwa'.

Viongozi hao wawili hatahivyo waliangazia uamuzi wa majaji wawili waliopinga uamuzi hao ambao walisema kuwa kesi iliowasilishwa katika mahakama hiyo haikuwa na uzito wowote.

Amesema kuwa mafanikio yote ya katiba mpya ilioidhinishwa 2010 yamepotezwa na uamuzi huo ambao umewawacha watu wachachee kuongoza dhidi ya walio wengi.

Amesema kuwa katiba ilikuwa imeweka maadili ya kidemokrasi , ugatuzi na kuwapatia raia haki na uhuru na kupunguza mamlaka ya urais ili raia waamue wanavyotaka.

MASIKINI;MSICHANA ALIYEBAKWA NA WALIMU INDIA YUKO MAHUTUTI

Msichana wa India ambaye alidaiwa kubakwa na walimu wawili wa shule katika kipindi cha wiki tatu yuko katika hali mahututi baada ya kulazimishwa kuavia mimba..

Polisi imemtioa nguvuni Mkuu wa shule yake na mwalimu wake katika jimbo la kaskazini mwa India la Rajasthan.

Polisi wanasema kuwa alipoteza fahamu baada ya washukiwa skumlazimisha kutoa mimba katika hospitali ya kibinafsi.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 18 alilazwa hospitalini baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo na wahudumu katika shule yake wakabaini kwamba alikuwa mjamzito.

Hali yake ya afya ilianza kuwa mbaya kwa haraka baada ya kuavia mimba, lakini haijafahamika wazi ni nini hasa kilichoifanya hali yake kuwa mbaya,alisema polisi katika wilaya ya Sikar said.

Polisi wanaamini kuwa masomo ya ziada yanayotolewa katika saa ambazo si za kawaida yalitumiwa kuwaita wanafunzi ili kuwezesha vitendo kama hivyo vya unyanyasaji kufanyika.

TRUMP AONGEZA VIKWAZO ZAIDI KWA KOREA KASKAZINI

Rais Donald Trump amesaini sheria mpya ya kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini juu ya mpango wake wa nuklia.

Waziri wa fedha wa Marekani ameidhinisha vikwazo hivyo dhidi ya makampuni ya fedha yanayofanya biashara zake ndani ya Korea Kaskazini.

Rais Trump pia amesema kuwa Benki Kuu ya Uchina iliagiza benki nyingine za Uchina kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.

Hatua hii inakuja katika kipindi cha chini ya wiki mbili baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo ipya dhidi ya taifa hilo kwasdababu ya jaribilo lake la hivi karibuni la nuklia.

Hali ya wasi wasi imetanda katika kipindi cha wiki za hivi karibuni kutokana na hatua ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa tajiri zaidi duniani.

KOREA KASKAZINI YAFANANISHA HOTUBA YA TRUMP NA MBWA

Mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini ameifananisha hotuba ya Trump kwa Umoja wa Mataia na kibweko cha mbwa.

Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Bw Trumo alisema kuwa ataiharibu Korea Kaskazini ikiwa itakuwa tisho kwa Marekani na washirika wake.

Matamshi ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Ri Yong-ho, ndiyo ya kwanza rasmi ya Korea Kaskazini tangu hotuba ya Trump.

Korea Kaskazini imendelea na mpango wake wa nyuklia na kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza kuhusu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un, Bw Trump aliuambia Umoja wa mataifa kuwa Bwana Kim ako katika mikakati ya kujitia kitanzi.

Bwana Ri anatarajiwa kutoa hotuba yake kwa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.

Wataalamu wanasema kuwa Korea Kaskazni imaharakisha mipango yake ya kuunda makombora ya masafa marefu na mipango yote ya nyuklia.

ROUHANI WA IRAN AIKOSOA HOTUBA YA TRUMP KWA UMOJA WA MATAIFA

Rais Hassan Rouhani wa Iran ametumia hotuba yake kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kumshambulia rais wa Marekani Donald Trump, kutokana na lawama alizotoa dhidi ya nchi yake.

Kwenye hotuba kwa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, rais Trump aliijumuisha Iran kuwa kati ya mataifa maovu duniani.

Amesema kuwa nchi yake haitachukua hatua za kwanza kukiuka makubalaniano lakini akasema Iran itajibu hatua yoyote ya kukiuka makubaliano hayo.

Ikulu ya White House mwezi uliopita ilisema kuwa Iran ilikuwa inatimiza makubaliano hayo lakini Trump anasema kuwa Iran inayakiuka.

Mwaka 2015 Iran iliafikia makubaliano na mataifa mengi makubwa duniani yakiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani.

Vikwazo vya kuharibu uchumi dhidi ya Iran viliondolewe na shirika la kudhibiti nyuklia duniani likasema kuwa Iran imepunguza shughuli zake za nyuklia.

Iran inasema kuwa ina haki ya kuwa na nishati ya nyuklia na imesisitiza kuwa mpango wake ni wa amani.

SUU KYI: AIPUUZA UN

Kiongozi wa Myanmar Aung San Suu kyi amesema kuwa serikali yake haina hofu ya kuchunguzwa kuhusu njia inashughulikia suala la watu wa Rohingya.

Ilikuwa hotuba yake ya kwanza kwa nchi kuhusu ghasia katika jimbo la Rakhine ambazo zimesababisha zaidi ya watu 400,000 wa jamii ya Rohingya kuvuka mpaka na kuingia nchini Bangladesh.

Kwenye hotuba yake kwa bunge la Mynammar, Aung San Suu kyi alisema amuhusuniswa na kuendelea kutaabika kwa watu wote katika mzozo huo na kwamba Myanma imejitolea kutatua suala hilo kwa jamii zote nchini humo.

Bi Suu kyi ambaye ameamua kutohudhuria mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa mjini News York badaye wiki hii, alisema kuwa alikuwa anataka jamii ya kimataifa kufahamu kile kilichokuwa kikifanywa na serikali yake.

BAADA YA KIMBUNGA MARIA: KISIWA CHOTE CHA PUERTO RICO HAKINA UMEME

Kimbunga Maria kimekata umeme katika kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu milioni 3.5.

Abner Gómez, ambaye ni mkuu wa utoaji huduma za dharura alisema kuwqa hakuna mtu anayetumia umeme aliye na huduma hiyo kwa sasa.

Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hyo.

Maria kwa sasa kinaondoka nchini Puerto Rico na kumepunguza nguvu zake hadi kiwango cha pili.

Baada ya kimbunga Maria kuipiga Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia manyumbani mwao kuanzia saa kumi na mbili jioni na hadi saa kumi na mbili asubuhi.

Hi ni hatua ya kuwazuia watu kupata ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka na vifuzi vilivyo barabara za mji.

Mapema Bw Rossello alimuomba Rais Donald Trumo kukitangaza kisiwa hicho kuwa eneo la janga baada ya kimbunga kusababisha mafuriko makubwa na upepo unaotishia maisha.

Alisema kuwa kuna uwezekano wa uharibu mkuwa licha ya vitisho 500 kubuniwa kuwalinda watu.

Kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 7 katika kisiwa cha Dominica ambacho kiliathiriwa vibaya siku ya Jumatatu

KIMBUNGA CHENYE NGUVU MARIA CHAHARIBU DOMINICA

Kimbunga Maria kilichopata nguvu na kufikia kiwango cha tano kimepiga kisiwa cha Caribbean cha Dominica kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 260 kwa saa.

Waziri mkuu Roosevelt Skerrit aliandika katika mitandao ya kijamii kuwa paa la nyumba yake limeng'olewa.

Alisema nyumba yake ilifurika maji na baadaye kusema kuwa alikuwa ameokolea.

Uwanja wa ndege wa Dominica na bandari vimefungwa.

Maria kinapitia njia ambayo kimbunga kama hicho wa jina Irma kilisababisha uharibifu wakati kikipitia eneo hilo mwezi huu.

Kisiwa kilicho karibu cha Martinique kiliwekwa katika tahadhari huku kingine cha Ufaransa cha Guadeloupe kiliwaamrisha watu kuondoka.

Baadhi ya sehemu hizo bado zinarejea hali ya kawaida baada ya kupigwa na kimbunga Irma , ambacho ni kimbunga cha kiwango cha tano kilichosababisha vifo vya watu 37 na kusababisha hasara ya mabiliono ya dola.

Visiwa vinavyokumbwa na kimbunga Maria ni pamoja na visiwa vya Leeward vikiwemo Antigua na Barbuda.

Kituo cha vimbunga cha Marekani (NHC) kiliongeza nguvu ya kimbunga hicho siku ya Jumatatu kutoka kiwango cha pili hadi kiwango cha nne na kisha kiwango cha tano ambacho ni kiwango cha juu zaidi.

Watabiri wa hali ya hewa walionya kuwa mvua kubwa inayosababishwa na kimbunga hicho inaweza kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo ya kutishia maisha.

Page 9 of 104