blog category

RAIS PAUL BIYA ALAANI VURUGU, CAMEROON

Rais wa Cameroon, Paul Biya amelaani ghasia zilizotekelezwa na pande zote baada ya polisi kuwapiga risasi na kuwauwa watu nane wakati wa maandamano ya raia wa nchi hiyo wanaozuungumza kiingereza wanaotaka kujitenga kuwa na eneo lao.Watu wanane wamejeruhiwa katika ghasia hizo.

Ghasia hizo zimetokea wakati wa maadhimisho ya miaka miaka hamsini na sita tangu kujumuishwa kwa jimbo la wazungumzaji wa kiingereza ndani ya Cameroon.

Wazungumzaji wa lugha ya Kiingereza ambao ni wachache wamekuwa wakiandamana takriban mwaka sasa kwa kile wanachosema kubaguliwa katika mfumo wa elimu na sheria.

UPINZANI NCHINI KENYA WAITISHA MAANDAMANO

Chama cha upinzani nchini Kenya NASA kimeitisha maandamano Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.

Hatua hii ni ya kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa August 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini.

NASA umeeleza kwamba hautovamia makao ya tume ya IEBC kama ilivyotajwa awali kuwatimua kwa lazima maafisa hao, badala yake unasema maandamano yatakuwa ya amani katika barabara za mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwao.

Hilo ni mojawapo ya masharti iliyotoa NASA kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.

Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wapinzani ambao amesema watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi za raia wa nchi hiyo.

Upinzani unasisitiza kuwa una haki ya kuandamana kwani hata upande wa serikali - Muungano wa Jubilee - umeshafanya maandamano kama hayo hivi juzi walipoelekea katika mahakama ya juu zaidi wakitaka majaji wa mahakama hiyo waondolewe.

HATIMAE CATALONIA IMEKUWA HURU'

Kiongozi wa neo la Catalonia Carles Puigdemont anasema kuwa eneo la Uhispania limepata haki ya kuwa huru kufuatia kura ya maoni yenye utata ambayo imekubwa na ghasia.

Alisema kuwa sasa mlango umefunguliwa kwa eneo hilo kutangazwa kuwa huru.

Maafisa wa Catalonia baadaye walisema kuwa asilimia 90 ya wale walioapiga kura waliunga mkono uhuru kwenye kura ya maoni ya siku ya Jumapili.

Mahakama ya katiba nchini Uhispania imeitangaza kuta hiyo ya maoni kuwa iliyo kinyume na sheria na mamia ya watu walijeruhiwa wakati polisi walitumia nguvu kujaribu kuzuia zoezi hilo.

Polisi walichukua makaratasi ya kupigia kura na masanduau kutoka kwa vituo vya kupigia kura.

MERKEL ASISITIZA KUWA NA MSIMAMO WA CHAMA CHAKE

Kansela wa Ujerumani ,Angela Merkel amesema kuwa chama chake hakitaegemea sera za mrengo wa kulia kujaribu kuwashawishi wapiga kura ambao walimuacha wakati alipokuwa anapambana na chama kinachopinga sera za uhamiaji cha AfD wakati wa uchaguzi wa jumapili.

Lakini Merkel amesema atajaribu awezavyo kurejesha Imani ya idadi kubwa ya watu ambayo walijisikia kutengwa.

Mafanikio ya chama cha mrengo wa kushoto cha AfD

Kimekiacha chama chake Merkel,CDC bila kuwa na na mshirika wa wazi kuunda serikali.

Merkel amesema alitaka kuunda serikali imara ambapo amezungumza na chama cha Liberals na Greens pamoja na So Social Democrats ambao walijitoa kuungana kwa mara nyingine na Christian Democrats.

WASHAURI WA TRUMP WASHUTUMIWA KUTUMIA BARUA PEPE BINAFSI

Gazeti moja la Marekani limeandika kuwa, washauri sita wa karibu wa rais Trump wamekuwa wakitumia barua pepe binafsi kuzungumzia masuala yahusuyo Ikulu ya Marekani tangu rais Trump kuingia madarakani.

Gazeti la New York times limeyataja majina ya washauri hao na mtoto wake Ivanka ni miongoni mwao.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, rais Trump alitishia kuwafunga wapinzani wake pale ambapo Hillary Clinton alipotumia barua pepe yake ya binafsi wakati alipokuwa katibu wa serikali ya Marekani.

Na siku ya jumapili, mume wa Ivanka, Jared Kushner alitajwa pia kutumia barua pepe yake binafsi kuwasilisha shughuli za serikali.

Gazeti moja la Marekani limeandika kuwa, washauri sita wa karibu wa rais Trump wamekuwa wakitumia barua pepe za binafsi kuzungumzia masuala yahusuyo Ikulu ya Marekani tangu rais Trump kuingia madarakani.

VIJANA WAANDAMANA GUINEA NA KUCHOMA MOTO KITUO CHA POLISI

Mamia ya vijana wamefanya maandamano katika maeneo ya uchimbaji madini nchini Guinea, huku wakichoma moto kituo cha polisi na kuwasha moto kwenye jengo lingine la umma.

Habari kutoka mji wa Kolaboui, katika Wilaya ya Boke, zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya walinda, usalama na waandamanaji waliokuwa na rungu.

Wakaazi wa eneo hilo wanadai kutonufaika na utajiri wa madini ulio katika eneo lao.

Madini hayo ya Bauxite hutumika kuzalishia Alumini.

MAREKANI YALIA NA KOREA KASKAZINI

Marekani imeilalamikia Korea Kaskazini, kwa kauli yake kuwa ina haki ya kuzitungua ndege za kivita za Marekani hata kama zipo nje ya anga la taifa hilo.

Msemaji wa ikulu ya Marekani ya white house Sarah Huckabee Sanders, amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini kwamba Marekani imetangaza vita,ni ya kipuuzi.

Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ni kufuatia ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter,uliokuwa ukisema utawala wa Pyongyoung hauwezi kudumu kwa muda mrefu.

Akizungumza katika kituo cha mafunzo cha kimataifa mjini Washington,Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha, amesema dunia inapaswa kupatiwa nafuu na maudhi ya Korea Kaskazini.

Hatuwezi kuwa na vita nyingine katika ukanda wetu,hatuwezi kuwa na vita katika rasi ya Korea. Madhara yake hayawezi kuwa kwa bara la Asia tu,bali hata kwa kaskazini mashariki mwa Asia na jamii ya kimataifa kwa ujumla.

Hatuwezi kuhatarisha usalama wa raia wetu,waliofanya kazi ya kujenga demokrasia kwa miongo saba sasa na ujenzi wa uchumi kutokana na vita vilivyowahi kutokea..")

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon Kanal Robert Manning amesema iwapo Korea kaskazini haitaacha vitendo vyake vya kuudhi,watatoa idhini kwa Rais kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini. Naye Balozi China wa umoja wa mataifa Liu Jieyi amesema suala hili linaingia katika hatua ya hatari.

Korea Kakskazini mbali ya kuwekewa vikwazo,imeendelea na majaribio yake ya Nyuklia na makombora,kinyume na msimamo wa umoja wa mataifa

KINGA MPYA YA MWILI INAYOWEZA KUSHAMBULIA 99% YA HIV YATENGENEZWA

Wanasayansi wamekuwa wakitengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi na hivyo kuzuwia maambukizi kuendelea.

Chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.

Kazi ya utengenezaji chembe chembe hizo za kinga ya mwili imetokana na ushirikiani baina ya Taasisi ya Marekani ya Afya na kampuni maduka ya dawa ya Sanofi.

Shirika la kimataifa la kukabiliana na ukimwi -International Aids Society linasema kuwa huu ni "ugunduzi wa kihistoria ".

Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuwia ama kutibu maambukiziya HIV

Miili yetu huhangaika kupigana na virusi vya HIV kwasababu virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kujibadilisha katika hali nyingine pamoja na muonekano wake.

Aina kadhaa za virusi vya HIV - katika mgonjwa mmoja zinaweza kufananishwa na zile za mafua wakati wa msimu wa baridi.

Kwa hiyo mfumo wa kinga ya mwili najipata katika vita dhidi ya magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababishwa na HIV.

Watafiti wamekuwa wakijaribu kutumia uwezo wa mwili wenyewe wa kupunguza uharibifu wa kinga ya mwili kama njia ya kutibu HIV, ama kuzuwia maambukizi hayo mapema.

Page 8 of 104