blog category

MMOJA WA PACHA WALIOTENGANISHWA INDIA ATIA TUMAINI

Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India.

Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake. Ngugu yake, Kalia hata hivyo bado hajapata fahamu.

Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha.

Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus.

Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa.

MAHAKAMA YA JUU NCHINI KENYA KUSIKILIZA KESI UCHAGUZI

Mahakama ya juu nchini Kenya leo Jumatano itasikiliza kesi ya dharura iliyowasilishwa na wapiga kura watatu dakika za mwisho wakidai kuwa Kenya haiko tayari kufanya uchaguzi huo.

Mahakama imeombwa kuingilia kati na kuamua - iwapo uchaguzi wa marudio utafanyika..

Wanataka uchaguzi huo uahirishwe.

Rais Uhuru Kenyatta anasema uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa siku ya Alhamisi.

Muungano wa upinzani chini ya kinara Raila Odinga umetaka wafuasi wake wasusie zoezi hilo, ukiutaja kuwa uchaguzi usioweza kuwa wa huru na wa haki.

Odinga amesema Serikali ya Kenya na tume ya Uchaguzi zimeshindwa kushughulikia mapungufu yaliyosababisha mahakama ya juu zaidi nchini humo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Agosti.

Hatua hiyo inajiri baada ya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurejelewa.

Kuna utata kati ya sheria za uchaguzi, katiba na vile mahakama ilivyofafanua sheria hizo.

Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.

Kumeshuhudiwa maandamano ya wafuasi wa upinzani wanaopinga uchaguzi huo wa marudio na wanashinikiza maguezi ndani ya tume ya uchaguzi IEBC na pia katika mfumo wenyewe wa uchaguzi.

KIM JONG-UN ATEMBELEA KIWANDA CHA BIDHAA ZA UREMBO PYONGYANG

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametembelea kiwanda ya bidhaa za urembo mjini Pyongyan akiandamana na mke wake Ri Sol-ju na dada yake Kim Yo-jing.

Vyombo vya habari vilichapisha picha za ziara hiyo siku ya Jumapili.

Kuoneka hadharani kwa Kim Yo-jong, kunakuja muda mfupi baada ya kupandishwa cheo ndani serikali ya Korea Kaskazini.

Bidhaa za urembo kutoka nchi za kigeni zimekuwa adimu nchini Korea Kaskani kutokana na vikwazo.

Korea Kaskazini inaonekana kujenga sekta yake ya bidhaa za urembo ambapo bidhaa kama Bomhyanggi na Unhasu vimepata umaarufu.

Licha ya umaarufu wake wa kupigwa picha akiwa katika vituo vya kijeshi na maeneo ya kufanyia majiribio makombora, ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za urembo ni moja ya propaganda ya kuhalalisha utawake wake kwa watu wa Korea Kaskazini.

SENETA WA REPUBLICAN AACHIA NGAZI MAREKANI

Seneta wa Chama cha Republican nchini Marekani, Jeff Flake, amesema hatogombea nafasi yake katika uchaguzi wa mwaka 2018.

Amesema nafasi yake inaweza isiwepo katika chama hicho.

Katika hotuba kali inayokosoa utawala wa rais Trump, seneta huyo wa jimbo la Arizona amesema katu hatoacha kusema.

Ameongeza kusema kuwa siasa za Marekani zimekuwa za kutojali, na tabia ya kujishusha hadhi kutoka ikulu ya Marekani.

Lakini amesema, desturi ya kudharau maadili ya demokrasia na misingi yake katu isionekane kama jambo la kawaida.

Mwanzoni, rais Trump alilaumiwa na seneta mwengine wa Republican, Bob Corker, ambae alimweleza rais huyo kama rais ambae sio mwaminifu.

Msemaji kutoka ikulu ya White House Sarah Sanders amesema "huenda ni hatua nzuri" Bwana Flake anajiuzulu, akiashiria kwamba hatoshinda kuchaguliwa tena.

IRAN YAMPIGA KIFUNGO DAKTARI MKAAZI WA SWEDEN KWA UJASUSI

Mahakama nchini Iran inaaminika kumhukumu kifo daktari mmoja mzaliwa wa Iran aliye na kibali cha kuishi nchini Sweden wakimtuhumu kwa kuifanyia ujasusi Israel.

Mkuu wa mashtaka nchini Iran alisema mtu alipatikana na hatia ya kuwapasha habari majasusi wa Israel anuani 30 za wanasayansi wa nyuklia, wawili kati yao waliouawa kwenye mashambulizi ya mabomu mwaka 2010.

Lakini mke wake daktari Ahmadreza Djalali, alisema kwa mume wake alikuwa amekuhukumiwa kwa mashtaka sawa na hayo.

Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnety International, lilisema kwa hukumu hiyo ilitolewa baada ya mateso ya kisaikolojia na hukumu isiyo ya haki.

Mkuu wa mashtaka huko Tehran Abbs Jafari-Dowlatabadi, aliuambia mkutano wa maafisa wa mahakama kuwa mtu ambaye hakutajwa jina aliwapa majasusi wa Isreal anuani za watu 30 muhimu.

Alisema kuwa anuani hizo ni za wanasayansi wa nyuklia Massoud Ali-Mohammadi na Majid Shahriari, ambao waliuawa kwenye milipuko ya mabomu mjini Tehran mwezi Januari na Novemba mwaka 2010.

Mkuu wa mashtaka alisema kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa hizo kwa Israel ili alipwe pesa na msaada wa kupata kibali cha kuwa mkaazi wa Sweden.

Amnesty international ilisema kuwa Bw. Djalali ambaye ni daktari na muathiri kwenye taasisi ya Karolinska mjini Stockholm, alikuwa kwenye ziara ya kibishara nchini Iran mwezi Aprili mwaka 2016, wakati alikamatwa na maafisa wa ujasusi na kuzuiliwa bila ya kuruhusiwa kukutana na wakili kwa muda wa miezi saba.

Bw. Djalali anasema kuwa wakati akiwa kuzuizini alilazimishwa mara mbili kukiri mbele ya kamera kwa kusoma taarifa zilizokuwa zimeandikwa na wale waliokuwa wakimhoji.

Anasema alikuwa chini ya shinikizo kali kupitia mateso ya kisaskolojia na vitisho vya kumuua na kuwakamata watoto wake ili aweze kukiri kuifanyia ujasusi serikali ya Israel.

TRUMP: ASEMA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI NI KUPOTEZA MUDA TU

Rais wa Marekani Donald Trump amemuambia waziri wake wa mashauri ya nchi za nje kuwa anatupa muda wake akijaribu kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Rex alifichua hayo siku ya Jumamosi akisema kuwa Korea Kaskazini haitili maanani mazungumzo hayo.

Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye majibizano makali miezi ya hivi karibuni.

Marekani inataka Korea Kaskazini kusitisha mipango yake ya silaha baada ya kufanya majaribio kadha ya makombora ya na kudai kufanya jaribo la bomu la haidrojeni ambalo linaweza kutundikwa kwa kombora la masafa marefu.

Hi sio mara ya kwanza Donald Trump amekinzana na maafisa wa vyeo vya juu kwenye utawala wake.

Mwezi Agosti alisema kuwa jeshi la Marenia lilikuwa tayari kukabiliana na Korea Kaskazini, saa chache baada ya waziri wake wa ulinzi kujaribu kutuliza misukosuko akisema kuwa jitihada za mazungumzo zilikuwa zinafanikiwa.

Matamshi yake yanakuja siku moja bada ya Bw Tillerson kufichua kuwa maafisa wa Marekani walikuwa na mawasiliano na Korea Kaskazini licha na kuwepo vita vya maneno kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

WALIOCHELEWESHA MAENDELEO MORCCO WAPIGWA KALAMU

Mfalme wa Morocco Mohammed amewafuta kazi mawaziri wake wa elimu, makaazi na afya kwa kuchelewesha maendeleo ya kiuchumi katika jimbo la Rif lililopo kaskazini.

Eneo hilo lilishuhudia maandamano mwaka jana ambayo yalisababishwa na kifo cha muuza samaki katika makabiliano na polisi - tukio ambalo liliashiria matumizi ya nguvu kupitiliza, rushwa na hali ya kutojali.

Mwezi July, Mfalme Mohammed aliwasamehe watu ambao awali walikamatwa wakati maandamano hayo yakiendelea, huku akiwalaumu maafisa wa serikali kushindwa kupeleka miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif.

Eneo hilo lilikuwa kati kati ya vuguvugu ya kisiasa ya mwaka 2011 ambayo ilichochea maandamano nchini Morocco.

KIFO CHA KIM JONG-NAM: WANAWAKE WAKANA KUHUSIKA

Wanawake wawili wamekana mashtaka ya kumuua Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, wakati wa kuanza kwa kesi yao nchini Malaysia.

Bwana Kim alifariki mwezi Februari kwenye uwanja wa Kuala Lumpur, katika kisa cha kusikitisha kilicho ishangaza dunia.

Mwaname raia wa Vienam Doan Thi Huong, 29 na mwingine raia wa Indonesia Siti Aisyah, 25, wanalaumiwa kwa kumwekea kemikali hatari ya VX usoni, alipokuwa akisubiri kuabiri ndege kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.

Lakini wanawak hao wamedai kuwa maajenti wa Korea Kaskazini waliwahadaa kufanya hivyo.

Pyongyang imekana kuhusika kwa vyovyote vile kwenye mauaji hayo

Wanawake hao walikuwa wamefungwa mikono na kuvaa mavazi yasiyopenya risasi, kwa mujibu wa shirika la AFP

Ikiwa watapatikana na hatia wanawake hao watahukumiwa kifo. Mawakili wao wanasema kuwa washukiwa wakuu wameondoka nchini Malaysia.

Kisa hicho kilisababisha mzozo wa kidiplomasia na kuharibika kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Malaysia ambapo kila nchi iliwatimua mabalozi wa nchi nyingine.

Page 7 of 104