blog category

WATU WENGI WAUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA AUSTRALIA

Watu nchini Australia wamepiga kura kwa wingi katika hatua ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja kwenye kura hiyo ya kihistoria.

Kura ilionyesha kuwa asilimia 61.6 ya watu walipiga kura kuruhuru wapenzi wa jinsi moja kufunga ndoa.

Wanaounga mkono ndoa za jinsia moja wamekuwa wakisherehekea maeneo ya umma wakiimba na kucheza,

Waziri mkuu Malcolm Turnbul alisema serikali yake kwa sasa itaruhusu kupitishwa sheria hizo bungeni ifikapo krismasi.

Matokeo hayo ya Jumatano yanafikisha kikomo iliyokuwa wakati mmoja kampeni kali.

Kura hiyo yenyewe imekosolewa na wale wanaounga mkono ndo za jinsia moja wengine wakisema kuwa haikuhitajika wakati bunge lilikuwa na uwezo wa kuijadili moja kwa moja.

Wati walikuwa wanashiriki kwa hiari kinyume na uchaguzi ambao ni wa lazima nchini Australia.

Zaidi ya watu milioni 12.7 karibu asilimia 79.5 ambai ni wapiga kura walishiriki katika zoezi hilo la majuma 8 ambapo swali moja tu liliulizwa, "sheria ya ndoa inaweza kubadilishwa kuruhusu wapenzi wa jinsia moja kufunga ndo?"

KIONGOZI WA CATALONIA ALIYEFUTWA ATIMKIA UBELGIJI"

Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema.

Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi.

Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku.

Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa.

Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita.

Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.

Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba.

Serikali ya Ctalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya wapiga kura walishiriki huku asilimia 90 ya wapiga kura hao wakiunga mkono uhuru

Siku ya Ijumaa bunge la Catalonia likatangaza uhuru.

Kisha waziri mku wa Uhispania akatangaza kuvunjwa kwa bunge la eneo hilo na kuondole kwa Bw. Puigdemont kama kiongozi wa Catalonia.

MKUFU WA ALMASI WAUZWA DOLA MILIONI 33.7 MJINI GENEVA

Mkufu wa almasi kwa karati 163 ambao ni mkubwa zaidi wa aina yake kuuzwa, sasa umeuzwa kwa dola milioni 33.7 katika mnada huko Geneva.

Mkufuku huo ulichongwa kutoka kwa almasi ya karati 404 iliyopatikana nchini Angola.

Mkufu uliokamilika ulitengenezwa kutoka kwa dhahabu nyeupe, almasi na mawe ya thamani.

Uliuzwa katika hoteli ya Four Seasons mjini Geneva baada kuwekwa kwenye maonyesho huko Hong Kong, London, Dubai na New York.

Bei ya mkufu ilikuwa ya juu kuliko ile iliyotarajiwa ya dola milioni 30.

Aliyeununua mkufu huo hajatajwa.

URAIS KENYA TANGAZWA BINGWA NA KURA 7.5M

Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96. Bw Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo hiyo ni asilimia 38.84. ya walio jiandikisha nchini humo.

Rais Kenyatta, akihutubia mara baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura.

Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe.

"Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu," amesema.

Bw Odinga alikuwa ametarajiwa kutangaza mwelekeo kwa wafuasi wake baada ya tangazo la matokeo kufanywa na Bw Chebukati.

Taarifa zinasema ameamua kufanya hivyo hapo kesho.

Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati Mgombea Chama Kura Asilimia Uhuru Kenyatta Jubilee 7,483,895 98.28 Raila Odinga (Alisusia) ODM 73,228 0.96 Mohamed Abduba Dida ARK 14,107 0.19 Japheth Kavinga Kaluyu Mgombea wa kujitegemea 8,261 0.11 Michael Wainaina Mwaura Mgombea wa kujitegemea 6,007 0.08 Joseph Nthiga Nyagah Mgombea wa kujitegemea 5,554 0.07 John Ekuru Aukot Thirdway Alliance 21,333 0.28 Cyrus Jirongo UDP 3,832 0.05

Bw Chebukati amesema anaamini uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Mwenyekiti huyo amesema mambo aliyosema yalihitajika kufanyika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki yalitimizwa. Amesema walitaka kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa.

"Hata tulibadilisha tarehe kutoka 17 hadi 26 Oktoba kuhakikisha tuna muda wa kutosha," amesema.

Kadhalika, amesema alikuwa na kundi la kusimamia mradi wa uchaguzi wa urais kuondoa majukumu kutoka kwa makamishna ambao walituhumiwa na baadhi ya wadau.

"Naweza kusema kwa uhakika, kwamba 26 Oktoba kabla ya uchaguzi kuanza, nilikuwa nimeridhika kwamba tulikuwa tumefanya kila kitu kuhakikisha kila Mkenya angetekeleza haki yake kikatiba," amesema.

"Na haki hii mtu anafaa kuitekeleza bila kutishiwa au kuzuiwa."

Bw Chebukati anasema alishangaa kwamba watu waliotafuta wa kushambulia walimwendea yeye.

Hata hivyo, anasema ndani ya tume nao walimwogopa.

"Hatutaweza kufurahisa kila mtu. Nimedumisha na kuheshimu sheria, kama mwanasheria ziwezi kuvunja sheria niliyojitolea kuilinda," amesema.

Matokeo yalivyokuwa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu Mgombea Chama Kura Asilimia Uhuru Kenyatta Jubilee 8,203,290 54.27 Raila Odinga ODM 6,762,224 44.74 Mohamed Abduba Dida ARK 38,093 0.25 Japheth Kavinga Kaluyu Mgombea wa kujitegemea 16,482 0.08 Michael Wainaina Mwaura Mgombea wa kujitegemea 13,257 0.09 Joseph Nthiga Nyagah Mgombea wa kujitegemea 42,259 0.28 John Ekuru Aukot Thirdway Alliance 27,311 0.18 Cyrus Jirongo UDP 11,705 0.08

MIILI 9 ILIYOKATWAKATWA TOKYO JAPAN

Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamume mmoja baada ya kupata viungo vya miili tisa katika nyumba yake iliyo Zama huko Tokyo.

Polisi walipata vichwa viwili kwenye jokovu nje ya nyumba ya mshukiwa kwa jina Takahiro shiraishi, wakati wakichunguza kutoweka kwa mwanamke mmoja.

Pia walipata viungo vya watu saba kwenye majokovu yaliyo ndani ya nyumba yake.

Mtu huyo wa umri wa miaka 27 anashtakiwa kuwa ndiye alitupa miili hiyo.

Polisi walikuwa wamepata miili ya wanawake 8 na mwanamume mmoja, mingine tayari ikiwa imeanza kuoza.

Jirani wake alisema kuwa alikuwa ameanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake tangu Bw. Shiraishi ahamie nyumba hiyo mwezi Agosti.

Polisi walifanya ugunduzi huo walipokuwa wakimtafuta mwanamke wa umri wa miaka 23 ambaye amekuwa hajulikani aliko tangu tare 21 mwezi Oktoba.

Wachunguzi waligundua kuwa Bw. Shiraishi amekuwa akiwasiliana na mwanamke huyo baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anataka kujiua.

ALIYEKUWA KIONGOZI WA CATALONIA ATANGAZA NIA

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uhispania, amesisitiza msimamo wa serikali yake, kuwa kiongozi wa Catalonia ambaye alifutrwa anaweza kuwania tena uchaguzi wa Disemmba ikiwa hatakuwa gerezani.

Alfonso Dastis alizunguamza wakati wa mkutana wa kuunga mkono umoja wa Uhispania ambao ulifanyika katika mji mkubwa zaidi huko Catalonia wa Barcelona.

Carles Puigdemont aliondolewa ofisini baada ya Madrid kulivua eneo la Catalonia usimamizi wake baada ya eneo hilo kutangaza uhuru.

Serikali kuu ya Uhispania kwa sasa imechukua udhibiti kwa idara za Catalonia

Mkuu wa mashtaka nchini Uhispania anaandaa kumfungulia mashtaka Bw. Puigdemont na maafisa wengine wa Catalonia kwa kukiuka sheria ya Uhispania.

Bw. Puigdemont anasema hatambui amri ya kutoka Madrid ambayo ilimundoa madarakani.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nadani nchini Uhispania amewaandikia polisi wote huko Catalonia akiwataka kuonyesha uzalendo kwa awamu mpya ya uongozi.

Aliwashauri polis wote ambao sasa wako chini ya udhibiti kutoka Madrid kuhusu wajibu wao wa kufuata maagizo.

MTU ALIYEPANGA KUMUUA RAIS VLADIMIR PUTIN AJERUHIWA UKRAIN

Mwamamue moja kutoka Chechenia ambaye analaumiwa kwa kupanga kumuua rais wa Urusi Vladimir Putin amejeruhiwa na mke wake kuuliwa wakati wa shambulizi karibu na mji mkuu wa Ukrain Kiev.

Adam Osmayev alijeruhiwa lakini anaweza kuishi baada ya gari alilokuwa akilitumia kumiminiwa risasi kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya ukrain.

Wizara hiyo ilisema kuwa mke wake Osmaye, Amina Okuyev aliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji cha Hlevaha.

Mwaka 2012 maafisa nchini Urusi walisema kuwa Bw. Osmayev alikuwa sehemu ya njama ya wanamgambo kumuua Bwa Putin.

Vyombo vya habari vya Urusi viliripoti wakati huo kuwa watu walipanga kutega mabamu kwenye barabara ya Kutuzovsky mjini Moscow, inayotumiwa na Bw Putin kila siku.

Urusi baadaye iliitaka Ukrain kumsalimisha Bw. Osmayev lakini mamlaka nchini Urusi zikakataa kufanya hivyo, zikisema kuwa zilitaka kungoja hadi mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya kuamua kuhusu ombi lake la kupinga kusalimishwa kwa Urusi.

Mwezi Juni alinusurika jaribio la kumuua mjini Kiev. Mshambuliaji kisha akapigwa risasi na kujeruhiwa na Bi Okuyeva.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika kwenye shambulizi la siku ya Jumatatu.

Hii inakuja chini ya wiki moja baada ya mbunge wa Ukrain kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu kwenye mji mkuu Kiev.

Mlinzi wa Ihor Mosiychuk na mtu mwingine waliuawa wakati wa mlipuko huo.

Bi Okuyeva wakati moja alifanya kazi kama mshauri wake.

IS WAKAMATWA UTURUKI

Polisi nchini Uturuki imewakamata mamia ya watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kikundi cha wanamgambo wa IS.

Raia wawili wa Azerbaijan na wengine 28 wa Syria, ni miongoni mwa waliokamatwa katika mji wa Mashariki wa Erzurum na mji wa Bursa uliopo Kaskazini Magharibi.

Wengine walikamatwa katika mji mkuu Ankara siku ya Jumamosi.

Mpiganaji wa IS aliwaua watu 39 katika ukumbu mmoja wa usiku uitwao Reina mjini Istanbul, na tukio hilo bado limeacha simanzi kubwa.

Page 6 of 104