blog category

53 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA MAKOMBORA YA URUSI

Takriban raia 53 wameuawa katika shambulio la kombora la Urusi katika kijiji kilichopo mashariki mwa Syria Al-Shafah, kundi la uangalizi linasema.

Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu Syria lililo na makao yake Uingereza (SOHR) linasema 21 kati ya wanaoripotiwa kuuawa Jumapili ni watoto.

Kijiji hicho kipo Deir al-Zour, mojawapo ya majimbo ya mwisho ambako wangambo wa Islamic State wanendelea kudhibiti ardhi.

Awali SOHR lilisema watu 34 wameuawa katika makombora yaliolenga makaazi ya watu .

Lakini mkuu wa shirika hilo limeliambia shirika la habari la AFP kwamba sasa wanaamini idadi hiyo ipo juu zaidi.

Awali Urusi ilithibitisha kwamba walipuaji wasita wa mabomu ya masafa marefu walitekeleza mashambulio ya angani katika eneo hilo, lakini ikasema iliwalenga wanamgambo na ngome zao.

Urusi ni mshirika wa kariu wa rais wa Syria Bashar al-Assad katika vita vya muda mrefu vya kiraia nchini humo.

Mazungumzo ya amani yanayoungwamkono na Umoja wamataifa yanatarajiwa kuanza upya Geneva wiki ijayo, lakini awamu kadhaa za mazungumzo hayakufuwa dafu.

POLISI WAVAMIA WAHAMIAJI PAPUA NEW GUINEA

Polisi wa Papua New Guinea (PNG) wameingia katika kituo cha mahabusu cha wahamiaji kilichokuwa kinamilikiwa na Australian kwa azma ya kuwaondosha wanaoomba uhamiaji waliosalia, imethibitisha serikali ya Australia.

Mamia ya wanaume wamekataa kuondoka kwenye kituo hicho kilichopo katika kisiwa cha Manustangu kilipofungwa tarehe 31 Oktoba, wakielezea hofu ya usalama wao.

Alhamisi, wanaume waliokuwa katika kituo hicho walisema polisi wa PNG walikuwa wamewapatia saa moja wawe wameondoka.

Australia imesema kuwa operesheni hiyo inaendeshwa na Papua New Guine- PNG.

Chini ya sera tata, Australia iliwashikilia watu wanaoomba uhamiaji wanaowasili kwa boti kwenye kambi katika visiwa cha Manus na Nauru, ambalo ni taifa dogo leneo la Pacific.

Australia ilifunga kituo hicho cha kisiwa cha Manus baada ya mahakama ya PNG kuamua kuwa kilikuwa ni kinyume cha sheria, na kuwataka wanaoomba uhamiaji kuhamia kwenye vituo vingine vya wanaoomba uhamiaji vilivyopo kwenye maeneo mengine ya kisiwa hicho.

Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull alisema kuwa taifa lake ''halitashinikizwa " kuwakubali wanaume hao wahamiaji, akirejelea kuwa sera ya muda mrefu ya kuwashikilia itachochea biashara haramu ya binadamu.

Mmoja wa wakimbizi hao, Abdul Aziz Adam, alisema kwua watu wapatao 420 wanaoomba uhamiaji walibakia kwenye kituo hicho Alhamis Thursday, na walikuwa watulivu.

Watu hao walikataa kuondoka kwasababu wanahofia kuwa wanaweza kushambuliwa na jamii za watu waishio kwenye kisiwa hicho.

Makundi ya kutete haki za binadamu yansema wahamiaji hao wamewahi kushambuliwa awali.

JESHI LA PAKISTAN LASEMA LIKO TAYARI KUSAIDIA KUKOMESHA MAANDAMANO ISLAMABAD

Jeshi la Pakistan linasema liko tayari kuisaidia serikali kuwatawanya waandamanaji wenye itikadi kali za kiislamu walioifunga barabara kuu wa Islamabad.

Serikali ililiomba jeshi liisaidie kurudisha utulivu baada ya polisi kushindwa kuwatawanya waandamanaji Jumamosi.

Hatahivyo taarifa ya jeshi inaonekana kuishutumu serikali kwa namna ilivyoshughulikia hali, ikieleza kuwa maafisa wa polisi hawakutumiwa vizuri.

Inaaminika kuwa takriban watu 6 wameuawa na Wengine takriban 200 wamejeruhiwa.

Jeshi limeomba ufafanuzi zaidi kabla ya kuagiza kutumwa kwa wanajeshi.

Waandamanaji wamefunga barabara kwa wiki kadhaa wakitaka waziri wa sheria Zahid Hamid, afutwe kwa kazi kwa makosa ya kukufuru.

Maandamano yamesambaa hadi katika miji mingine ukiwemo Lahore na bandari ya kusini Karachi.

Siku ya Jumamosi, serikali ilifunga kwa muda vituo vya kibinfasi vya habari na kufunga baadhi ya mitandao ya kijamii ukiwemo Facebook, Twitter na Instagram - kutokana na wasiwasi kwamba matangazo ya moja kwa moja ya hatua ya polisi huenda yakachochea hisia kali za kidini.

Waandamanaji wamefunga barabara kwa wiki kadhaa wakitaka waziri wa sheria Zahid Hamid, afutwe kwa kazi kwa makosa ya kukufuru.

Maandamano yamesambaa hadi katika miji mingine ukiwemo Lahore na bandari ya kusini Karachi.

MLADIC APEWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA MAUAJI YA KIMBARI BOSNIA

Kamanda wa zamani wa jeshi la Boznia Jenerali Ratko Mladich amehukumiwa maisha jela na Mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu wa kivita-ICC.

Mladich alipatikana na hatia ya kutekeleza mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita pamoja na dhulma dhidi ya binadamu katika iliyokuwa utawala wa Yugoslavia.

Hukumu imepokelewa kwa hisia tofauti.

Kundi la wamama wa Srebrenitsa, limesema kuwa limefurahishwa mno na hukumu hiyo.

Lakini mwanamke mmoja Muislamu raia wa Boznia, ambaye wavulana wake wawili na mumewe waliuwawa katika vita hivyo, ameiambia bbc kuwa Bwana Mladich anastahili hukumu kubwa na kali zaidi.

HOFU YAONGEZEKA KWA MLIMA WA VOLKANO KULIPUKA

Takriban watu laki moja karibu na mlima Agung kisiwani Bali wametakiwa kuhama wakati maafisa wanahofia mlima huo wa volkano kulipuka pakubwa.

Maafisa Indonesia wameongeza kiwango cha hatari na kupanua zaidi eneo linalokaribiana na mlima huo wa vokano unoendelea kuchemka linalotarajiwa kuathirika.

Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa.

Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3400 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.

Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.

Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama eneo hilo na kwenda kwingine.

Mlima huo wa volkano ulionekana ukitoa moshi na sauti za milipuko zilisikika kwa umbali wa kilomita 12 kutoka juu ya mlima huo.

Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.

UFARANSA YATAKA LIBYA KUJADILIWA NA UN

Ufaransa imetoa wito wa kufanyika mkutano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili vitendo vibaya wanavyofanyiwa Wahamiaji nchini Libya.

Hatua hiyo imekuja baada ya taarifa kutoka nchini Libya kusema kuwa Wahamiaji wa Kiafrika wamekuwa wakiuzwa kama watumwa.

Baada ya mkutano wake na Kiongozi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekuelezea kuuzwa huko kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na kuongeza kuwa hatua zaidi zinahitajika kuchukuliwa kuvunja mtandao wa watu wanaohusika na biashara haramu ya binadamu.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuwekwa iwapo mamlaka za Libya hazitachukua hatua, kupiga marufuku vitendo hivyo.

MNANGAGWA AKUTANA NA RAIS JACOB ZUMA AFRIKA KUSINI

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekutana na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati ambapo anasubiriwa kurudi nyumbani jana.

Bwana Zuma alitarajiwa kuwasili atika mji mkuu wa Harare leo ili kuwa mpatanishi wa mgogoro uliokuwa ukiendelea lakini akafutilia mbali zaiara hiyo baada ya rais Mugabe kujiuzulu.

China imesema kuwa imeheshimu uamuzi wa rais Robert Mugabe wa kujiuzulu na kwamba bado atasalia kuwa rafiki wa raia wa Uchina.

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni Lu Kang ameongezea kuwa sera za China kwa Zimbabwe hazitabadilika. Uhusiano wa China na Zimbabwe ni mkubwa tangu vita vya Rodesian vya msituni.

Bwana Mugabe alikosa kuungwa mkono na Usovieti hivyobasi akarudi China ambayo iliwapatia wapiganaji wake wa Gorila vifaa pamoja na mazoezi.

Mataifa yote mawili yaliimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia wakati wa uhuru wa Zimbabwe 1980 na rais Mugabe alimtembelea waziri mkuu wa China mwaka uliofuata.

JESHI LA ZIMBABWE LATOA UFAFANUZI JUU YA KAULI YA MKUU WA MAJESHI

Jeshi la Zimbabwe limesoma taarifa kwenye kituo cha runinga cha serikali ZBC, likisema kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu.

Hata hivyo limesema kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi na Rais Mugabe yuko salama.

Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Harare mapema leo.

Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaa baada ya jeshi kudhibiti kituo cha ZBC.

Mwanamume mmoja ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi alisema kuwa jeshi linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe 93, na familia yake wako salama.

Page 5 of 104