blog category

TRUMP AMSHAMBULIA MSAIDIZI WAKE WA ZAMANI STEVE BANNON

Rais Donald Trump amemshambulia msaidizi wake wa zamani wa Ikulu ya White house Steve Bannon,kwamba alipoteza akili zake mara tu alipopoteza ajira yake.

Trump amefikia hatua hiyo kufuatia Bannon kunukuliwa na kitabu kipya kilichopishwa akiwa anaelezea jinsi mtoto wa rais Trump alivyokutana kwa siri na kundi la watu kutoka Urusi ili kupanga njama za uchaguzi.

Ndani ya kitabu hicho kilichoandikwa na mwandishi wa habari Michael Wolff,afisa huyo wa zamani wa ikulu ya Marekani,ameelezea namna ambavyo Donald Trump mtoto,mwanaye rais Trump alivyopewa taarifa na Urusi zilizolenga kummaliza kisiasa Bi Hillary Clinton ili yeye aweze kushinda.

Hata hivyo kutokana na shutuma hizo ndani ya kitabu hicho zilizopewa uzito na afisa huyo wa zamani wa ikulu ya white house,rais Donald Trump amesema kuwa lolote la kuweza kumuathiri yeye binafsi na urais wake pia,bali amesisitiza kuwa amegundua kuwa ofisa huyo hakupoteza kazi yake tu lakini alipoteza akili zake pia.

Amesema pia kuwa Steve anafanyayote hayo kwa maslahi binafsi,akifikiri kuwa suala la ushindi si rahisi kama ilivyokuwa katika ushindi wangu,hana lolote la kuweza kufanya kuhusiana na historia ya ushindi wetu ambao ulipatikana kwa kura za wanawake na wanaume waliokuwa wamesahaulika.

Steve Bannon, ni afisa wa zamani wa rais Trump nayetajwa kuwa mtu muhimu na alibuni kauli mbiu ya rais Trump Marekani kwanza yaani America first kabla kuacha kazi mwezi August mwaka jana.

APPLE YAREKEBISHA TATIZO KUBWA LA 'NENO LA SIRI'

Kampuni ya Apple imesema kuwa inarekebisha tatizo kubwa katika mfumo wake wa operesheni wa Mac.

Tatizo hilo katika toleo lake jipya la MacOS High Sierra,l inaruhusu mtu yeyote kuingia katika mashine hiyo bila kutumia neno la siri na kupata haki zote za mtumizi wa mashine hiyo.

''Tunarekebisha programu ili kuliangazia swala hilo'', Apple ilisema katika taarifa.

Tatizo hilo lilifichuliwa na mtaalam wa maswala ya usalama wa mitandaoni nchini Uturuki Lemi Ergin.

Hata hivyo bwana Ergin alikosolewa kwa kutofuata maelezo ya ufichuzi huo yanayofuatwa na wataalam wengine wa usalama wa mitandao.

Maelezo hayo yanawahitaji wataalam wa usalama wa mitandaoni kuelezea kampuni kuhusu mapungufu katika bidhaa zao hivyobasi kuwapatia muda wa kutosha kurekebisha tatizo hilo kabla ya kutangaza kwa umma.

ETHIOPIA KUWAACHILIA HURU WAFUNGWA WA KISIASA

Waziri Mkuu wa Ethiopia ametangaza kuwa wafungwa wote wa kisiasa ambao wamekuwa wakizuiliwa korokoroni nchini humo wataachiliwa huru.

Aidha, amesema kituo hatari cha kuwazuilia wafungwa wa kisiasa ambacho kimekuwa kikitumiwa kuwatesa watuhumiwa pia kitafungwa.

Hailemariam Desalegn amesema kwenye kikao na wanahabari kwamba mashtaka yote dhidi ya wale ambao kesi zao bado hazijamalizika yatafutiliwa mbali.

Ethiopia kwa muda mrefu imetuhumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu kwa kuwakamata wapinzani wake kwa wingi na kuwazuilia katika juhudi za kuzima upinzani dhidi ya serikali.

Hata hivyo, hii ndiyo mara ya kwanza kwa serikali kukiri kwamba inawazuilia wafungwa wa kisiasa.

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limekuwa likiituhumu serikali kwa kutumia sheria za kukabiliana na ugaidi kuwafunga wapinzani wake.

Shirika la Amnesty International limesema hatua ya leo huenda ikaachilia sura mpya kwa haki za kibinadamu Ethiopia.

Wanaozuiliwa katika magereza na vituo mbalimbali kote nchini humo ni pamoja na wanaharakati wa upinzani kutoka majimbo ya Amhara na Oromia.

Majimbo hayo yalishuhudia maandamano ya kupinga serikali 2015 na 2016.

Kuna piawatu kutoka jimbo la watu wa mataifa ya kusini, na wanahabari ambao wamekuwa wakiikosoa serikali.

Ni vigumu kueleza hasa ni wafungwa wangapi wa kisiasa wanazuiliwa nchini humo, lakini mwandishi wetu anakadiria kwamba kuna takriban watu 1,000 wanaozuiliwa kwa makosa mbalimbali chini ya sheria za kupambana na ugaidi.

Bw Hailemariam amesema kituo kikuu cha kuwazuilia wafungwa cha Maekelawi mjini Addis Ababa ambacho HRW tangu 2013 walidai kimekuwa kikitumia mateso kupata habari kutoka kwa washukiwa kitafungwa.

KOREA KASKAZINI YADAI KUSHAMBULIA ENEO LOLOTE MAREKANI

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo lolote la Marekani.

Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.

Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano.

Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo .

Kitengo cha habari cha taifa hilo kimesema kuwa kombora hilo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53.

Kombora hilo lililofyatuliwa kwa mwinuko halikupitia katika anga ya Japan kama makombora mengine hapo awali na lilianguka kilomita 250 karibu na pwani yake ya kaskazini , kulingana na maafisa wa Japan.

Ripoti hiyo imesema kuwa kama taifa lenye nguvu za kinyuklia na linalopenda amani, Korea Kaskazini itafanya kila iwezalo kutekeleza lengo lake la kuleta amani na udhabiti duniani.

Imesema kuwa, silaha zake za ulinzi dhidi ya sera ya kibepari ya Marekani, hazitatishia taifa lolote duniani iwapo maslahi ya Korea Kaskazini hayatakiukwa.''Hilo ndio tangazo letu''

EQUATORIAL GUINEA YAZIMA JARIBIO LA MAPINDUZI

Mamluki wamejaribu kuipindua serikali ya Equatorial Guinea, kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo.

Takriban wanaume 30 waliojihami kutoka Chad, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya kati walikamatwa mwezi uliopita, kulingana na waziri mmoja.

Walipatikana wakiwa roketi, bunduki na risasi kwenye mpaka nchini Cameroon.

Serikali ya Rais Teodoro Obiang Nguema, imekuwa ikilaumiwa kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.

Wanajeshi nchini Equatorial Guinea walimuua kwa kumpiga risasi mamluki wakati wa makabiliano siku ya Jumatano karibu na mpaka na Cameroon, kwa mujibu wa runinga ya taifa.

Bw. Obiang amekuwa madarakani kwa karibu miaka 40, baada ya kutwaa madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1979 na kumuondoa madarakani mjomba wake Francisco Macias Nguema ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi.

Katika taarfa iliyosomwa kupitia radio ya taifa, waziri wa ulinzi Nicholas Obama Nchama aliwalaumu mamluki waliokuw wamepewa kazi na makundi ya upinzani na kusaidiwa na mataifa ambayo hayakutajwa.

Mwanajeshi huyo wa zamani wa Uingereza na mafanyabiashara alikamatwa nchini Zimbabwe mwaka 2004 na kusafishwa kwenda Equatorial Guinea miaka minne baadaye.

Mwaka 2008 Bw. Mann alihukumiwa miaka 34 jela, lakini mwaka mmoja baadaye aliachuliwa baada ya kusamehewa na Bw. Obiang.

Equatorial Guinea ni moja ya nchi wazalishaji wakubwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu wake wanaishi katika hali ya umaskini.

MWANAMFALME MITEB AACHILIWA HURU

wanamfalme wa Saudia Miteb bin Abdullah ameachiliwa huru zaidi ya wiki tatu baada ya kukamatwa kwa madai ya kuhusika na ufisadi , maafisa wanasema.

Mwanamfalme Miteb ambaye alionekana kuwa miongoni mwa warithi wa ufalme huo aliachiliwa huru baada ya kukubali kutoa faini ya dola bilioni moja.

Ni miongoni mwa wanasiaasa na wafanyibiashara 200 waliokamatwa nchini humo kutokana na vita dhidi ya ufisadi mnamo terehe 4 mwezi Novemba.

Watu wengine watatu pia wameachiliwa huru baada ya kukubali kulipa faini.

Ni kweli mwanamfalme Miteb aliachiliwa huru alfajiri Jumanne na duru zilizopo karibu na serikali zilizoambia chombo cha habari cha AFP.

Miteb ambaye ni binamu wa mwanamfalme Mohammed bin Salman na ambaye aliongoza kitengo cha walinzi wa kulinda ufalme huo ndiye aliyekuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa kisiasa kukamatwa katika vita hivyo dhidi ya ufisadi.

Mwana huyo wa mfalme Abdullah alifutwa kazi muda mfupi kabla ya kuzuiliwa.

Wanawafalme, mawaziri na wafanyibiashara wakuu walikamatwa mwanzoni mwa mwezi huu na kuzuiliwa katika hoteli moja ya kifahari kwa madai ya ufisadi.

URUSI YAPOTEZA MAWASILIANO NA SATELAITI YAKE BAADA YA KUIZINDUA

Urusi imepoteza mawasiliano na satelaiti yake ya hali ya hewa saa chache baada ya kuizindua.

Mawasiliano yamepotea kwa sababu haiko katika mzingo wak , kulingana na shirika la angani la Roscoms.

Uzinduzi huo ulifanyika kutoka eneo la Vostochny cosmodrome mashariki mwa Urusi.

Ni uzinduzi wa pili kutoka kambi hiyo ambayo ilifunguliwa mwaka uliopita.

PAPA AFANYA ZIARA MYANMAR INAYOTUHUMIWA KWA MAUAJI YA WAISLAMU WA ROHINGYA

Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya.

Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar.

Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya.

Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchinihumo.

Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila'.

Zaidi ya WaRohingya 600,000 wamekimbilia mpakani - na wakimbizi wakielezea kukabiliwa na mauaji, ubakaji na kuteketezwa moto kwa vijiji - jeshi imekana tuhuma zote.

Papa atakutana na kiongozi wa Myanmarr - Aung Sun Suu Kyi - Jumanne - huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka yake minne kama kiongozi wa kanisa katoliki.

Page 4 of 104