blog category

AJALI YA NDEGE IRAN WATU WOTE 66 WAANGAMIA

Watu 66 wameuawa kwenye ajali ya ndege ya abiria nchini Iraan, maafisa wa kampuni wamesema.

Ndege hiyo ya shirika la Aseman, ilikuwa safarini kutoka mjini Tehran kwenda mji wa kusini magharibi wa Yasuf wakati ilianguka kwenye milima ya Zagros kati kati mwa Iran.

Shirika la msalaba mwekundu lilituma kikisi cha uokoaji kweda eneo hilo karibu na mji wa Semirom mkoa wa Isfahan.

Ndege hiyo namba 3704 iliondoka Tehran mwendo wa saa (01:30 GMT) na kutoweka kutoka kwa rada baadaye.

Maafisa wanasema kuwa hali mbaya ya hewa imetatiza jitihada za uokoaji.

Ndege hiyo inaaminiwa kuwa ya miaka 20 iliyotengenezewa nchini Ufaransa.

Ripoti zinasema kuwa wale waliokuwa ndani ya ndege ni abiria 60, walinzi wawili, wahudumu wawili, rubani na msaidizi wake.

SENETI MAREKANI LAIDHINISHA MATUMIZI YA SHUGHULI ZA SERIKALI

Bunge la Seneti nchini Marekani limeidhinisha matumizi ya muda kufadhili shughuli za serikali katika kumaliza mjadala uliozua sitofahamu kwa siku tatu.

Muswada huo, ulioidhinishwa na idadi kubwa ya maseneta, utasaidia kufadhili huduma za serikali kwa wiki nyingine mbili na nusu.

Muswada huo pia umepelekwa baraza la wawakilishi na baadaye kusainiwa na Rais Trump.

Wawakilishi wa chama cha Democratic walisema kuwa wataunga mkono muswada huo kama utatoa hatma ya maelfu ya wahamiaji waliongia marekani wakiwa watoto ambapo sasa wanakabiliwa na kurudishwa sehemu walizotoka.

Hadi sasa wahamiaji hao wanalindwa na mpango wa kuwasadia watu walioingia Marekani wakiwa watoto DACA.

Akizungumza baada ya kura hizo za seneti, kiongozi wa chama cha Republic Mitch McConnell amezitaka pande zote mbili kufikia makubaliano yenye tija.

WAFUNGWA WACHUKUA UDHIBITI WA GEREZA MJINI RIO DE JANEIRO, BRAZIL

Wafungwa wamechukua udhibiti wa gereza kwenye mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil na wanawashika mateka baadhi ya wafanyakazi wa gereza hilo.

Polisi waliojihami wanalizunguka gereza hilo lenye msongamano wa wafungwa la Japari ambalo liko chini ya udhibiti wa genge moja la wahalifu lenye guvu nyingi mjini humo.

Wafungwa watatu ambao walihusika katika kulidhibiti gereza hilo wamepigwa risasi lakini hawajapa majeraha ya kuwatishia maisha.

Ghasia hizo zinatokea siku mbili baada ya Rais wa Brazil Michel Temer, kusaini sheria ya kuwapa wanajeshi ruhusa ya kusimamia usalama wa mji wa Rio de Janeiro.

Maafisa wa gereza wanasema ghasia hizo huenda zimechangiwa na hatua mpya za ulinzi.

GEORGE WEAH AAHIDI KUTIMIZA MATARAJIO

Nyota wa zamani wa kandanda duniani George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.

Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.

Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.

Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."

Kiongozi huyo ametumia hotuba yake kusifu uhusiano wa karibu kati ya taifa hilo na Marekani na China.

Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.

Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo katika uwanja wa Samuel Doe viungani mwa mji wa Monrovia.

NETANYAHU AISHAMBULIA IRAN AKIITA "CHUI MILIA HATARI"

Waziri mkuu wa Israel ameishambulia vikali Iran akiuambia mkutano wa ulinzi huko Munich kuwa Iranana tisho kubwa kwa dunia yetu.

Benjamin Netanyahu alisema kuwa "Israel haitaruhusu Iran kuiweka kamba ya ugaidi kwenye shingo lake.

Bw Netanyahu alifananisha makubaliano ya Munich ya mwaka 1938 yaliyoonekana kama jitihada zilizofeli za kuifurahisha Ujerumani ya Nazi na makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015.

Alisema kuwa Iran inadanganya kuwa haikutuma ndege isiyo na rubani kwenda Israeli wiki iliyopita ambayo ilidunguliwa na jeshi la Israel.

Akishika kifaa cha kile alichokitaja kuwa mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyodunguliwa, Netanyahu alimwambia moja kwa moja mjumbe wa Iran ambaye ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, akimwambia: "Unatambua hiki, unastahili, ni chenu, msitujaribu."

MWANAMUZIKI HUGH MASEKELA AFARIKI DUNIA

Hugh Masekela, mwanamuziki maarufu wa mtindo wa jazz kutoka Afrika Kusini aliyechangia juhudi za kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo, amefariki dunia akiwa na miaka 78.

Familia ya mwanamuziki huyo mcheza tarumbeta, kupitia taarifa, imesema Masekela amefariki akiwa mjini Johannesburg baada ya kuugua saratani ya tezi dume kwa muda mrefu.

Masekela alipata umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wake wa kipekee wa Afro-Jazz na vibao vilivyokuwa maarufu kama vile Soweto Blues.

Wimbo huo alioutoa 1977 ulihusika sana katika harakati za kupambana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Amekuwa akitambuliwa na wengi kama "baba wa Jazz nchini Afrika Kusini.

Alizaliwa mnamo Aprili tarehe 4 1939. Anasifika kwa ujuzi wake kupuliza tarumbeta na alikuwa ni mojawapo ya wakosoaji wa wazi wa ubaguzi wa rangi.

Alizaliwa katika mtaa uliopo kaskazini mashriki, alianza kuimba na kupiga kinanda akiwa mtoto.

Akiwa na umri wa miaka 14 alianza kupiga tarumbeta baada ya kutizama filamu ya hollywood kumhusu mwanamuziki wa Kimarekani mwa mtindo wa Jazz.

Alikabidhiwa tarumbeta yake ya kwanza na Trevor Huddleston, aliyekuwa askofu baadaye aliye kampeni dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Masekela na baadhi ya wanafunzi wenzake shuleni waliunda bendi iliyojulikana kama Huddleston Jazz Band, bendi ya kwanza ya Okestra ya vijana Afrika kusini.

Mwishoni mwa miaka ya 1950 alikwenda Marekani na kuunda urafiki na Harry Belafonte na akajiunga na shule ya muziki.

DONALD TRUMP AISHUTUMU FBI MAUAJI YA FLORIDA

Rais wa Marekani Donald Trump, ameirushia cheche za maneno shirika la upelelezi nchini humo- FBI, kwa kukosa kupata vidokezi muhimu vya mapema, kuhusiana na shambulio la Jumatano huko Florida, wakati mtu mwenye silaha alipowashambulia wanafunzi wa shule na kuwauwa watu 17.

Amesema kuwa FBI inapoteza muda mwingi kujaribu kubaini kuwa timu yake ya Kampeini ya Urais ilishirikiana na Urusi kuiba kura mwaka 2016 badala ya kutoa uilinzi kwa wamarekani.

Mkutano huo umefanyika nje ya mahakama ya jimbo hilo katika mji wa Fort Lauderdale, kilomita chache kutoka kwenye shule ambayo mwanafunzi wa zamani, Nikolas Cruz, aliwauwa watu 17.

Katika mtandao wake wa Tweeter, Bwana Trump, ameandika kuwa FBI inafaa kuzingatia kazi yake muhimu, huku akiongeza kusema kuwa, ni huzuni kubwa na ni jambo lisilokubalika kwamba, dalili ya uwezekani wa kutokea mashambulizi, haikutambuliwa mapema.

Awali Maelfu ya watu huko Florida, wakiwemo manusura wa kisa hicho cha Jumatano walijumuika pamoja katika mkutano mkubwa, wakitoa wito wa kuwepo kwa sheria ya udhibiti silaha nchini Marekani.

UBAKAJI KATIKA HOSPITAL KENYA, WANAWAKE WAANDAMANA

Makundi ya wanawake kutoka mashirika tofuati nchini Kenya yameandamana ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua kuhusiana na madai kuwa akina mama waliojifungua wamekuwa wakidhulumiwa kingono katika Hospitali kuu ya Taifa, Kenyatta National Hospital.

Maandamano hayo yanafanyika wakati ambapo ripoti ya uchunguzi uliyoagizwa na waziri wa afya nchini humo inatarajiwa kutolewa rasmi.

Waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu aliagiza uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.

Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao siku ya Ijumaa zinadai kina mama waliojifungua wamekuwa wanashambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.

Wanaotuhumiwa ni wahudumu katika vyumba vya maiti, wanaonyooshewa kidole pia kwa kutumia maiti kuwashutua akina mama waliojifungua katika hospitali hiyo.

Page 3 of 104