Wito huo umetolewa na Mratibu wa Mafunzo kutoka Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania Victor Maleko katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuanzia oktoba 9mpaka 13 mwaka huu ya kuandika Haabari za mazingira, yanayo fanyika katika ukumbi wa Hotel ya Nala Senturion ulioko Mjini Dodoma.

Aidha Wito umekuja mara baada ya waandishi wengi nchini kuandika habari za mambo mengi hali inayo pelekea ufanisi wa kazi zao kupungua ikiwa ni kutokana na kuto kuwa mbobezi katika jambo moja.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wametumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa umoja huo kwa kuandaa mafunzo hayo yenye tija kwa waandishi wa habari na wametoa wito kwa washiriki hao kuizingatia elimu wanayo ipata hapo ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mafunzo hayo ya Kuripoti Habari za mazingira yanatolewa kwa waandhishi wa habari wapatao Ishirini na Saba kutoka Tanzania bara na Zanzibar yana lengo la kuleta mabadiliko katika jamii baada ya Waandishi hao kujengewa uelewa kuhusiana na mazingira ili wawasirishe katika jamii kupitia kalamu zao.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh