Changamoto ya ukosefu wa Mitandao Vijijini hapa nchini imetajwa kuwa ndio Sababu kubwa ya kukwamisha kupata Taarifa za maendeleo kwa wakazi wa maeneo hayo na kukwamisha juhudi za Serikali kufikia Tanzania ya Viwanda.

Hayo yamebainishwa mapema hii leo na Walaghabishi wanao patiwa mafunzo ya siku tatu ya namna ya kutumia mitandao ya kijamii ili iwasaidie kupata taarifa za maendeleo katika vijiji vyao, ambapo wamesema kuwa kukosekana kwa mtandao kunasababisha wakose haki zao za msingi.

Miungoni mwa washiriki wa Mafunzo hayo Zena Hamisi Nakoni mkazi wa Kata ya Nanguruwe amesema kuwa Chanangamoto ya Mtandao katika kata yao imekuwa kubwa sana ila sio kigezo cha wakazi hao kukosa kupata taarifa kwani kupata taarifa kwa kutumia mitandao hiyo hiyo inayo suasua.

Aidha ametoa Shukrani kwa MSOAPO na OXFAM kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kuingia katika ulimwengu wa kisasa kwa kupata taarifa za maendeleo kupitia simu zao za mkononi.

Mustafa Kwiyunga ambaye ni Mratibu wa MSOAPO ambao ndio waratibu wa mafunzo hayo ya siku tatu kwa kushirikiana na OXFAM yanayo fanyika katika ukumbi wa Benki kuu tawi la Mtwara, amesema kuwa wameamua kutoa mafunzo hayo kwa walaghabishi Hamsini kutoka katika kata tano ikiwemo Msimbati, Madimba, Nanguruwe, Mayanga na Ziwani, kwa lengo la wananchi hao kupata Taarifa mbalimbali zitakazo saidia katika shughuli za Maendeleo.

Mratibu huyo amesema kuwa mara baada ya mafunzo hayo walaghabishi hao watapatiwa simu za Mkononi ili ziwasadie kuwapatia taarifa za maendeleo katika vijiji vyao. Kwa upande wake Bill Marwa mratibu wa mawasiliano ya kisasa kutoka OXFAM Tanzania amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa mitandao ya kijamii na takwimu mpaka mwezi Januari mwaka huu zinaonesha watu bilioni 3.5 sawa na asilimia hamsini 50 % ulimwenguni wanatumia Mtandao.

Pia amesema kuwa Mitandao ya kijamii imefungua fursa nyingi za maendeleo ulimwenguni na kusaidia watu kunufaika sana ingawa kumekuwa pia na matumizi mabaya ya Mtandao ,ikiwemo propaganda na wizi.

Ikumbukwe kuwa nchini Tanzania mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka 2016 kulikuwa na watumiaji wa mtandao milioni 16.9 zaidi ya asilimia Arobaini ya Watanzania. 2 Attachments

0768671579

Add comment


Security code
Refresh