Wananchi wa ushirika wa Aminika Gold mine co-operative society Ltd wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida wameshauriwa kuacha tabia ya kuwa kama kikundi cha wanywa kahawa na badala yake washikamane pamoja kwa lengo la kuimarisha ushirika wao, uweze kuwa na tija.

Wito huo umetolewa juzi na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Miraji Mtaturu, wakati akifungua mkutano wa uchunguzi bodi ya wakurungezi ushirika wa Aminika.

Alisema ushirika wa Aminika ambao una muunganiko wa vikundi vitano, na wanachama wake ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Singida Halima Kasungu , waandishi wa habari na viongozi mbali mbali serikali.

Akifafanua,alisema kwenye ushirika au kikundi cho chote kuna faida nyingi, ikiwemo ya kuwa na nguvu zaidi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali, pia ni rahisi kukopeshaka , na kupata misaada mbalimbali.

Akisisitiza, alisema Rais Dk. Magufuli ameonyesha dhamira ya wazi kwamba anataka kuwaona wachimbaji wadogo wa madini, wanafaidika na shughuli yao hiyo.

Aidha, DC Mtaturu amewataka wanachama wa Aminika kuacha kulalamika Kuwa maeneo waliyopewa hayana dhahabu, kwa madai kwamba, uwezo wao wa uchimbaji madini, ni mdogo na utaalamu hawana.

Awali katibu wa bodi, Himisi Nkingi, alisema toka wameanza uchimbaji mwaka 2014- 2017, wamezalisha gram 200 ya dhahabu yenye thamani ya shilingi 13,095,000,

Alisema katika kipindi hicho wamelipa mkaraba wa serikali hadi sasa, shilingi 480,000 na shilingi 39.286.50 ikiwa ni service levy ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi.

Aidha, Nkingi alisema wanadaiwa kodi ya serikali jumla ya shilingi 5,318,000 na wapo kwenye mchakato wa kulipa deni hilo.

Katibu huyo, alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya uchimbaji wa madini ya dhahabu na gharama zake kubwa za uendeshaji.

Wakati huo huo, Mrajisi wa ushirika mkoa wa Singida,Thomas Nyamba, alisema kuwa Mohammed Ally Nyalandu, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa ushirika wa Aminika.

Amewataja wajumbe wa bodi kuwa no Ana Petro, Waziri Y. Waziri, Mohammed Ally, Abdala Mohammed, Mustapha Selemani, Foloratina Yona na Fatuma Makula.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh