Zaidi ya wananchi 3000 katika eneo la Vikindu nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wamepata matibabu ya macho bure na kupewa miwani ambapo wengine zaidi ya 350 wamefanyiwa Upasuaji baada ya kubainika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho kunakosababisha kutoona Vizuri.

Madaktari bingwa kutoka nchini Pakistani chini ya taasisi ya kiislam ya International Islamic Relief pamoja na shirika la kimataifa la Al Basal kutoka nchini Jeddah Saudi Arabia wameendesha kambi ya matibabu hayo kwa siku nne.

Baadhi ya wananchi waliopatiwa matibabu ikiwemo upasuaji wameishukuru kwa msaada huo wa matibabu bure huku wananchi wengi zaidi wakijitokeza na wengine kutoa wito waongeze muda kutokana na uhitaji wa wananchi.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh