Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA wametakiwa kuacha kuendesha shughuli za kibinadamu hasa kilimo karibu na vyanzo vya maji ili kuhifadhi mazingira.

Kaimu Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini TABORA-TUWASA,Bwana CHRISTOPHER SHIGANZA amesema changamoto zilizopo katika bwawa la IGOMBE ni pamoja na watu kulima karibu na vyanzo vya maji na kusababisha kujaa kwa tope kwenye bwawa hilo.

Bwana SHIGAZA pia amesema ili kudhibiti hali hiyo TUWASA imeweka mipaka karibu na vyanzo vya maji pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi karibu na vyanzo hivyo Naye mkuu wa wilaya ya TABORA,Mwalimu QUEEN MLOZI ameagiza watu wanao jishughulisha na shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa wilaya pia amewataka viongozi kutembelea maeneo mbalimbali ili kujua matatizo yaliyopo na kuacha kufanya kazi zao wakiwa maofisini.

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya TABORA imetemelea bwawa la IGOMBE ili kukagua hali ya upatikanaji wa maji katika Manispaa ya TABORA pamoja na uhifadhi wa mazingira yanayozunguka bwawa hilo.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh