Ofisi ya madini kanda ya kaskazini imetoa ufafanuzi kufuatia uvumi wa wizi wa madini ya Tanzanite katika mgodi wa Tanzanite One Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambapo imesisitiza kuwa hakuna madini yaliyoibwa.

June 21 mwaka huu ndio tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya tetesi kuzagaa kuwa kuna utoroshaji wa madini hayo hali iliyokilazimu kituo hiki kutafuta mamlaka husika kubaini ukweli wa jambo hili na kujua mbichi na mbivu tukapiga hodi kwa Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Adam Juma akiwa ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za madini yote katika ukanda huu.

Kituo hiki hakikuishia hapo kinafika mbali zaidi ili kujiridhisha na hali ya ulinzi na utaratibu mzima wa uingizwaji wa madini katika mgodi wa madini ya Tanzanite One hususani chumba maalumu cha uchambuzi kutoka mgodini na baadae utunzwaji wa madini hayo.

Kufuatia tetesi za kila mara za wizi na utoroshwaji wa madini Msaidizi wa Kamishna wa madini kanda ya kaskazini,mhandisi Adam anatoa maelekezo ili kuondoa sintofaham hii.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh