Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameipongeza Safari Redio kwa niya yao Thabiti ya kuwasaidia wanawake na watoto kupitia vipindi vyao vya kijamii hali iliyo mpa faraja ya kutembelea Redio hiyo.

Waziri Mwalimu ameyabainisha hayo wakati akizungumza katika kipindi maalumu kilicho rushwa mchana wa leo wa (Novemba 21 2016) Redio Safari 89.9 Mtwara, ambapo amesema kuwa amefarijika kufika katika studio za Redio hiyo.

Amesema kuwa Safari Redio kama wadau wakubwa wa Maendeleo ya jamii, ina wajibu mkubwa kama unao fanywa sasa hivi na Redio hiyo na waendelee kuhabarisha na kuelimisha Jamii husika ili watambue umuhimu wa kujali afya zao kwa kulipia huduma za matibu kupitia CHF.

Aidha Waziri Mwalimu amezungumzia mpango wa Tumaini la mama wenye dhamira ya kumpatia huduma bora mama mjamzito na watoto, ambao ulikuwa unazinduliwa leo katika viwanja vya mashujaa manispaa ya Mtwara Mikindani.

Kupitia Mpango huo unao husisha mikoa ya Lindi na Mtwara Mh waziri amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa kati ya wanawake 100 kuna wanawake 30 wanapewa ujauzito wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.

Aidha kupitia Mradi huu kuna fedha zitatolewa za huduma za akina mama wajawazito na vifaa vya kujifungulia .

Aidha kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Nanyamba Abdallah Dadi Chikota amesema kuwa kupitia Mpango huu wananchi wa Jimbo lake la Nanyamba watanufaika na Mpango huu wa Tumaini la mama, na watanufaika kupitia fedha hizo zinazo tolewa kwa ajili ya huduma za afya na vifaa hivyo.

Mh Chikota amesema kuwa katika jimbo lake kuna changamoto kubwa za uhuduma za fya hususani upungufu wa vituo vya afya, hivyo mpango huo utakuwa mkombozi kwao.

Pia Mbunge huyo ametoa wito kwa wananchi wake kuchangia huduma ya matibabu kupitia mpango wa CHF wakati huu ambao wanapata fedha za malipo ya mauzo Korosho.

0768671579

Add comment


Security code
Refresh