blog category

WANANCHI WA MIKINDANI WAMLILIA MBUNGE WAO

Wakazi wa Tarafa ya mikindani ambao wanatumia kituo cha Afya mikindani wamemuomba mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Maftaha Nachuma kuwatatulia kero wanazo zipata katika kituo hicho cha afya ikiwemo ujenzi wa uzio na umeme.

Kero hizo wamezitanabaisha mapema hii leo walivyotembelewa na Mbunge huyo ambaye aliambatana na mbunge wa viti maalum (CUF) wa mkoa wa Mtwara Shamsia Mtamba, kwa Dhamira ya kuziangalia changamoto zilizopo katika kituo hicho cha Afya na kukabidhi vyandarua 20.

Miungoni mwananchi hao ni pamoja na Athumani Salumu Chibwana ambae amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya umeme, ulinzi kwa sababu ya kukosa uzio katika kituo hicho cha afya, na uhaba wa watumishi.

Mh Nachuma amewahakikishia wananchi hao kuwa cahangamoto hizo atazifanyia kazi na kuhakikisha wanapata huduma nzuri ya Afya, huku akiahidi kukutana na wadau mbalimbali wa afya na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuhakikisha wanamaliza changamoto hizo.

Aidha amesema kuwa wako mbioni kuhakikisha wanajenga jengo la kupumzikia wagonjwa katika kituo hicho cha afya kupitia Fedha za Mfuko wa Jimbo.

Kwa Upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Shamsia Mtamba amesema kuwa ameguswa na ameumia baada ya kuona adha wanayo ipata wagonjwa katika kitua hicho cha afya hususani akina mama, huku akiahidi kushirikiana na Mbunge wa jimbo hilo kutatua changamoto zilizopo katika kitua hicho .

Katika hatua nyingine Bi Mtamba ametumia Fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuweza kusaidia kutatua changamoto hizo.

Modestus Mrope ni Mganga mfawidhi wa kituo hicho ametoa shukrani kwa kutembelewa na wabunge hao na ametolea ufafanuzi wa baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa watumishi hali inayopelekea kuhelemewa na wagonjwa.

Ikumbukwe kuwa kituo hicho cha Afya kina wakunga Saba, wauguzi 12 na Madaktari wawili 2 lakini kwa sasa amebakia mmoja na mwingine yuko Likizo hali inayo wakwamisha kuhudumia kwa wakati.

RC MTWARA AOMBA BARAKA ZA WAZEE KUHARAKISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa aomba kupata ushirikiano na ameahidi kutoa bagua watu kwani serikari ya awamu ya tano imejikita kuwahudumia wananchi bila kujali duni au kabila chama cha siasa.

Amesema hayo hapa jana alipokutana na wazee wa mkoa wa mtwara ili kupata maoni au na changamoto zinazowakabili,na baadhi ya changamoto zilijibiwa hapohapo pia ameahidi kukutana na wazee hao kila baada ya miezi sita na watapata majibu ya mambo ambayo waliuliza kama yamefanyiwa kazi .

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani bi Beatrice Dominiki amesema kuwa halmashauri ya Mtwara inaendelea kutoza ushuru kwa wafanyabiasha ili kuendesha huduma ya utoaji taka sokoni,usafishaji ya soko pamoja na vyoo.

Aidha wazee waliohudhuria kikao hicho na mkuu wa mkoa wamesema kuwa wanapata changamoto kubwa katika kipindi hichi ambacho wameuza korosho pindi waendapo benki kufata pesa zao moja ya changamoto ni kucheleweshewa malipo yao pindi wanapokuwa kutopata ushirikiano wa kutosha.

kwa upande wa mabenk wamekiri changamoto hizo na kuahidi mbele ya m,kuu wa mkoa kutoa huduma bora hasa kwa wazee,wajazito na watu wenye mahitaji maalumu pindi wanapoenda benki pia wameshauri wazee kutotoa pesa zote benki pindi wanapopata malipo ya korosho ili kuzuia kuibiwa pia kuweka akiba.

WANASAYANSI WADAI ZIWA VICTORIA LIPO HATARINI KUKAUKA

Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa.

Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.

Jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.

DK. KIGWANGALLA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA NATA,NZEGA AAHIDI USHINDI KWA CCM

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amemnadi mgombea nafasi ya Udiwani Ndugu John Cheyo Mabonde katika uchaguzi mdogo kwenye Kata ya Nata iliyopo katika jimbo hilo la Nzega Vijijini huku akiwaahidi wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na wananchi kuwa wataibuka na ushindi wa kimbunga.

Akiwa katika Kitongoji cha Udutu, Kijiji cha Mwamalulu Kata hiyo ya Nata, Dk. Kigwangalla aliweza kumnadi Mgombe huyo wa Udiwani ambapo aliwataka wananchi wa Kata hiyo kujitokeza kwa wingi kumpigia kura za NDIYO ili aweze kushinda nafasi hiyo ili kumuongezea Rais Magufuli watendaji wa kumsaidia kumletea maendeleo ikiwemo Uchumi.

“Nawaombeni sana, siku ya Jumapili wananchi kujitokeza kwa wingi sana na kuichagua CCM kupitia mgombea wake Bwana John Cheyo Mabonde ili awe Diwani wa Kata hii ya Nata. Kura zenu zitasaidia chachu ya maendeleo kwa Kata hii pamoja na jimbo kwa ujumla na kufanya itimie ile namba tatu! Yaani Rais wa CCM Mh.Magufuli, Mbunge wa CCM, Mimi Kigwangalla na Diwani wenu Mabonde.” Alisema Dk.Kigwangalla wakati akimnadi Mgombea huyo wa Udiwani Bwana Mabonde.

Aidha, Dk.Kigwnagalla aliongeza kuwa, CCM itapata ushindi wa kishindo kwani kwa sasa wapinzani wamekosa mwelekeo na wameamua kurudi CCM kwa kuunga juhudi za Rais Magufuli.

“Kwa sasa historia imeandikwa. Hii ni kwa kura zenu wana Nzega. Muliichagua mimi kuwa Mbunge wenu kwa tiketi ya CCM na Rais akanipa nafasi ya Unaibu Uwaziri ndani ya miaka miwili akanipa tena nafasi ya Uwaziri ili ni jambo la kubwa sana kwani ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wanaNzega na sasa yametimia. Kwa kulipa shukrani hizi ni kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi CCM” Alimalizia Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mgombea wa Udiwani huyo Bwana Mabonde wakati wa kutoa sera zake, aliweka wazi kuwa, amejipanga kumsaidia Rais Magufuli katika vita mpya ya Uchumi aliyoianzisha.

“Naombeni kura ilikuwasaidia Wananchi wenzangu wa Nata. Kura zenu zitaongeza chachu ya kumsaidia Rais Magufuli katika uchumi ambao unaanzia chini ngazi ya mwananchi mmoja mmoja hadi juu. Vita hii ya kiuchumi ni yetu sote. Tuwapuuze wapinzani wanaopita huku kwani tunaanza kuwashuhudia wakihama vyama vyao na kuungana na CCM.” Alieleza Mgombea huyo wa Udiwani Bwana Mabonde.

Pia alimshukuru Mh Mbunge kwa kuendeleza utekelezaji wa ahadi yake ya kusaidia wananchi ikiwemo Kata hiyo na Kata zingine ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini ambapo alisema atashirikiana nae bega kwa bega katika kufanikisha jimbo hilo linaendelea kubaki mikononi mwa CCM vipindi vyote.

Kampeni hizo zitaendelea mpaka Novemba 25 jioni ambapo siku ya Jumapili ya Novemba 26 ndipo kutafanyika uchaguzi rasmi.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo wa awali kufariki dunia hivyo nafasi kuwa wazi kwa muda mrefu.

MEYA AWEKA WAZI ALLICHOAMBIWA POLISI

Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia CHADEMA Jacob Boniface ambaye jana alishikiliwa na polisi, ameweka wazi sababu ambayo jana ilimsababishia kukamatwa na jeshi la Polisi na kulala ndani, huku uchaguzi ukiendelea.

Akizungumza na mwandishi wa Safari Media Meya Jacob amesema yeye alikuwa ni msimamizi wa vituo vya kupigia kura ambayo ipo kisheria, lakini baada ya muda alishangaa kuona polisi wanakuja kumkamata kwa tuhuma ambazo hazikuwa za kwlei.

“Nilikuwa nasimamia uchaguzi kama msimamizi wa uchaguzi wa chama changu, nikiwa kituoni nashangaa kuona nakuja kukamatwa na polisi, nilipofika kule wakaniambia kuwa wamepata taarifa kwamba nimejipanga kufanya vurugu na wenzangu, kitu ambacho sio kweli”, amesema Jacob Boniface.

Meya huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi machachari wa CHADEMA amesema mpaka sasa hajajua hatma yake kama anapelekwa mahakamani au la, kwani aliachiwa huru majira ya saa saba usiku baada ya kulipa dhamana, huku uchaguzi ukiwa umeshakwisha.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO AWATAKA WAFANYABIASHARA KUUZA MBOLEA KWA BEI ELEKEZI

Makatibu tawala kote nchini wametakiwa kutafiti na kubaini wafanyabiashara wadogo wa mbolea wanaokiuka bei elekezi kutokana na wafanyabiashara wakubwa kuwauzia wafanyabiashara hao wadogo kwa bei elekezi ya rejereja badala ya bei ya jumla.

Mwito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza kati ya mikutano saba (7) katika Kanda saba (7) za kilimo nchini inayotegemewa kufanyika ambao ni muhimu kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wa kuelimishana kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi.

Mhe Naibu Waziri wa Kilimo aliwasihi Makatibu Tawala hao wa Mikoa na wataalamu wa kilimo kuhakikisha kwamba wanasimamia bei elekezi ya mbolea, Wanatoa Elimu kwa Wakulima ili wanunue mbolea bora na pia kuimarisha vikundi vya wakulima ili waweze kutumia nguvu ya umoja katika kuboresha kilimo kwa ajili ya utoshelevu wa mahitaji ya kaya zao na kuuza ziada hapa nchini na nchi za nje.

Alisema kuwa wafanyabiashara licha ya kufahamu kuwa wanatakiwa kugawana faida na wauzaji wa rejareja lakini bado wanakiuka taratibu za kisheria hivyo aliwaagiza kuacha tabia hiyo ili mawakala wauze kwa rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao.

Alisema Katika Sekta ya Kilimo mbolea ni moja ya pembejeo zinazohitaji ushirikiano mkubwa kutokana na ukweli kwamba inahitajika kwa wingi na ina gharama kubwa, inahitaji utaalamu katika matumizi yake na kwamba ni bidhaa inayoharibika kwa haraka endapo viwango vya utunzaji wake havizingatiwi.

Mhe Mwanjelwa aliwaagiza wakaguzi wote wa mbolea nchini kufuatilia na kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara wa mbolea ana leseni ya kufanya biashara ya mbolea ambayo itatolewa bure na TFRA na pia wahakikishe kwamba wote wamepata mafunzo haraka iwezekanavyo.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa Wizara ya kilimo ilitunga Kanuni ya Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer Bulk Procurement Regulations) na kuzitangaza kwenye Gazeti la Serikali kupitia tangazo G.N. 49/2017.

Pamoja na kuunda kanuni hizo, Wizara ya kilimo ilirekebisha Kanuni ya Mbolea ya mwaka 2011 kwa Kanuni zilizotangazwa katika Gazeti la Serikali kwa tangazo G.N. Na. 50/2017 ili kuipa nguvu TFRA kukokotoa, kutangaza na kusimamia bei elekezi ya mbolea.

Aliwaagiza pia wafanyabiashara wanaotunza mbolea bila kuzingatia viwango vilivyowekwa na TFRA kuacha haraka tabia hiyo kwani kwani wanasababisha mbolea kumfikia mkulima ikiwa imepungua ubora au kuharibika kabisa na hivyo kumfanya mkulima asipate tija inayotokana na matumizi ya mbolea.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amewataka wataalamu hao Kutenda haki katika uwajibikaji wao, Kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, uwajibikaji uliotukuka, na nidhamu ya hali ya juu.

Aliongeza kuwa kwa yeyote atakaye kwenda kinyume na matakwa ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.

KIKWETE AFUNGUKA KUHUSU UCHAGUZI MDOGO

Mbunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CMM Mh. Ridhiwani Kikwete ameeleza kutofurahishwa na vitendo vya uvunjivu wa amani na migawanyiko, vilivyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa madiwani nchini uliofanyika jana.

“Siasa ya uchaguzi haipaswi kuwa mwanzo wa migawanyiko, mbegu tunayopanda leo kama haikukemewa itakuja kutusumbua siku sijazo, niwaombe Watanzania wenzangu, tudumishe upendo na tukatae fujo zisizo na lazima”, amesema Ridhiwani.

Aidha Ridhiwani ametoa ushauri unaolenga kuondoa visingizio na propaganda za kutumia wanachama kama ndio sehemu ya vurugu hizo akidai kuwa wafanya vurugu hao ni wananchi na sio CCM wala CHADEMA kama ambavyo kila upande unadai.

“Wanaopigana ni wananchi, sio CCM wala CHADEMA, maana naona pande zote zinalalamika, tuwe na hukumu sahihi, la msingi tukatae fujo, nchi hii ni muhimu na tuenzi mawazo sahihi ya wazee wetu”, ameongeza Ridhiwani.

Wananchi katika Kata 43 za mikoa 19 nchini kote jana wamepiga kura kuchagua madiwani katika uchaguzi mdogo ambapo vitendo kadhaa vya vurugu viliripotiwa kutokea huku CHADEMA ikijitoa kushiriki uchaguzi huo katika kata 5 za wilaya ya Arumeru.

JTI YATOA VIFAA TIBA TABORA

Kampuni ya Japan Tobacco International (JTI) imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 13.5 kwa Zahanati ya Kijiji cha Usindi wilayani Kaliua kwa ajili ya uboreshaji wa huduma matibabu kwa wakazi wa eneo hilo.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vitanda vya wagonjwa, vitanda kwa ajili ya wakina mama kujifungulila, darubini za kuchunguzia magonjwa, viti vya wagonjwa na mizani ya kupimia uzito.

Akipokea msaada huo jana katika Kijiji cha Usindi kwa niaba ya wakazi wake , Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha huduma kwa mama wajawazito, huduma za uchunguzi wa magonjwa na kuongeza ufanisi wa kazi kwa wataalumu wa Zahanati hiyo.

Alisema kuwa uwepo wa vifaa utasaidia sio tu kutoa huduma kwa wakazi wa Kijiji hicho pekee hata majirani na wapiti njia ambao watahitaji huduma ya dharura.

Busalama alisema kuwa wakazi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakilazimika kutembelea umbali mrefu kutafuta matibabu, kwa hiyo msaada huo utawasidia kuwapunguzia wakazi wa Kijiji hicho kwenda mbali kutafuta huduma za kiuchunguzi.

Aliishukuru Kampuni ya JTI kwa juhudi zao za kutumia sehemu ya faida wanayopata kutokana na ununuzi na uuzaji wa tumbaku na kuamua kurudisha kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali inayolenga kuondoa matatizo kwao.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ya Kaliua aliwapongeza viongozi wa Chama cha Msingi cha Usindi AMCOS kwa uaminifu wao ambao kupitia Chama hicho umewezesha Kampuni ya JTI kuamua kutoa msaada kwa Zahanati ya Kijiji hicho.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Aristides Raphael alisema msaada huo walioupata utasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Zahanati hiyo na kuahidi kupeleka mtaalamu wa maabara ili wakazi wa hapo waanze kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa.

Alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakazi wa Kijiji hicho kutotembea umbali mrefu kutafuta huduma za uchunguzi wa kimaabara kwa baadhi ya magonjwa na badala yake watapata palepale.

Naye Mwalikilishi wa Kampuni ya JTI Ally Kalugala alisema kuwa vifaa walitoa kwa ajili ya Zahanati ya Usindi ni sehemu ya mpango wao wa kushirikiana na wakulima ambao wamekuwa wakifanyakazi nao katika kuhakikisha kuwa wanashiriki vizuri katika uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Alisema kuwa wataendelea kutoa misaada kwa wakulima ambao wa kijiji cha Usindi na maeneo mengine katika kusaidiana katika utatazi wa matatizo mbalimbali yanawakabili na kupunguza juhudi zao za kujikwamua na umaskini.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Usindi AMCOS Mikidadi Mustapha alisema kuwa wamekuwa na mahusiano mazuri na Kampuni ya JTI na uzalishaji umekuwa ukiongezeka kila mwaka.

Alisema kuwa ushirikiano huo ndio umepelekea kuwa na mazungumzo na Kampuni hiyo kwa ajili ya kuomba msaada wa vifaa ambapo hatimaye wamepatiwa vifaa kwa ajili ya Zahanati ya Kijiji.

“Ni washukuru sana JTI kwa kuwa hii sio mara ya kwanza kwenu kusaidia jamii mnayoshirikiana nayo …ni hivi karibuni mlikabidhi kisima chenye uwezo wa kuzalisha lita 7000 , hii ni ishara kuwa mnashirikiana vizuri na wakulima ambapo wafanyia kazi zenu” alisema Busalama.

Page 5 of 168